Pages

lundi 20 avril 2015

MONUSCO YAITAKA SERIKALI YA RDCONGO KUANDAA MAZINGIRA MAZURI YA KISIASA KUELEKEA UCHAGUZI

Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kudhaminia usawa baina ya wanasiasa, mashirika ya kiraia, pamoja na watetezi wa haki za binadamu wakati huu taifa hilo likielekea kwenye chaguzi mbalimbali zitazo tamatishwa na ule wa Rais hapo Novemba mwaka 2016.

Akizungumza katika mahojiano na shirika la habari la Ufaransa AFP, mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Martin Kobler amesema ni muhimu kutowa nafasi kwa vyama vyote vya kisiasa, mashirika ya kiraia, wanaharakati wanaotetea haki za binadamu na kwamba wanawasiliana na serikali kuhakikisha hatuwa hii muhimu inakuwepo.

Martin Kobler amesema jukumu la Monusco ni kutetea pia haki za binadamu, na hili sio swala la kuingilia ndani maswala ya serikali bali ni kuomba haki za binadamu ziheshimishwe.

Wachambuzi wa siasa wanaonakuwa wito huo umekuja wakati muafaka, licha ya kudorora kwa ushirikiano kati ya mashirika ya kiraia na serikali katika siku za hivi karibuni

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...