Pages

vendredi 27 février 2015

OMAR AL BASHIR NIPO TAYARI KUNG'ATUKA NIKIANGUKA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA RAIS


Rais wa Sudani Omar Hassan Al Bashir anaewania uchaguzi mkuu wa rais unaotarajiwa kufanyika April mwaka huu nchini humo amefahamisha jana kwamba ataachia ngazi iwapo atashindwa kwenye uchaguzi huo uliosusiwa na vyama vikuu vya upinzani.

Akiwa katika kampeni za uchaguzi zilizoanza juma hili katika mji wa Wad Madani kusini mashariki mwa Karthoum, Bashir amesema yupo tyari kujiuzulu kupitia kura katika uchaguzi wa rasis na wa bunge unaotarajiwa kufanyika April 13.

rais Bashir amesema raia ndio wanaojukumu la kuamuwa nani awaongoze kupitia kura. Bashir mwenye umri wa miaka 71 mgombea uraia kwa tikiti ya chama cha National Congress amewatuhumu viongozi wa upinzani kususia uchaguzi na kwamba hakuna nafasi kwa watu ambao wanataka kuongoza nchi kupitia shinikizo ya mataifa ya magharibi kwa kwenda Addis Abeba au Paris.

Vyama vikuu ya upinzani na waasi vilitiliana saini ya kususia uchaguzi huo jijini Adis Abeba nchini Ethiopia na Paris.

mercredi 25 février 2015

ULISHAWAHI KUISKIA HII HAPA ?


Mfano wa Keki ya Birthday

Wataalamu wa kutengeneza keki wanajiandaa kwa shughuli ya utengenezaji wa Keki ya Birthday ya miaka  450 ya jiji la Rio nchini Brezil, itayokuwa na mita 450, ndani yake itakuwa tani 2.5 ya unga wa ngano, tani 2,1 ya sukari, tani 1, 5 ya margarine, yai mia tatu, lita 1000 ya maziwa na mazaga zaga mengine.

Keki hiyo ya mita 450 itawekwa kwenye barabara ya Carioca mjini kati siku ambayo wananchi watakuwa wanasherehekea miaka 450 ya jiji hilo March Mosi mwaka huu, na ambapo kila aliehudhuria sherehe hizo atatakiwa kuhonja.

Mea wa jiji la Rio tayari ametowa kitita kinachokadiriwa kufikia Euro elf 31 kwa ajili ya manunuzi ya vifaa juu ya kutengeneza keki hiyo kubwa kuwa kutengenezwa duniani

MAREKANI YASHINIKIZA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA KUIWEKEA VIKWAZO VYA SILAHA SUDANI KUSINI


Marekani imewasilisha kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mapendekezo ya vikwazo kwa viongozi wanaohusika na mzozo nchini Sudani Kusini inayokabiliwa kwa sasa na mzozo wa kivita na mauaji ya kikabila yanayoendelea kushuhudiwa.

Muswada huo unaagiza vikwazo kwa viongozi walengwa wa moja kwa moja, kuziuia mali zao, na kuwanyima haki ya kusafiri wale wote wanaotishia amani na utulivu, na wanaozuia misaada kuwafikia walengwa nchini humo.

Mbali na vikwazo hivyo kwa viongozi husika na mzozo nchini Sudani Kusini, Marekani inapanga pia kulishinikiza baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuiwekea vikwazo vya silaha nchi hiyo. Umoja wa Ulaya unaunga mkono mapendekezo haya.

Hata hivyo viongozi wa mrekani wamegawanyika kutokana na pendekezo hilo, upande mmoja unaunga mkono pendekezo hilo, huku mwingine ukiona kwamba vikwazo vya silaha vitamdhoofisha zaidi rais Salva Kiir dhidi ya mpinzani wake Riek Mashar.

MTOTO MDOGO AFARIKI WENZIE TAABANI BAADA YA MAMA KUPULIZIA DAWA YA KUUWA WADUDU NDANI


Mtoto mmoja kichanga amepoteza maisha nchini Canada huku ndugu zake wengine wanne wenye umri kati ya miaka 2 na 7 wakiwa katika hali mahtuti baada ya mama yao kupulizia dawa ya kuuwa wadudu ndani ya nyumba, dawa ambayo inadaiwa kuwemo sumu.

Duru kutoka kwa mmoja wa familia hiyo ameeleza kwamba mama huyo alitumia dawa hiyo kutoka nchini Pakistan ili kuuwa wadudu waliokuwa wameshambulia nyumba hiyo, bila hata hivyo kujuwa kwamba inasumu ndani yake.

Habari zaidi zinaeleza kuwa dawa hiyo hutumiwa katika sekta ya kilimo kwa ajili ya kulinda mbolea katika ghala baada ya kukaa kwa muda mrefu. Mtoto huyo mchanga alifariki muda mfupi tu baada ya kufikishwa hospitalini.

BARAZA LA SENETI NCHINI BURUNDI LAIDHINISHA MAJINA YA VIONGOZI WA IDARA YA UPELELEZI


Baraza la Senet nchini Burundi, limeidhinisha majina ya viongozi wa idara ya upelelezi yaliowasilishwa na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ikiwa ni miezi kadhaa kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais.

Rais Nkurunziza amemteuwa Brigadia jenerali Etienne Ntakarutimana anaelezwa kuwa mtu muaminifu kwake na ambae ameidhinishwa na barazala Seneti bila pengamizi baada ya kuchaguliwa na wajumbe 37 dhidi ya 37 waliokuwepo bungeni.

Jenerali Ntakarutimana mwenye umri wa miaka 43 ni mionogni mwa viongozi wa kundi la waasi zamani wa CNDD-FDD lililoongozwa na rais Nkurunziza ambalo liligeuka kuwa chama madarakani kwa sasa, aliwahi kuongoza idara ya ujasusi katika jeshi la Burundi.

Mtangulizi wake aliekalia nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu, brigadia jenerali Godefroid Niyombare pamoja na mkuu wa itifaki kwenye idara hiyo walifutwa kazi pamoja na mkuu wa usalama wa ndani. Kisa na mkasa chaelezwa ni baada ya viongozi hao kumshauri rais Nkurunziza kutowania muhula mwingine watatu katika uchaguzi mkuu wa Juni.

Kwa sasa inaelezwa kwamba rais Nkurunziza amemteuwa mtu muaminifu kwake ambae atakuwa na kibarua kigumu cha kusimamia usalama wakati rais Nkurunziza atapotangaza kuwania urais kwa muhula wa 3 na kukabiliana na matukio yatayo tokana na hatuwa hiyo, hususan maandamano.

Rais Nkurunziza hajatangaza rasmi kuwania muhula wa 3, lakini kumekuwa na dalili tosha zinazoonyesha kwamba anania ya kugobmea kwa mara ya 3, jambo ambalo lipo kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Mbali na upinzani nchini humo unaopinga hatuwa hiyo ya kuwania muhula wa 3, rais Pierre Nkurunziza anakabiliwa pia na upinzani wa ndani katika chama chake, ambapo wapo viongozi ambao wamemtaka atowe nafasi kwa mtu mwingine.

mardi 24 février 2015

MZOZO WAIBUKA KATIKA CHAMA FNL, JAQUES BIGIRIMANA AMFUTA UADHIFA WAKE KATIBU MKUU WA CHAMA HICHO


Emmanuel Miburo
Kamati ya watu 27 wanaotaka matawi ya chama cha FNL kuungana na kuwa kimoja, yamewataka Agathon Rwasa kuwa mwenyekiti wa FNL huku Jacques Bigirimana akiwa makam wake ili kuunda nguvu moja kwa ajili ya Uchaguzi.

Emmanuel Miburo katibu mkuu wa tawi la FNL ya Jacques Bigirimana linalo tambulika na serikali, amesema kamati ya watu 27 ambao wengi wao walikuwa ni kutoka tawi la Jacques Bigirimana na wajumbe 18, huku wengine 9 wakiwa ni kutoka tawi la FNL ya Agathon Rwasa.

Emmanuel Miburo amesema kamati hiyo ilifanya tathmini na kuomba muungano,lakini kwa mshangao mkubwa mwenyekiti Jacques Bigirimana hakutaka hata kusikiliza yaliomo katika ripoti hiyo ya kamati ilioundwa kwa kiasi kikubwa na wajumbe wa tawi lake.
Jacques Bigirimana

Kulingana na ripoti ya kamati hiyo, inaagiza viongozi hao kuunda kamati ya mseto na kuandaa kongamano March Mosi mwaka huu wa 2015 ili kuidhinisha nyadhifa mbalimbali za viongozi wa chama.

Katika majadiliano ya wajumbe wa kamati hiyo, walikuwa wamependekeza Jacques Bigirimana kuendelea kuwa mwenyekiti wa FNL, na kumteuwa Agathon Rwasa kuwakilisha chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa rais, lakini mwisho wa siku wajumbe hao waliafikiana kumteuwa Rwasa kuwa kiongozi na kuandaa kongamano March 1.

Mbali na kupinga hatuwa hiyo, Jacques Bigirimana amesema hajamtuma yeyote kumuwakilisha, na kuchukuw ahatuwa ya kumfuta kwenye uongozi katibu wake Emmanuel Miburo aliechaguliwa kupitia kongamano la chama hicho.

Agathon Rwasa
Jambo ambalo Miburo anasema Jacques Bigirimana hana uwezo wa kunfuta uadhifa kwa sababu sio yeye aliemteuwa, bali kongamano pekee la chama ndilo lenye uwezo wa kunfuta uadhifa wake, na kubaini kwamba upande wa tawi la Jacques Bigirimana, viongozi na wafuasi wote wanaridhia uwepo wa kongamano kuu la chama hicho, ispokuwa pekee Jacques Bigirimana.

lundi 23 février 2015

UBELGIJI YAITAKA DRCONGO KUKUBALI USHIRIKIANO WA MONUSCO KATIKA KUPAMBANA NA FDLR


Raymond Tchibanda na Didier Raynders
 Serikali ya Ubelgiji imemuomba rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuridhia msaada wa kijeshi wa vikosi vya kimataifa MONUSCO katika kukabiliana na waasi wa kihutu wa FDLR mashariki mwa nchi hiyo.

Ombi hilo limewasilishwa na Naibu Waziri Mkuu mwenye dhamana ya Ushirikiano na Maendeleo, Dekro Alexander na mwenzake wa Mambo ya Nje, Didier Reynders walioko ziarani mjini Kinshasa.

Katika mkutano wao na Waziri Kwa Congo Raymond Tshibanda siku ya Jumapili, mawaziri hao wamemuomba mwenyeji wao kukubali ushirikiano na msaada wa MONUSCO katika kuwasaka waasi wa FDLR, huku waziri Tshibanda akielezea uwezekano huo kwa masharti ya kuheshimu uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Juma lililopita, Joseph Kabila aliwaambia mabalozi wa kimataifa mjini Kinshasa kuwa nchi yake haiitaji tena msaada wa vikosi vya MONUSCO katika operesheni ya kuwapokonya silaha waasi hao na kukosoa tabia yao ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.

Awali MONUSCO kwa upande wake wamekataa kutoa msaada wa kijeshi kwa operesheni hiyo kufwatia uteuzi wa majenerali wawili ambao wanatuhumiwa kushiriki katika vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kuendesha operesheni hiyo.


vendredi 20 février 2015

VIONGOZI WA EAC WAKITANA JIJINI NAIROBI RAIS KIKWETE AKABIDHIWA USUKANI



Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekuwa wakikutana jijini Nairobi nchini Kenya, kujadili na kuthathmini maendeleo ya Jumuiya hiyo ikiwemo harakati za uundwaji wa shirikisho la kisiasa na matumizi ya sarafu moja.


Marais wa Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda na Uagnda wanasema juhudi kubwa zinaendelea kuwaunganisha wananchi wa Jumuiya hiyo.


Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema maendeleo ya jumuiya hiyo yanaonesha mshikamano kati ya wananchi wa nchi hizo na kuhudi za viongozi.


Hata hivyo, Rais Kikwete amesisitiza kuwa Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania mwezi Oktoba na Burundi mwezi Juni itakuwa ni kipimo cha Demokrasia katika nchi hizo mbili za Jumuiya hiyo.


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliyemaliza muda wake kama Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo naye amesisitiza umuhimu wa viongiozi wa Jumuiya hiyo kuungana kwa manufaa ya wananchi wa Jumuiya hiyo.

WATU 25 WAPOTEZA MAISHA KATIKA SHAMBULIO LA BOMU JIJINI MOGADISHU


Watu 25 wameuawa mjini Mogadishu nchini Somalia baada ya kundi la kigaidi la Al Shabab kutekeleza shambulizi la bomu katika hoteli maarufu mjini humo.

Walioshuhudia milipuko hiyo ya bomu wanasema, baada ya milipuko hiyo miwili, kulifuatiwa na ufwatulinianaji wa risasi katika hoteli hiyo maarufu ambayo pia inaelezwa ilikuwa na Mawaziri wa serikali.

Haya ndio mashambulizi mbaya kuwahi kutokea katika siku za hivi karibuni mjini Mogadushu katika nchi hiyo inayoendelea kupambana na kundi la Al Shabab linaloshrikiana kwa karibu na Al Qeada.

Ripoti kutoka katoka Ikulu ya Mogadishu imethibitsiha maafisa yaliyotokea baada ya mashambulizi hayo na kusabisha zaidi ya watu 70 kujeruhiwa.

Kundi la Al Shababa limethibitisha kuhusika na shambulizi la leo na limekuwa likijaribu kuipundua serikali Hassan Sheikh Mohamud inayotambuliwa Kimataifa.
Al Shabab imekuwa ikilenga kutekeleza mashambulizi yake katika Hoteli mbalimbali, Uwanja wa ndege na Ikulu ya Mogadishu bila mafanaikio.

Maelfu ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika wapo nchini humo kukabilianana kundi hilo la kigaidi.

JESHI LA IRAQ NA WAASI WA KIKURDI WAUNGANA KUKABILIANA NA ISLAMIC STATE



Muungano wa jeshi la Iraq na Kikurdi linaungana kuchukua tena mji wa Mosul uliodhibitiwa na kundi la Kiislamu la Islamic State.

Ripoti kutoka Marekani zinasema wanajeshi 25,000 wanaandaliwa kukabiliana na Islamic State ili kuukoboa mji wa Mosul.

Pentagon inasema operesheni hiyo huenda ukafanyika mwezi Aprili na May katika mji huo wa Kaskazini mwa Afrika ambao una kati ya wapiganaji elfu moja na elfu mbili wa Islamic State.

Mji Mosul ambao ulikuwa na wakaazi zaidi ya Milioni 2 kabla ya kutekwa na Islamic State, umebaki na watu wachache.

Wakati uo huo, wakuu wa majeshi kutoka zaidi ya Mataifa 20 wanakutana nchini Saudi Arabia kujadili namna ya kuliimarisha jeshi la Iraq kupambana na Islamic State.

Marekani juma hili ilikuwa na Mkutano wa Kimataifa kuhusu namna ya kupambana na makundi ya kigaidi na rais Barrack Obama alisema, nchi yake haikabiliani na Uislamu bali na magaidi.

ANGALIA PICHA ZA VIONGOZI WA EAC KATIKA MKUTANO WAO JIJINI NAIROBI HII LEO













WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NCHINI BURUNDI ATAHADHARISHA KUHUSU MAANDAMANO


Waziri wa mbo ya ndani nchini Burundi Edouard Nduwinama ametahadharisha hii leo kuhusu tukio lolote la kuzua vurugu nchini humo siku moja baada ya kushuhdiwa maandamano makubwa ya kumuunga mkono muandishi wa habari, na kuutuhumu upinzani kwamba unafanya kila mbimnu kuvuruga mchakato wa uchaguzi.


Hakuna takwimu kamili zilizotolewa lakini muandishi wa habari wa AFP aliekuwepo jijini Bujumbura aleza kwamba maelfu kwa ma mia ya watu walimiminika jana katika barabara mbalimbali za jiji kumpokea mkurugenzi wa kituo cha radio RPA ambae alikuwa ameachiwa huru kutoka katika jela kuu la Muramvya kwenye umbali wa kilometa zaidi ya 50 na Bujumbura.

Waziri Nduwimana amesema wanafuatilia tangu kipindi kadhaa wito unaotolewa na upinzani wa kuwataka watu kuandamana na kwamba kilicho shuhudiwa jana ilikuwa ni kipimo kwa hawa na wale kuangalia uwezekanao wa kutekeleza mpango wao.

Hata hivyo waziri Nduwimana amekiri kwamba katiba ya burundi inaruhusu watu kuandamana, lakini kilichofanyika jana amesisitiza ni uasi ulioandaliwa.

Lengo hasa la kuandaa maandamano waziri huyo wa mambo ya ndani amesema radio RPA na washirika wake wa upinzani wanalenga kuangusha taasisi za serikali na kuzuia uwepo wa uchaguzi mkuu wa rais nchini humo, na kwamba serikali haitokubali tena jambo hilo kutokea.

Wizara ya mambo ya ndani ilikuwa imekataza kufanyika kwa maandamano, lakini wananchi walitupilia mbali katazo la serikali na kuandamana kwa kishindo huku polisi wakiwaacha wananchi ambao waliandamana kwa utilivu, kabkla ya polisi kuinglia kati dakika za mwisho kwa kuwatawanya kwa kuwamwagia maji.

Joto la kisiasa limeendelea kupanda nchini Burundi wakati huu nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais Juni ijayo, hasa kuhusu hatuwa inayosubiriwa ya kujichagulisha kwa muhula wa 3 au la kwa rais wa nchi ihyo bwana Pierre Nkurunziza.

RAIS NKURUNZIZA WA BURUNDI AWAFUTA KAZI WAKUU WA IDARA YA USALAMA

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amewafuta kazi Mkuu wa kitengo cha Ujasusi Meja jenerali Godefroid Niyombare, pamoja Mkuu wa itifaki kwenye idara hiyo ya ujasusi Jenerali Léonard Ngandakumana, pamoja na mkuu wa usalama wa ndani Jenerali Sylvestre Ndayizeye hatuwa inayokuja ikiwa ni miezi mitatu tu baada ya kuteiliwa kwenye uadhifa huo.

Msemaji wa rais wa Burundi Leonidas Hatungimana hajaeleza sababu za kufutwa kazi kwa kiongozi huyo ikiwa ni miezi mitatu kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais.

Hata hivyo duru za kuaminika licha ya kukanushwa, zaelezwa kwamba hivi karibuni maafisa hao walimshauri Rais Nkurunziza kutowania muhula wa 3, kwani ni hatuwa ambayo inaweza kuitumbukiza taifa hilo katika janga la machafuko,

Inaelezwa kuwa Nkurunziza alishauriwa na maafisa wake kuwa ikiwa atatangaza kuwania, hatapata uungwaji mkono kutoka kwa wananchi na chama chake cha CNDD FDD.

jeudi 19 février 2015

ANGALIA KWA PICHA MAPOKEZI YA BOB RUGURIKA JIJINI BUJUMBURA


HALAIKI WAJITOKEZA KUMPOKEA BOB RUGURIKA JIJINI BUJUMBURA



Wakaazi wa jiji la Bujumbura wamefurika kwa wingi katika barabara za jiji hilo kumpokea mkurugenzi wa radio RPA Bob Rugurika ambae ameachihuru kwa dhamana kutoka katika jela la Mkoani Muramvya kwenye umbali wa kilometa zaidi ya 60 na jiji la Bujumbura. Imekuwa vigumu kukadiria idadi kamili ya umati huo uliojitokeza kuimba kucheza na kuonyesha furaha yao.

Hapo jana usiku polisi kutoka jijini bujumbura ilikwenda kumtowa jela mkurugenzi huyo jambo ambalo alipinga katu katu akihofia usalama wake, kwani hakuna taifa lolote duniani linalo amuru mfungwa kutolewa jela Usiku.


Mahakama ya rifaa ya jijini Bujumbura iliamuru kuachiwa huru kwa dhamana kwa muandishi huyo wa habari ambae pia ni mkurugenzi wa radio moja ya kibinafasi inayo sikika zaidi jijini Bujumbura ambae anatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya watawa 3 raia wa Italia na kutiwa mbaroni tangu mwezi Januari.

Radio RPA inachukuliwa kuwa karibu zaidi na upinzani ni miongoni mwa radio zinazo sikilizwa kwa asilimia kubwa na wananchi wa Burundi. Kuzuiliwa kwa Bob Rugurika kulikosolewa vikali na wananchi wa Burundi pamoja na upinzani lakini pia mashirika ya kiraia bila kuweka kando jumuiya ya kimataifa na mashirika yanayo tetea haki za binadamu.

Mahakama hiyo inamtuhumu Bob Rugurika kutumia sauti ya mtu ambae alikiri kuhusika katika mauaji ya watawa hao watatu raia wa Italia wenye umri wa miaka 75, 79, 83 waliouawa mwezi Septemba mwaka jana Wilayani Kamenge kaskazini mwa Bujumbura. Mtu huyo anawatuhumu viongozi kadhaa wa serikali akiwemo aliekuwa mkuu wa idara ya upelelezi Adolphe Nshimirimana.

Mahakama ya Bujumbura ilimtia nguvuni mtu mmoja raia wa Kamenge kuwa ndie muhusika wa mauaji hayo. Jambo ambalo raia wa eneo hilo wanasema mtu huyo hawezi kuhusika na mauaji kwani ni mpungufu wa akili wa muda mrefu na watu wote wa eneo hilo wanamfahamu.

Yote haya yanajiri ikiwa ni siku kadhaa kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais, bunge, tarafa wakati huu joto la kisiasa likionekana kushika kasi katika nchi yenye historia ya mauaji ya kisiasa na kikabila.

Rais wa sasa Pierre Nkurunziza anatuhumiwa kuwa na mpango wa kuwania muhula wa 3, jambo ambali ni kinyume na katiba ya nchi hiyo na kuendelea kuuminya upinzani na kuwanyima haki ya kujieleza.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...