Serikali
ya Marekani imewataka viongozi wa bara la Afrika kuheshimu tofauti za
kisiasa zilizoko nchini mwao na kuwa na uvumilivu wa kisiasa ambao
ndio nguzi kuu ya kuwa na demokrasia ya kweli katika kufikia
mafanikio ya muda mrefu.
Rais Obama amewataka ma rais walipo madarakani bara Afrika kuheshimi muda waliopewa na katiba kukaa madarakani
Rais Obama amewataka ma rais walipo madarakani bara Afrika kuheshimi muda waliopewa na katiba kukaa madarakani
Wito
huu umetolewa wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya viongozi hao na
rais Barack Obama, ambaye alitumia siku ya kwanza ya mkutano huu,
kusisitiza masuala ya usalama, biashara na demokrasia kama msingi
mkuu utakaoshuhudia nchi za Afrika zikipata maendeleo ya haraka.
Kuhusu
biashara, rais Obama amesema kuwa haoni shida nchi ya China kuwa
mwekezaji mkubwa barani Afrika lakini akaonya kuhusu uwekezaji
unaofanywa na taifa hilo na kuwataka viongozi hao kuwa makini na
rasilimali ambazo China imekuwa ikizilenga kwenye bara hilo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire