Upinzani nchini Burundi imetowa wito wa maandamano tena
leo Jumatatu April 20 mwaka 2015 katika jiji kuu la Bujumbura. Wito
huu umetolewa na mmoja kati ya viongozi wa upinzani wa chama cha
UPD-Zigamibanga Chauvino Murwengezo ambae amewataka wafuasi wa
upinzani na wale wote wanaopinga muhula wa 3 wa rais Pierre
Nkurunziza.
Hayo yanajiri wakati mwishoni mwa Juma mahakama kuu
jijini Bujumbura ikiwafungulia Mashtaka waandamanaji 65 waliokamatwa
wakati wa maandamamno ya kumshinikiza rais Piere Nkuzrunziza
kutowania urais kwa muhula wa tatu.
Siku ya Ijumaa juma lililopita shughuli zilizorota
kutokana na vurugu za maandamano ambapo Polisi wa Usalama
waliwasambaratisha waandamanaji ambao walidai kuandamana kwa amani na
utulivu.
Kidole cha lawama kinaelekezwa kwa vyombo vya Usalama
nchini humo ambavyo vimeonekana kuegemea upande mmoja, kwani wafuasi
wa rais Nkurunziza wanaounga mkono muhula wa 3 wanapoafanya
maandamano hupewa ulinzi mkali wa polisi.
Kiongozi mmoja wa upinzani amesema iwapo machafuko
yatatokea au vurugu, zinasababishwa na polisi na wao ndio wataulizwa
kupitia viongozi wao ambao hawataki kutowa haki sawa kwa wote.
Hali hii ya wasiwasi inayo shuhudiwa kwa sasa nchini
Burundi imesababisha watu zaidi ya elfu nane kukimbilia nchini
Rwanda na DRCongo kwa hofu ya kuzuka kwa machafuko.
Upinzani pamoja na Mataifa ya Magharibi yanamtaka rais
Nkurunziza kuheshimu katiba na kutowania wadhifa huo wakati wa
Uchaguzi wa urais mwezi Juni.
Nkurunzinza mwenyewe hajajitokeza na kutangaza ikiwa
atawania au la.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire