Serikali
ya Burundi imetishia jana kulitumia jeshi iwapo maandamano ya kupinga
muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza yatagubikwa na ghasia wakati
huu nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais.
Waziri wa
ulinzi nchini humo jenerali Pontien Gaciyubwenge amesema iwapo
itahitajika na kamanda wa majeshi ambae ni rais wa jamuhuri jeshi
lake litajiunga na vikosi vingine katika swala zima la ulinzi dhidi
ya wanataka kuyumbisha amani.
Upande
wake waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana amesema vikosi vya
Usalama na utawala vipo makini na vitachukuw ahatuwa stahiki ili
kuwafikisha mahakamani wahusika wote wa maandamano.
Hayo
yanajiri wakati huu wanasiasa wa Burundi waliokimbilia ugenini
wakimtaka rais Nkurunziza kutumia uamuzi wa busara na kutowa uhuru
kwa wote kwa ajili ya maandalizi thabiti ya uchaguzi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire