Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametoa wito wa kukomeshwa kwa
mashambulizi na mauaji dhidi ya raia wa kigeni tatizo ambalo
linaonekana kuendelea kusambaa nchini humo.
Wimbi
hilo la mashambulizi na mauaji dhidi ya raia wa kigeni linaonekana
kukithiri nchi Afrika kusini ambapo mpaka sasa watu wasiopungua sita
wameuawa.
Rais
Jakob Zuma amesema kuwa taifa limeshudia matukio ya kutisha na
kwamba haikubaliki raia wa kigeni kushambuliwa na kuuawa wakati
hawana hatia na hawastahili kufanyiwa unyama.
Zuma
ameeleza kuwa polisi wamesambazwa katika maeneo mbalimbali ili
kuwalinda raia wa kigeni na kuwakamata watekelezaji wa mashambulizi
na mauaji hayo.
Amesema
kuwa hakuna kosa lolote linaloweza kuhalalisha mauaji na kuharibiwa
kwa mali za watu hao na kuongeza kuwa serikali yake itafanya kila
linalowezekana kukomesha hali hiyo.
Wiki
mbili zilizopita maduka na nyumba zinazomomilikiwa na raia wa kigeni
kutoka nchi za Somalia, Ethiopia, Malawi na nchi nyingine
zilizingirwa mjini Durban na familia kulazimishwa kuondoka.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire