Ma rais Jakaya Kikwete kushoto, Uhuru kenyatta kati, na Yoweri museveni kulia |
Akizungumza katika Mkutano wa viongozi wa Jumuiya hiyo mjini Arusha Tanzania makao makuu ya Jumuiya hiyo, rais Kenyatta amesisitiza kuwa makubaliano yaliofikiwa ya matumzi ya sarafu moja mwaka uliopita ni mwanzo wa mafanikio ya Jumuiya hiyo na wananchi wa mataifa hayo kutengamana kwa urahisi
Kuhusu mzozo wa Sudan Kusini, rais Kenyatta amesema kuwa Jumuiya hiyo itafanya kila kilicho ndani ya uwezo wake kusaidia kurejesha amani lakini akatoa wito kwa pande mbili zinazozazana kuacha vita na kukubaliana.
Mazungumzo ya kujadili ombi la Sudan Kusini kujiunga kama Mwanachama wa Jumuiya hiyo yameahirishwa hadi mwezi Septemba mwaka huu. Mbali na rais Kenyatta viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, rais Uganda Yoweri Museveni, Makamu wa rais wa Burundi Prosper Bazombanza na Waziri Mkuu wa Rwanda Pierre Damien Habumuremyi.