Msuluhishi
wa Umoja wa Afrika katika mgogoro wa Sudani rais wa zamani wa Afrika
Kisini Thabo Mbeki amewasili jijini Khartoum kwa ajili ya kusaidi
kushinikiza mazungumzo ya amani karti ya serikali na waasi wa jimbo
la Kordofan kabla ya kuanza kwa mazungumzo jijini Addis Ababa nchini
Ethiopia.
Mazungumzo
kati ya wajumbe wa serikali ya rais Omar hassan al Bashir na waasi wa
jimbo la Kordofan yanatarajiwa siku ya Ijumaa mjini Addis Abeba
nchini Ethiopia.
Msuluhishi
wa Umoja wa Afrika Thabo Mbeki ambaye ni rais wa zamani wa Afrika
Kusini anafanya ziara jijini Karthoum itayofuatiwa na mkutano wa tume
ya pande tatu ya kimataifa ilioundwa katika mazungumzo ya amani
mwaka 2011 kati ya serikali ya Kharthoum na kundi hasimu la waasi wa
Kordofan.
Hayo
yanajiri wakati pande hizo mbili husika na mzozo nchini Sudani
zinajadili kuhusu pendekezo lililotolewa na msuluhishi wa Umoja wa
Afrika juu ya usitishwaji mapigano utaoruhusu mashirika ya misaada
kuwafikia mamia ya watu waliokwama katika eneo la machafuko na ambao
wanahitaji msaada wa kibinadamu.
Usuluhisi
ulitowa pendekezo hilo kwa nyakati tofauti kwa serikali ya Khartoum
na waasi wa kundi la SPLM-N baada ya kuahirisha mazungumzo jijini
Addis Abeba. Pande hizo mbili zinatuhumiana kutokuwa na nia thabiti
ya kumaliza machafuko.
Mazungumzo
kati ys Karthoum na waasi yanalenga kusitisha mzozo wa miaka mitatu
katika eneo la Kordofan Kusini na Nile Bleu, mzozo uliowagusa watu
zaidi ya milioni moja.
Hadi
sasa haijulikani takwimu za watu walipoteza maisha katika majimbo ya
Kordofan Kusini na Bleu Nile, lakini Umoja wa Mataifa unasema
takriban watu milioni moja na nusu wameguswa na mzozo huo.