Makam
wa rais wa zamani nchini Burundi Frederick Banvuginyumvira ambae pia
ni naibu mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Sahwanya Fredebu,
amesema maandamano ya amani yanayoandaliwa na waziri wa mambo ya
ndani Edouard Nduwimana ni kampeni tosha za kisasa za chama cha
CNDD-FDD.
Banvuginyuvira
amesema waandamanaji wanaondamana kwa ajili ya amani hawawezi kuimba
na kutowa wito wa kumchaguwa Nkurunziza huku wakionyesha picha yake
pamoja na ujumbe wanaotowa wa vitisho dhidi ya wanasiasa wa upinzani
na wanaharakati wa mashrika ya kiraia.
Makam
huyo wa rais wa zamani ameitaka tume ya uchaguzi kutoendelea kukaa
kimya kiasi cha kuonekana kwamba inaunga mkono hali hiyo, amewataka
pia viongozi wakuu wa serikali kutafuta suluhu ya matatizo ya warundi
na sio kuendelea kuwatumia wananchi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire