Serikali
ya Ethiopia imelaani vikali mkanda wa Video uliochapishwa na kundi la
Islamic State ukionyesha watu 28 wakiuawa kwa kukatwa vichwa na
ambao waliwasilishwa na kundi hilo kama raia wa Ethiopia.
Mbali
na Ethiopia, serikali ya Marekani pia imetowa taarifa ambamo pia
imelaani mauaji hayo ambayo imeyaita ya kinyama.
Kundi
hilo la IS kitengo cha Libya limeoyesha mkanda huo ikiwa ni miezi
miwili baada ya kuonyeshwa kwa mauaji mengine ya watu 21 wachristo
waumini wa Copte kutoka Misri, hali iliozua ghadhabu kwa serikali ya
Misri iliojibu tukio hilo kwa mashambulizi ya kijeshi katika ngome za
kundi hilo nchini Libya
mkanda
huo wa video wenye dakika 29 inaonyesha makundi mawili ya watu
waliowasilishwa kama waumini wa kanisa la Ethiopia ambalo wamesema ni
adui.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire