Pages

jeudi 27 mars 2014

SHEMEJI WA OSAMA BEN LADEN AKUTWA NA HATIA YA KUSHIRIKIANA NA WANAMGAMBO WA AL SHABAB


Mahakama ya mjini New York nchini Marekani imemkuta na hatia shemeji wa aliyekuwa kiongozi wa Kundi la Al-qaeda duniani Osama Bin Laden kwa makosa ya kushirikiana na mtandao wa kigaidi kudhuru maisha ya wamarekani.

Suleiman Abu Ghaith, amekutwa na hatia ya kushiriki njama za kuua raia wa Marekani na kuunga mkono ugaidi wakati akiwa kama msemaji wa kundi hilo kati ya mwaka 2001 na 2002.
Abu Ghaith sasa anakabiliwa na hukumu ya kifungo cha maisha kwenyeb gereza la Marekani katika kesi iliyodumu kwa majuma matatu, kesi ambayo ni ya kwanza ya juu kusikilizwa na mahakama ya kiraia.

JENERALI FATAH AL SISI ATANGAZA KUJIUZULUU WADHIFA WAKE WA MKUU WA MAJESHI KWA AJILI YA KUWANIA UCHAGUZI WA RAIS


Mkuu wa majeshi wa Misri, Jenerali Abdeli Fattah al-Sisi ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake ya ukuu wa majeshi ili kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi ujao huku akiahidi kupambana na ugaidi iwapo atateuliwa.

Sisi ambaye amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kuipindua serikali ya Mohamed Morsi anapewa nafasi kubwa ya kushinda kiti hicho kwakuwa hakuna upinzani mkubwa anaotarajiwa kuupata toka kwa wagombea wengine.

Licha ya kuungwa mkono na sehemu kubwa ya wananchi wa Misri, hatua yake ya kuamua kugombea urais kwenye uchaguzi wa mwezi June, kumeleta mgawanyiko miongoni mwa wananchi ambapo wapo wanaoona kuwa kiongozi hiyo hakupaswa kuwania kiti hicho na badala yake angebakia kwenye nafasi yake ya ukuu wa majeshi na waziri wa Ulinzi.

Tayari baadhi ya waangalizi wa uchaguzi wanakosoa hatua ya al-Sisi wakisema uchaguzi hautakuwa huru na haki kwakuwa Serikali yenyewe inayoandaa uchaguzi huo haikuchaguliwa na wananchi.

VIKOSI VYA SERIKALI YA SOMALIA VIKISAIDIWA NA MAJESHI YA AMISOM VYAUTEKA MJI MUHIMU WA WI BUR


Wanajeshi wa Serikali ya Somalia kwa kushirikiana na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika AMISOM, wamefanikiwa kuuchukua mji muhimu wa Wl-Bur toka kwenye mikono ya wanamgambo wa Al-Shabab.

Mji huo ulioko umbali wa kilometa 350 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu, ulikuwa ni ngome muhimu ya wapiganaji wa Al-Shabab waliokuwa wakiutumia kupanga mashambulizi yao dhid ya vikosi vya Serikali na vile vya AMISOM.

Kanali wa jeshi la Somalia, Mohamed Adan amethibitisha vikosi vyao kuingia kwenye mji huo na kuongeza kuwa wapiganaji hao walikimbia nasasa wanatekeleza mashambulizi ya kushtukiza toka kwenye maeneo ya misitu ambako nako wataanza operesheni maalumu ya kuwasambaratisha.

Licha kwa sehemu kubwa vikosi hivyo kufanikiwa kushikilia miji muhimu toka kwa wapiganaji wa Al-Shabab, bado wanamgambo hao wameendeleza mashamblizi makubwa mjini Mogadishu na kutishia hali ya usalama.


SERIKALI YA TANZANIA YAKUBALI KUWATUMA WANAJESHI WAKE WA KULINDA AMANI NCHINI SUDANI KUSINI


Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa hivi karibuni itatuma wanajeshi wake kwenda nchini Sudan Kusini kulinda amani kufuatia ombi la katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Hapo jana, waziri wa mambo ya kigeni wa Tanzania, Benard Membe, amesema nchi yake imekubali ombi la Katibu mkuu Ban Ki Moon aliyeomba nchi hiyo itume wanajeshi wake nchini Sudan Kusini kusaidia kulinda amani.

Waziri Membe amesema kuwa kutokana na mchango wa vikosi vya Tanzania nchini Jamhuri ya Kidekrasia ya kongo, Umoja wa Mataifa umeona uiombe tena nchi ya Tanzania kutuma wanajeshi wake Sudan Kusini.

Hata hivyo waziri Membe hakusema ni lini hasa wanajeshi hao wataondoka Tanzania kuelekea Sudan Kusini.

mercredi 26 mars 2014

MAAFISA WATATU WA ULINZI WA RAIS OBAMA WAREJESHWA JIJINI WASHINGTON BAADA YA KUKUTWA WAMELEWA KUPITA KIASI

Walinzi wa tatu wa karibu sana wa rais Barack Obama wa Marekani ziarani barani Ulaya, warejeshwa nyumbani baada ya kukutwa wamelewa kupita maelezo. Afisa hao wa ulinzi kutoka idara ya ujasusi walirudishwa jijini Washington Jumapili iliopita siku moja kabla ya kuwasili wa rais Obama jijini Amsterdam. Gazeti la Washington Post lililovumbua taarifa limesema mmoja kati ya maafisa hao alikutwa amelewa chepe huku hajitambuwi baranai karibu na Hoteli walikokuwa wamefikia.

Maafisa hao wote wa tatu ni kutoka kitengo maalum cha idara ya Ujasusi kinacho husikana ulinzi wa Rais wa Marekani iwapo itatokea shambulizi. Kazi yao wanahusika na kubaki kwenye eneo la tuko na kujibu mashambulizi, wakati kundi nyingine likihusika na kumlinda rais kwa kumuondowa haraka sana kwenye eneo la tukio. Kundi hilo la maafisa wanaojibu mashambulizi, ni la maafisa walioajiriwa kutokana na kuwa na uwezo wa na ujuzi wa hali ya juu.

Wanajeshi hao wanatuhumiwa kuvunja sheria inayo tumiwa kwa maafisa wote wa ulinzi wa rais Barack Obama: kutojihusisha na kilevi chochote kwa muda wa saa kumi kabla ya kuanza shughuli.

Maafisa hao walifanya sherehe kwa pamoja siku ya Jumamosi, wakiwa na dhamira ya kurejea katika hali ya kawaida kabla ya kutuwa kwa ndege ya Air Force One, Jumatatu March 24 asubuhu, hawakupima muda wa kilevi walichotumia na hivo kutokea kwa hali hiyo iliosababisha mmoja kati ya walinzi kuwasiliana na ubalozi wa Marekani.

Gazeti la Washington Post, limekumbusha kuwa, Sheria ihusuyo kanuni ya maafisa wa ujasusi ilibadilishwa mwaka 2012 baada ya kutokea kwa kashfa nchini Colombia ambapo maafisa 10 waliachishwa kazi baada ya kuwasiliana na kituo kimoja cha Makahaba. Hasira ya chini kwa chini ya rais Barack Obama ndio ilioplekea kujiuzulu kwa mkurugenzi wa Idara ya ujasusi wa Marekani

SERIKALI YA KENYA YAAMURU WAKIMBIZI WOTE WA SOMALIA KUREJEA KAMBINI WAKATI HUU IKIENDELEA KUWASAKA MAGAIDI

Wakimbizi wa kambi ya Daadab nchini Kenya

 Serikali ya Kenya imeagiza wakimbizi wote walioko nchini humo kurejea kwenye kambi zao za Daadab na Kakuma, agizo linalokuja likilenga kukabiliana na mashambulizi zaidi yanayoshuhudiwa nchini humo.

Waziri wa ulinzi wa Kenya, Joseph Ole Lenku amewataka wananchi kumripoti raia yeyote ambaye wanahisi ametoka kwenye kambi hizo na kwamba atakayebainika kukaidi agizo la Serikali atachukuliwa hatua za kisheria.

Wakimbizi wa kambi ya Kakuma nchini Kenya
Tangazo la Serikali ya Kenya linakuja kufuatia shambulio la siku ya Jumapili kwenye kanisa moja mjini Mombasa ambao watu wanne walipoteza maisha kwenye mfululizo wa msahmbulizi ambayo yanadaiwa kufanywa na wapiganaji wa Somalia ambao baadhi yao wanadaiwa kutoka kwenye makambi ya wakimbizi toka kwenye taifa hilo.

Nchi hiyo inakumbwa na mfululizo wa mashambulizi toka ilipotuma wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na wapiganaji wa Al-Shabab.


HALI YA KIBINADAMU NCHINI SUDANI KUSINI NI YA KUTISHA WAKATI MSIMU WA MVUA UKIKARIBIA


Mamilioni ya watu walionaswa kwenye mapigano nchini Sudan Kusini wanakabiliwa na hali mbaya ya chakula wakati huu msimu wa mvua ukikaribia, hii ni kwa mujibu wa ripoti moja ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kibinadamu nchini humo.

Mkuu wa tume ya kuratibu misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, John Ging amesema nchi hiyo inakabiliwa na baa la njaa kutokana na uhaba wa chakula hali inayowafanya wananchi wengi zaidi kuwa kwenye hatari ya kupoteza maisha.

John Ging amesema licha ya kuwa hawajatangaza hali ya njaa nchini Sudan Kusini lakini ukweli wa mambo unaonesha dhahiri taifa hilo kuelekea huko na pengine kushuhudia hali hiyo ikitangazwa.
Kiongozi huyo ametaka kusitishwa kwa mapigano ili kutoa nafasi ya wananchi kupokea misaada ya kibinadamu.

RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZIZA KUWANIA MUHULA WA TATU KATIKA UCHAGUZI MKUU WA RAIS


Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi Edourd Nduwimana amefahamisha kwamba wale wote wanaopinga rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu kwa kufurahishwa kuona muswada wa marekebisho ya katiba umekwamishwa bungeni, hili halitamkwamisha Nkurunziza kuwania uchaguzi wa rais wa mwaka 2015 ujao. Hii ni mara ya kwanza waziri wa Mambo ya ndani kutangaza rasmi kuwa rais Nkurunziza atawania uchaguzi mkuu, na hivo kuzua mtafaruku kuhusu swala hili linalo wakera wengi.

Rais Nkurunziza alikuwa amejizuia kwa kipindi chote hichi kutamka rasmi kwamba atakuwa miongoni mwa wagomnbea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

hatuwa ya hivi majuzi ya bunge la taifa hilo kutupilia mbali muswada wa mapendekezo ya katiba ya nchi hiyo ili kumpa nafasi ya kuwania tena muhula mwingine wa tatu, ndiyo ambayo imebadili kalenda, na hivo waziri wa mambo ya ndani ambaye ni mtu wa karibu na utawala kupewa nafasi ya kuweka wazi kwa mara ya kwanza kuhusu hatuwa hii ya rais kuwania uchaguzi wa mwaka 2015.

Waziri nduwimana amesema “kile tunachopinga ni kuona kwamba kuna watu wanaoona kuwa swala la rais Nkurunziza kuwania uchaguzi mkuu kwa muhula wa tatu limekwisha, la hasha sio kweli. Kile ninacho washauri wanasiasa wataowania uchaguzi ni kujiandaa huku wakitambuwa kwamba watapambana na rais wa sasa. Mahakama ya kikatiba ndiyo itayo amuwa kwa njia moja ama nyingine na wananchi watatakiwa kuheshimu maamuzi.”

Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi ameanzisha mjadala huu kuhusu muhula wa tatu wa rais Nkurunziza ikiwa ni takriban wiki moja baada muswada wa mabadiliko ya katiba kukwama bungeni. Waziri wa mambo ya ndani yeye anasema rais Nkurunziza anawania muhula wa pili kwakuwa katika uchaguzi wa mwaka 2005 alichaghuliwa na bunge, na hivo muhula ulipo sasa ndio muhula wa kwanza. Mahakama ya kikatiba ndiyo itayo amuwa kuhusu hatuwa hii.

Hii inakuja baada ya kushindwa kwa hatuwa ya kwanza, utawala wa Burundi umeanzisha mvutano dhidi ya upinzani unaopinga katu katu kusikia kuwa Nkurunziza anajichaghulisha tena katika muhula wa tatu, na ambao wanasema hawana imani na mahakama ya kikatiba ambayo tayari imesha onyesha upendeleo na unaundwa na watu kutoka chama tawala.



Pour le parti de l’opposition, l’Union pour le progrès national (Uprona), ce recours à la Cour constitutionnelle est une nouvelle tentative de « passage en force » de la part du président. Selon l’article 96 de la Constitution de mars 2005, basée sur les accords d’Arusha ayant permis de mettre fin à la guerre civile burundaise (1993-2006), le président « est élu au suffrage universel direct pour un mandat de cinq ans renouvelable une fois ».
Joint par RFI, Charles Nditijé, le président de l'Uprona estime qu'il faudra s'opposer à cette « violation de la Constitution » : « C’est vraiment la voie de la confrontation qu’il ont décidé d’emprunter depuis le processus d’amendement de la Constitution. Les représentants du peuple viennent de refuser ces amendements qui offrent sur un plateau d’argent un troisième mandat au président de la République. Aujourd’hui, la Constitution est claire ; l’accord d’Arusha est clair. Nous devons nous préparer à refuser ce diktat, ce passage en force et cette imposition ».
Chama cha Upinzani cha Uprona kinasema kukimbilia katika mahakama ya kikatiba ni hatuwa nyingine ya pili ya matumizi ya nguvu yanayo tumiwa na rais. Kwa mujibu wa kifungu nambari 96 cha katiba ya March mwaka 2005 iliofikiwa chini ya makubaliano ya amani ya jijini Arusha yaliopelekea kusitishwa vita vya wenywe kwa wenyewe vya mwaka 1993-2006, rais wa jamhuri anachaguliwa kupitia kura za wananchi kwa kipindi cha miaka mitano ambayo inaweza kuongezwa mara moja.

Akizungumza na RFI, Charles Nditije mwenyekiti wa chama Uprona amesema inafaa kupinga kwa nguvu zote uvunjifu huu wa katiba ambao unaendelea kutekelezwa na chama tawala, wakati ambapo katiba ipo wazi, mkataba wa amani wa Arusha upo wazi, kwa hiyo amesema hatuwa hii ni ya kutupilia mbali.

mardi 25 mars 2014

URUSI YAFUTWA KWENYE KUNDI TAJIRI DUNIANI LA G8, NA MKUTANO WA JIJINI SOTCHI WA KUNDI HILO WAAHIRISHWA


Viongozi wa mataifa ya magharibi wameonyesha kwa mara nyingine tena uungwaji wao mkono kwa serikali mpya ya Ukraine na kupinga hatuwa ya Urusi kurejesha eneo la Crimea kwenye himaya yake, ikiwa ni katika siku ya pili na ya mwisho ya mkutano wa unaofanyika jijini Hague kuhusu Usalama.
Hapo jana rais Barack Obama wa Marekani na washirika wake walifuta mkutano wa G8 ambao ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi Juni jijini Sotchi nchini Urusi kama kupinga hatuwa iliochukuliwa na Urusi dhidi ya Crimea ambapo tayari serikali ya Kiev imewaondowa wanajeshi wake katika eneo hilo.
nchi saba zenye utajiri mkubwa duniani G7 zimeitahadharisha Urusi kuhusu hatuwa yoyote ambayo inaweza kuvuruga Usalama wa Ukraine.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema wametuma ujumbe mzito wa serikali ya Urusi, na kwamba vikwazo zaidi vitaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha Urusi inabadili msimamo wake.

VIONGOZI WA NCHI ZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI ICGLR WAKUTANA JIJINI LUANDA NCHINI ANGOLA

Kutoka kushoto ni rais Joseh Kabila,  rais Paul Kagame na mwenyeji wao Dos Santos
Viongozi kadhaa wa ukanda wa Afrika mashariki na kati wanakutana jijini Luanda katika kikao kilichoitishwa na rais wa Angola Edouardo Dos Santos mwenyekiti wa ICGLR.

Mkutano wa siku mbili utawakutanisha ma rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Deniss Sassou Nguesso rais wa Congo Brazaville, rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania na Rais Joseph Kabila wa DRCongo na rais Paul Kagame wa Rwanda.

Mkutano huo ulizinduliwa jana ambapo viongozi hao walipata chakula cha jioni pamoja chini ya mwenyekiti Dos Santos, wakiwepo ma rais Paul Kagame, Dennis Sassou Nguesso na rais Joseph Kabila.

Viongozi hao wanataraji kuzinduwa rasmi mkutano huo huku waku jadili kuhusu maswala ya ushirikiano na usalama wa nchi za kikanda.

VIONGOZI WA KIDINI NCHINI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI WAUOMBA UMOJA WA MATAIFA KUTUMA MAJESHI YA KULINDA AMANI NCHINI HUMO


Viongozi wa kidini nchini jamhuri ya afrika ya kati wameuomba Umoja wa Mataifa kutuma haraka iwezekanavyo vikosi vya Umoja huo vya kulinda amani katika nchi hiyo inayoendelea kukumbwa na mzozo wa kivita wenye sura ya kidini.

Kiongozi wa kanisa katoliki jijini Bangui Dieudonnee Nzapalanga amesema Jumuiya ya Kimataifa lazima ifanya jitihada za ziada ili kukomesha machafuko yanayoendelea kuripotiwa jijini Bangu na vitongoji vyake.
Hivi karibuni kiongozi huyo wa kanisa katoliki pamoja na Imam wa msikiti wa Bangui Imam Oumar Kobine Layama na yule wa kanisa la kiprotestanti, wamezuru mataifa mbalimbali hususan jijini New York Marekani na Italia ambako walikutana na jamii ya kikatoliki ya San'Egidio ambayo inaunga mkono juhudi zao.
Hayo yanajiri wakati mauji yakiendelea kuripotiwa huku na kule jijini Bangui ambapo hivi majuzi watu zaidi ya sita walipoteza maisha katika mapigano hayo yenye sura ya kidini.

RAIS WA KENYA UHURU MUIGAI KENYATTA ATOWA ONYO KALI KWA MAGAIDI WANAOTUMIA DINI KATIKA KUTEKELEZA MAUAJI

Rais Kenyatta Uhuru Kenyattta na Naibu waibu wake William Rutto wakiw anjiani kuelekea Arusha March 24, 2014
Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta hapo jana wakati Akiwa njiani kuelekea jijini Arusha ambako atahutubia kwa mara ya kwanza katika kikao cha Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashari, amewaonya wanamgamboa wa makundi ya Kigaidi wanaoendelea kutekeleza mashambulizi na kwamba hakutakuwa na msamaha wa aina yoyote ile kwa magaidi.

Onyo hili linatolewa wakati huu kukiwa na mfululizo wa matukio ya kigaidi katika Mkoa wa Pwani wa Mombasa nchini Kenya ambako hivi karibuni bomu na silaha zilikamatwa huku hivi majuzi watu wenye soilaha walimina risase kanisani na kuwauwa watu zaidi ya wanne.

Uhuru Kenyatta amesema serikali yake inatambuwa na kuheshimu kila dini, lakini kwa wale wachache wanaotaka kuchefua hali ya hewa hawawezi kuvumiliwa.

WAZIRI MKUU WA MALAYSIA NAJIB RAZAK ATANGAZA RASMI KUWA NDEGE ILIOPOTEA ILIANGUKA KUSINI MWA BARA LA AUSTRALIA

Waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak ametangaza rasmi kuwa ndege ya taifa hilo aina ya MH370 iliyopotea hivi karibuni, ilianguka kwenye bahari ya hindi kusini mwa bara la Australia ikiwa na abiria 239.

Akiwa mwenye huzuni, waziri mkuu Razak amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa moya walizozipata kupitia njia ya Sattelite wamepata uhakika kuwa ndege hiyo iliishiwa mafuta ikiwa kwenye eneo la bahari ya hindi na kuanguka.


Waziri mku Razaki amewataka wanafamilia waliopoteza ndugu zao kuwa na subira wakati huu wakisubiri uhakika zaidi toka kwa vikosi vya wanamaji wa Australia ambao walifanikiwa kubaini eneo ambalo ndege hiyo inadaiwa kuanguka.
Magazeti ya nchi hiyo hii leo kwenye kurasa zao yamechapicha majina ya abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo huku yakisubiri kupata taarifa rasmi za uthibitisho toka kwa mamla zinazoendelea na uchunguzi kwenye bahari ya hindi.

WAASI WA SYRIA WAZIDISHA MASHAMBULIZI DHIDI YA MAJESHI YA SERIKALI

Waasi wa jeshi huru nchini Syria wameanzisha mapigano makali dhidi ya wanajeshi wa Serikali ya rais Bashar al-Asad kwenye miji minne mikubwa ambayo awali waliipoteza kwenye mikono ya serikali.
Operesheni hii ya waasi wa Syria inaelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa ni hatua ya ulipizaji kisasi dhidi ya operesheni za Serikali ambazo zilifanikisha kuwapokonya miji hiyo na sasa wanajaribu kuirejesha kwenye himaya yao.

Katika hatua nyingine katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki Moon amesema hali ya misaada ya kibinadamu nchini Syria hasa kwenye miji yenye mapigano bado imeendelea kuwa changamoto kwakuwa bado wafanyakazi wa mashirika ya misaada wanashindwa kufika kwenye maeneo hayo.

WAFUASI 529 WA RAIS ALIYEPINDULIWA MADARAKANI NCHINI MISRI MOHAMED MORSI WAHUKUMIWA KUNYONGWA

Mahakama moja mjini Cairo imewahukumu kunyongwa wafuasi 529 wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohamed Morsi ambaye aliondolewa na jeshi, ikiwa ni hukumu inayotolewa baada ya kusikilizwa kwa vikao viwili pekee.

Hukumu hii ya kifo ni kubwa zaidi kutolewa kwa watu wengi kwa wakati mmoja kwenye historia ya dunia, hatua ambayo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa mahakama haikufuata mchakato sahihi wa kufikia kutoa hukumu hiyo.

Huenda uamuzi huo ukabatilishwa na mahakama ya rufaa kwakuwa mawakili wa watuhumiwa hao tayari wamewasilisha pingamizi lao dhidi ya hukumu ya kifo kwa wateja wao wakisisitiza kesi hiy kuchukua muda mfupi zaidi kuliko kawaida.

UMOJA WA MATAIFA WAONYA JUU YA KUENDELEA KUSHUHUDIWA KWA MASHAMBULIZI YA WANAMGAMBO WA AL SHABAB

Umoja wa mataifa UN umeonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa ongezeko la mashambulizi ya kushtukiza yanayotekelezwa na wapiganaji wa kundi la Al-Shabab nchini Somalia wakati huu ambapo operesheni kubwa inafanywa kukabiliana na wapiganaji hao.

Balozi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Somalia, Nicholas Kay amesema kuwa licha ya operesheni kubwa inayoendelea kufanywa na vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM kuwadhibiti wapiganaji hao, bado wanamgambo wa Al-Shabab wameendelea kuwa na nguvu na kuzidisha mashambulizi yao mjini Mogadishu.

Kay amesema kuwa wanamgambo hao wameshajua kuwa wamezidiwa kwenye vita hivyo na ndio maana na wao wameendelea kuzidisha mashambulizi zaidi dhidi ya vikosi vya Serikali na wanajeshi wa AMISOM.

Kauli ya Kay anaitoa wakati huu ambapo vikosi vya AMISOM vimeendelea kufanikiwa kuchukua miji zaidi iliyokuwa inakaliwa na wapiganaji hao.

lundi 24 mars 2014

WATU WANNE WAPOTEZA MAISHA NCHINI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI


Takribani watu wanne wameuawa katika mapigano ya Jumamosi mjini Bangui wakati ambapo vikosi vya jeshi la Kifaransa vilipoingilia makabiliano kati ya makundi ya wapiganaji.

Afisa wa jeshi la Umoja wa Afrika ambaye hakupenda jina lake litajwe a amesema kuwa Watu wanne, ikiwa ni pamoja na waislamu 2 waliuawa huku wengine saba wakijeruhiwa katika mapigano kati ya vikundi vyenye silaha, ikiwa ni pamoja na kundi la anti Balaka.

Afisa huyo aliongeza kuwa Mapigano yalizuka katika maeneo kadhaa kwa wakati mmoja na kusababisha jeshi la kimataifa kuingilia ili kukomesha mauaji lakini nayo yakawa sehemu ya mapigano.

Chanzo kimoja kutoka Jeshi la kifaransa kimearifu kuwa mapigano kati ya vikundi vyenye silaha dhidi ya jeshi hilo yameripotiwa ambapo wanajeshi hao wamejipanga kukabiliana nao kwa vile walishambuliwa na kujibu mashambulizi.

WATU WANNE WAPOTEZA MAISHA WENGINE 18 WAJERUHIWA BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA RISASE KANISANI MJINI MOMBASA


Watu wanne wamepoteza maisha na wengine zaidi ya kumi wamejeruhiwa katika shambulio lilitokea jana ndani ya kanisa moja jijini Mombasa baada ya watu wenye silaha kuingia kanisani na kuanza kuwavurumishia risase waumini.

Shambulio hilo linakuja wakati huu polisi katika eneo hilo ikijinasibu kuimarisha Usalama na kuwa tayari kujihami dhidi ya mashambulizi ya wanamgambo wa Al Shabab.

Kiongozi wa polisi katika Wilaya ya Likoni kusini mwa jiji la Mombasa Robert Mureithi amesema watu wawili walipoteza maisha papo hapo huku wengine wawili wakiuawa baada ya kufikishwa Hospitalini.

YOYA, T. MAX NA SLAY NDANI YA WIMBO MMOJA KATIKA ALBUM YA U’ILL LOVE CHANGES

_MG_4032 (2)
Katika muendelezo wa kuandaa na kukamilisha album ya mradi ya Album ya U’ill love changes, wasanii Yoya, T.Max na Slay wapo studio kwa ajili ya kurikodi wimbo ambo utakuwa miongoni mwa nyimbi zitazo beba album hiyo.
Akiulizwa kuhusu wimbo huo, Yoya amesema, ukiangalia Machine hizo tatu kuweka sauti zao pamoja, lazima kitoke kitu kizima, hivyo wapenzi wa Muziki watarajie kitu kizuri kutoka kwao.
_MG_4025
Upande wake Slay amesema amefurahishwa kwanza na mradi huo wa U’ill love changes, lakini pia kushiriki katika album hiyo ambayo itakuwa ni vol 1, hivyo ni fursa kubwa na nzuri sana kwake kuwemo katika hatuwa hii ya kwanza kabisa ya mradi huo.
_MG_4040 (1)
Aidha kuhusu swala la ushirikiano na wasanii wengine, Slay amesema, kwa muda mrefu, ubinafsi unaiponda sana tasnia ya muziki nchini Burundi kwa muda mrefu, hakika ushirikiano unahitajika katika kuikomboa sanaa ya Burundi ambayo imeshindwa kuvuka mipaka ya kikanda na hata ya kimataifa.

vendredi 21 mars 2014

UPINZANI NCHINI DRCONGO UNAPINGA MCHAKATO WA VIONGOZI WA CHAMA TAWALA CHA PPRD KUTAKA RAIS JOSEPH KABILA KUWANIA TENA UCHAGUZI BAADA YA MWAKA 2016


Upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo DRC unapinga mchakato unaodaiwa kuanza ndani ya chama tawala nchini humo cha PPRD ambapo viongozi wake wanalenga kukusanya saini zaidi ya laki 1 ili kumpa nafasi rais Joseph Kabila kuendelea kusalia madarakani hata baada ya mwaka 2016.

Hapo jana katibu mkuu wa chama cha PPRD, Claude Mashala amewaambia wanahabari kuwa wameanzisha harakati za kukusanya saini hizo ili kubadili katiba ya nchi hatua ambayo imepingwa vikali na upinzani ambao unasisitiza rais Kabila kutowania tena urais.

Hata hivyo spika wa bunge la DRC Aubin Minaku amenukuliwa hii leo akisisitiza kuwa rais Josephu Kabila hana mpango wa kuongeza muda wa yeye kusalia madarakani baada ya muda wake kukamilika.

Wachambuzi wa masuala ya siasa akiwa mjini Goma mashariki mwa DRC na hapa anasema mara nyingi rais anaweza asiwe yeye ameamua bali ni ushawishi wa baadhi ya watu jambo ambalo ni hatari.

MAKAM WA RAIS WA ZAMANI NCHINI BURUNDI FREDERIC BAMVUGINYUNVIRA AACHIWA HURU KWA DHAMANA KUTOKANA NA SABABU ZA KIAFYA



Frederic Bamvuginyumvira

Mahakama kuu inayo pambana na rushwa nchini Burundi, imemuachia huru kwa dhamana aliyekuwa makam wa rais wa zamani nchini humo Frederic Bamvuginyuvira kutokana na sababu za kiafya. Bamvuginyumvira alikamatwa Desemba 5 mwaka 2013 kutokana na kuhusishwa katika tukio la kutembea nje ya ndoa yake na baadae kujaribu kutowa rushwa.

Wakili wa Frederic Bamvuginyunvira Fabien Segatwa amesema mahakama inahusika na kupambana na rushwa imemuachia huru kwa dhamana mteja wake baada ya kutowa dhamana inayo lingana na franka za Burundi milioni moja, sawa na Euro 450.

Wakili Fabien Segatwa

Duru kutoka katika mahakama hiyo zimearifu kwamba Banvuginyumvira ameachiwa huru kwa dhamana kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu (Presha)

Wakili Segatwa amesema wameridhishwa na hatuwa hiyo kwani mteja wake hana sababu zozore za kusalia korokoroni kwakuw ahana hatia yoyote, anazuiliwa kutokana na sababu za kisiasa, hii itamsaidia kujitibisha na kujitetea kikamilifu. 

Frederic Bamvuginyumvira mwenye umri wa miaka 52 alikamatwa katika nyumba moja ya wageni akiwa na mwanamke mwenye umri wake, na baadae kutuhumiwa kosa la rushwa, kwa kumshawishi afisa polisi aliyemkamata ili amuachiye huru.

Katika tukio hilo, upinzani nchini Burundi inaituhumu serikali kubuni mbinu za kumuangusha kisiasa mwanasiasa huyo ambaye anaonekana huenda akawa tishio katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Kwa sasa Frederic Bamvuginyuvira ambaye ni naibu mwenyekiti wa chama cha FRODEBU anazaniwa kuwa ndiye mgombea mmoja wa upinzani katika uchaguzi wa mwaka 2015. Anchukuliwa kama mtu mwenye upinzani mkubwa sana kwa rais Pierre Nkurunziza ambaye anaonyesha nia ya kuwania muhula mwengine wa tatu.



jeudi 20 mars 2014

CHAMA CHA UPINZANI CHA MSD NCHINI BURUNDI CHAOMBA UUNDWAJI WA TUME HURU KUCHUNGUZA MACHAFUKO YA MARCH 8

Alexis Sinduhije, mwenyekiti wa chama cha MSD

Chama cha upinzani cha MSD kilicho fungiwa kwa muda wa miezi 4 nchini Burundi kimemuandikia baruwa katibu mkuu wa serikali ya Burundi kumtaka aunde tume maalum ya kimataifa ilio huru juu ya kuchunguza vurugu zilizotokea March 8 mwaka huu kwenye makao makuu ya chama hicho.
Chama hicho kimesema kipo tayari kushirkiana na tume hiyo ili kuweka wazi kuhusu ukweli juu ya yaliotokea siku hiyo na kitakubaliana na matokeo ya tume hiyo.
March 8 mwaka huu kulitokea vurugu kwenye makao makuu ya chama hicho cha MSD kinachoongozwa na Alexis Sinduhije ambapo watu kadhaa walipoteza maisha wengine kujeruhiwa huku wengine kutiwa mbaroni.
Kufuatia vurugu hizo chama hicho kinasema, ukweli lazima utambulike, ili wahusika wa vurugu hizo wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.


HALI YA WASIWASI YAENDELEA KUTANDA KATIKA MJI WA BWEGERA BAADA YA KUUAWA KWA MAMA MMOJA MJINI HAPO


Jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limedhamiria kuimarisha usalama katika mji wa Bwegera mtaani Uvira katika jimbo la kivu kusini baada ya kufanyika shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na watu waliojihami kwa silaha, usiku wa kuamkia siku ya jumatano.

Maafisa wakijeshi mjini humo wanasema mwanamke mmoja aliuawa mara baada ya kupatwa na risasi tumboni mwake huku Mji huo wa Bwegera ukiwa umegubikwa na Hali ya wasi wasi.

Kamanda wa Kikosi cha jeshi la serikali ya DRC, FARDC Kanali Elias Rubibi amelishutumu Kundi la wapiganaji wa kijadi wanaotumia majambia, visu na mapanga lakini pia ushirikina kwamba ndio wamekuwa wakizorotesha usalama katika eneo hilo.

RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA ATAJWA KATIKA RIPOTI YA UBADHIRIFU WA MALI ZA WALIPA KODI

Tume maalumu iliyokuwa imeundwa kuchunguza kashfa ya rushwa na matumizi mabaya ya fedha za walipa Kodi nchini Afrika Kusini, hatimaye hii leo imetoa ripoti yake ya kumtaja dhahiri rais Jackob Zuma na mawaziri wake kuhusika na ubadhilifi wa kiasi cha dola za Marekani milioni 23 za walipakodi.

Kiongozi wa tume hiyo, Thuli Madonsela amesema kuwa tume yake imebaini kuwepo mapungufu makubwa ya kisheria kwenye kuidhinisha matumizi ya fedha zilizotumika kufanya ukarabati kwenye makazi ya rais Zuma na kutaka awajibishwe kutokana na kushindwa kusimamia vema fedha za umma.


Thuli Madonsela
Ripoti hii inatolewa wakati huu ambapo rais Zuma anaendelea na kampeni zake za kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi may mwaka huu, hatua inayoelezwa kuwa ni pigo kwa utawala wake.

BALOZI WA UMOJA WA MATAIFA ANAYEHUSIKA NA MASWALA YA KUPIGA VITA UKIMWI ASEMA HATUWA YA SERIKALI YA UGANDA KUPIGA VITA NDO ZA JINSI MOJA ITASABABISHA U=ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Hatua ya Serikali ya Uganda kutia saini sheria mpya inayokataza mapenzi ya watu wa jinsia moja nchini humo, imeelezwa na umoja wa Matiafa kuwa huenda ikachangia kurejesha nyuma juhudi za taifa hilo kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.

Balozi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kupambana na maambukizi ya UKIMWI barani Afrika, Speciosa Wandira-Kazimbwe ambaye pia aliwahi kuwa makamu wa rais wa Uganda, amesema sheria hiyo inaongeza uwepo wa vitendo vya ubaguzi dhidi ya jamii ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Kazimbwe amesema hatua hiyo inarudisha nyuma juhudi za Uganda kupambana na maambukizi mapya, ambapo mwaka 2012 kulikuwa na wagonjwa milioni 1.5 pekee lakini kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wapya laki 1 na elfu 40.


MSHAMBULIAJI WA KUJITOWA MUHANGA WA TUKIO LA JANA NCHINI SOMALIA ALIKUWA NI MZEE MWENYE UMRI WA MIAKA 60 RAIA WA SOMALIA


Mshambuliaji wa kujitowa muhanga aliyejilipuwa jana jumnne katika mji wa Buula Burde ulionyakuliwa hivi karibuni kuotka mikononi mwa wanangmabo wa Alshabab alikuwa ni raia wa Norway mwenye asili ya somalia ambaye alikuwa na umri wa miaka 60.
Msemaji wa Al Shabab Abdulaziz Abu Musab ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kwamba mshambuliaji huyo mwenye umro wa miaka 60 anatambulika kwa jina la Abdullahi Ahmed Abdulle ambaye alijiunga na Al Shabab kutoka Norway kwa ajili ya kupambana na maaduwi wa Allah.
Msemaji huyo wa Al Shabab amesema mzee huyo amejitolea kwa ajili ya Allah, ikiwa ni ishara kwamba jihad haina umri.
Hapo jana, mshambuliaji wa kujitowa muhanga ambaye alikuwa katika gari, alijilipua kwenye Hoteli ambapo askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika Amisom kuotka nchini Djibouti walikuwa wamepiga kambi katika mji wa Buula Burde kwenye umbali wa kilometa 200 na jiji la Mogadishu na kusababisha mauaji ya askari kadhaa katika tukio hilo.
Mji wa Buula Burde ilikombolewa kutoka mikononi mwa Al shabab March 13 mwaka huu baada ya majeshi ya Amisom kufanya mashambulizi makubwa na kuwafurusha wanamgambo wa Al Shabab katika mji huo.
Kundi la wanamgambo wa alshabab limekuwa likipata pigo kubwa ya kiupoteza miji muhimu iliokuwa ikikalia tangu mwezi Agosti mwaka 2001 wakati ilipoanzishwa operesheni ya Amisom dhidi ya wanamgambo hao ambapo hatuwa ya kwanza ilikuwa ni kufurushwa katika mji wa Mogadishu.
Licha ya kupoteza miji kadhaa, kundi hilo la Alshab bado linashikilia maeneo kadhaa ya vijijini na sasa wanapambana kwa kutumia mbinu za kuendesha mashambulizi ya kujitowa muhanga katika jiji la Mogadishu.

mardi 18 mars 2014

NAVI PILLAY MKUU WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU KWENYE UMOJA WA MATAIFA AZURU NCHINI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Navi Pillay mkuu wa tume ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa UN

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay ameanza rasmi ziara ya siku tatu nchini Jamhuri ya Afrika ya kati ambapo atakuwa na mazungumzo na rais Catherine Samba Panza kuhusu machafuko yanayoendelea nchini humo.

Ziara hii ni muhimu kwa Navi Pillay ambaye analenga kuwashawishi viongozi wa taifa hilo kutafuta suluhu ya kitaifa itakayopelekea kumaliza mauaji ya ulipizaji kisasi pamoja na kuwachukulia hatua watu ambao watakuwa wamehusika na mauaji ya kiholela nchini humo.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati Bi Catherine Samba Panza

Ziara hii inakuja wakati huu tayari wataalamu wa masuala ya haki za binadamu wameanza uchunguzi wao kuhusu mauji ya kidini yanayoendelea kushuhudiwa kwenye taifa hilo kati ya waislamu na wakristo.

Wakati haya yanajiri, wanajeshi wa kulinda amani nchini humo Jumatatu hii wamesema wamefanikiwa kukamata shehena kubwa ya ghala la silaha jirani kabisa na uwanja wa ndege wa mjini Bangui na kwamba wameanza uchunguzi kubaini zilikuwa zinatumiwaje.

RAIS WA URUSI VLADIMIR POUTINE AENDELEA KUPUUZIA VIKWAZO VYA MATAIFA YA MAGHARIBI NA KUSAINI SHERIA YA CRIMEA KUWA SEHEMU YA URUSI


 Rais wa Urusi, Vladmir Putin ameendelea kutia ngumu dhidi ya vitisho na vikwazo ilivyowekewa nchi yake na mataifa ya magharibi kufuatia hatua yake ya kulitambua eneo la Crimea kama sehemu yake, akisema vitisho hivyo vinachukuliwa kama vita kwa nchi yake.

Akiwahutubia wabunge wakati wa sherehe za utiaji saini makubalino rasmi ya kulitambua eneo hilo kama sehemu ya Ukraine, rais Putin amesema nchi yake hitatishwa na vikwazo vya mataifa ya magharibi na kusisitiza kuwa Crimea ni sehemu na itaendelea kuwa eneo la Urusi na kamwe hawatotenganishwa na yeyote.

Kauli ya Putini pamona na kutia saini mkataba na viongozi wa Crimea waliokuwepo wakati wa hotuba hiyo, inaonekana kama ubabe wa nchi yake kutaka kuyaonyesha mataifa ya magharibi kuwa inalenga kulikamata eneo hilo na haina nia ya kusalimisha nia yake kwa viongozi hao.

Hatua hii ya Urusi inaelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa itaendelea kuamsha hasiara zaidi ya viongozi wa mataifa ya magharibi na huenda kukawa na athari kubwa kwa Urusi na dunia.

Picha kwa Hisani ya Chinanews.com

SERIKALI YA UGANDA YATAHADHARISHA JUU YA MBINU MPYA ZA WANAMGAMBO WA AL SHABAB KUTEKELEZA MASHAMBULIZI


Askari wa jeshi la Uganda katika kikosi cha Amisom

Serikali ya Uganda imeonya kuhusu mbinu mpya zinazopangwa na wapiganaji wa kundi la Al-Shabab nchini Somalia na kwamba wanamgambo hao wanapanga kutumia magari ya mafuta kutekeleza uhalifu wao, siku moja baada ya serikali ya Kenya kubaini bomu kwenye gari moja.

Uganda inasema imepokea taarofa kuhusu kuwepo mpango wa wapiganaji hao kutekeleza shambulio mjini Kampala na kwenye nchi zenye wanajeshi wake nchini Somalia na kwamba wanaongeza usalama.

Tangazo la Uganda inakuja wakati huu ambapo wapiganaji wa Al-shabab wameendelea kutekeleza mashambulizi yao dhidi ya wanajeshi wa kulinda amani na vikosi vya Serikali ya Somalia.

Wakati huo huo taarifa kutoka nchini Somalia zimearifu kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha katika shambulio la kujitowa muhanga lililotokea katika hoteli moja mjini Buula Burde nchini Somalia, mji ambao ulirejeshwa mikononi mwa serikali ya Somalia Ijumaa Juma lililopita baada ya majeshi ya Umoja wa Afrika Amisom kuwafurusha wanamgambo wa Al Shabab.

Duru za serikali nchini Somalia zimearifu kuwa askari wanne wa Djibouti waliomo katika kikosi cha Amisom, wamepoteza maisha katika shambulio hilo.

Mashahidi wanasema watu nane wamepoteza maisha baada ya gari lililokuwa limebeba mabomu kulipuka jana usiku katika hoteli ambayo walikuwa wamepiga kambi viongozi wa kijeshi wa Amisom kabla ya kufuatiwa na mashambulizi ya risase.

MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA NCHINI TANZANIA JAJI SINDE WARIOBA AWASILISHA RASIMU YA KATIBA



 Suala la Muundo wa Serikali, Madaraka ya rais na Ardhi ni moja kati ya mambo ambayo yanatarajiwa kuwa mjadala mzito wakati wa kikao cha bunge maalumu la katiba mjini Dododma wakati watakapoanza kujadili rasimu ya pili ya katiba baada ya hii leo kuwasilishwa bungeni.

Kufuatia hapo jana jioni kikao hichi kudumu kwa dakika tatu pekee baada ya kutokea mvutano wa kuhusu kanuni za bunge maalumu, hatimaye wabunge hao walikubaliana na hii leo walihudhuria kikao ambacho walipokea taarifa ya rasimu ya pili ya katiba iliyowasilishwa na mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Sinde Warioba.

Wakati wa uwasilishaji wake, Jaji Warioba mara kadhaa alilazimika kutumia muda mwingi zaidi kufafanua masuala nyeti yenye utata ambapo kubwa ni kuhusu muundo wa muungano na Serikali tatu ambapo zaidi ya asilimia 60 ya wananchi walipendekeza serikali tatu na wachache walitaka serikali moja.

Suala jingine ambalo jaji Warioba amesema lilikuwa na mjadala ni lile linalohusu madaraka ya rais ambapo wananchi walitaka rais apunguziwe madaraka, na hapa anaeleza mapendekezo ya tume yake.

Haki ya kumiliki ardhi ni jambo jingine ambalo hata wabunge wenyewe wanatarajiwa kuwa na mvutano, na hapa jaji Warioba anaeleza ni kwanini suala la ardhi liingizwe kwenye katiba?

Bunge maalumu la katiba limeahirishwa hadi siku ya Ijumaa ambapo rais wa jamhuri ya Muungani wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alifungua rasmi kwa hotuba na sasa wajumbe haop watatumia siku mbili za jumatano na alhamisi kufanya semina elekezi kuhusu masuala ya katiba kabla ya kuanza kuijadili rasimu ya pili.

lundi 17 mars 2014

VIONGOZI WA UGANDA WAWEKEWA VIKWAZO BAADA YA KUPITISHA SHERIA INAYOPIGA MARUFUKU NDOA ZA WATU WA JINSIA MOJA


Serikali ya Uganda imeendelea kuwa kwenye shinikizo toka kwa mataifa ya magharibi kufuatia hatua ya bunge na kisha rais Yoweri Museveni kutia saini muswada wa sheria unaokataza ndoa za watu wa jinsia moja nchini humo.

Safari hii, bunge la Umoja wa Ulaya EU, limekubaliana kwa kauli moja kuwawekea vikwazo vya kusafiri baadhi ya viongozi wa Serikali ya Uganda ambao walihusika moja kwa moja na kupitisha sheria hiyo ambayo wameikosoa.

Bunge hilo sasa linapitia mapendekezo ya vikwazo ambavyo vinapaswa kuwekewa rais wa Uganda Yoweri Museveni, spika wa bunge la Uganda, Rebecca Kadaga na rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ambao wametejwa kwenye muswada huo kuwa wamehusika moja kwa moja na kupitisha sheria hiyo kandamizi.

MASHIRIKA YA KIRAIA NCHINI BURUNDI YAMUANDIKIA RAIS WA TAIFA HILO BARUA YA WAZI KUZINGATIA USALAMA WA TAIFA HILO


Ikiwa ni siku mbili zimepita toka waziri wa mambo ya ndani wa Burundi, Edouard Nduwimana kutangaza kukifungia kwa miezi minne chama cha upinzani cha MSD, kinachoongozwa na Alexis Sinduhije, mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na wanahabari nchini humo wamemuandikia barua ya wazi rais wa jamhuri, Pierre Nkurunziza kuzingatia suala la usalama wa nchi.

Tamko hilo la mashirika ya kiraia yenye uhisiano na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC pamoja na wanahabari, limekuja kufuatia madai yao kuwa serikali inalenga kuminya uhuru wa demokrasia kwa kuzuia vyama vya siasa kutekeleza majukumu yao pamoja na wanahabari kuripoti habari zao hali inayotishia uwezekano wa kutokea vurugu nchini humo hata kabla ya uchaguzi mkuu.

Wachambuzi wa masuala ya siasa nao wanaona kuwa bado hali ya demokrasia nchini Burundi ni tete na imewekwa rehani na watu wachache

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...