Pages

vendredi 22 août 2014

NAVI PILLAYALAUMU UDHAIFU ULIOPO KWENYE BARWZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA


Kamishna wa haki za binadamu kwenye Umoja wa mataifa ambaye anaachia ngazi, amelaumu jana kuhusu udhaifu wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa kushindwa kkumaliza mgogoro katika maeneo kadhaa dunianikwa sababu ya kiwango cha maambukizi ya maslahi ya taifa.

Navy Pillay amesema Wanachama wa baraza la Usalama wanashindwa mara kadhaa kuchukuwa maamuzi na kuwawajibisha viongozi wanaohusika na mizozo, ameendelea kusisitiza hivo kiongozi huyo wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa aliyejiuzulu na ambaye anataraji kuondoka rasmi kwenye uongozi huu katika siku za hivi karibuni.

Navy Pilay amesema anafkiri kwamba maamuzi sahihi ya baraza la usalama ndio yanayoweza kuokoa maisha ya mamia ya watu duniani wanaokabiliwa na hali duni wakati huu kutokana na mizozo inayo wakumba katika nchi zao.

Kiongozi huyo raia wa Afrika Kusini amesema kuwa matumizi ya kura ya turufu kwenye barqaza la Usalama la umoja wa mataifa limekuwa kikwazo kikubwa kwa mataifa mengine kuchukuwa maamuzi.


MAREKANI YASISITIZA AZMA YAKE YA KULISHAMBULIA KUNDI LA ISLAMIC STATE



Serikali ya marekani imeendelea kushikilia uamuzi wake wa kuchukua hatua dhidi ya wanajihadi wa Dola laa Kiislamu linalo onekana kuwa hatari, na kuahidi kuendeleza mashambulizi nchini humo licha ya tishio la kundi hilo lawatu wenye msimamo mkali kutishia kumchinja mateka mwengine wa marekani baada ya kutekeleza kitendo hicho kwa muandishbi wa habari James Foley.

Mjini Geneva, Kamishna wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, Navi Pillay amelaumu kuhusu hatuwa ya kupooza kwa kushughuli za Jumuiya ya kimataifa, jambo ambalo linalo chochea kuibuka kwa wauaji, waharibifu na watesaji katika nchi za Syria na Iraq.


wakati Jumuiya ya kimataifa ikizuia kutowa msaada wa kupatikana kwa suluhu katika mzozo unaondelea nchini Syria, washington na baadhi ya washirika wake wamewapa silaha waasi wa kikurdi ili kupambana na kundi la dola la kiislam na kuandaa mkakati wa kudumu ili kujaribu kulitokomeza kabisa kundi hili lililoitwa kama Kansa ya dunia na rais Barack Obama.

DRCONGO YATISHIA KUSITISHA SHUGHULI ZA KUWASAFIRISHA WAKIMBIZI WA ANGOLA NCHINI KWAO


Serikali ya Jamhuri ya kidemirsia ya Congo imetishia kusitisha shughuli za kuwarejesha nyumbani wakimbizi takriban elfu 29 wa Angola iwapo kutaibuka tena dosari mpakani wakati huu viongozi wa Angola wakizuia watu 66 kuingia nchini kwao.
Mengi zaidi na Reuben lukumbuka.

waziri wa mambo ya ndani nchini jamuri ya kidemokrasia ya Congo Richard Muyej amesema iwapo dosari zitajitokeza tena kama ilivyo shuhdiwa hapo awali, watasitisha mara moja shughuli hizo na kuomba kukutana na viongozi wa Angola kwa ajili ya kupanga mikakati mipya kwa ajili ya kukamilisha shughuli hiyo.

Waziri huyo amesema anaamini kwamba dosari zipo up-iande wa vingozi wa Angola.

Takriban raia elfu 29 wa Angola waliopewa hifadhi nchini DRCongo wamemauwa kurejea nchini kwa kwa hiari. Wengine elfu 76 tayari wamerejea nchini kwao tangu mwaka uliopita wakati ilipoanza operesheni ya kuwarejesha nyumbani zilizoandaliwa na viongozi wa DRCongo, Angola, na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayowahudumia wakimbizi duniani UNHCR.

Jumanne juma hili kundi la kwanza lienye wakimbizi 500 liliondoka jijini Kinshasa kuelekea nchini Angola, lakini walipofika mpakani 182 walizuiliwa mpakani na hivyo serikali ya Congo inaluamu kutokana na kile ilichokiita udhaifu upande wa Angola katika kukamilisha shughuli hiyo kwa kutowatuma wataalamu nchini DRCongo kwa ajiloi ya kuwakaguwa wakimbizi hao, shughuli ilioendeshwa pekee na serikali ya Congo kwa ushirikiano na UNHCR



Baada ya mabishano ya muda mrefu, wakimbizi 116 waliruhusiwa kuvuka mpaka, lakini wengine 66 wakazuiliwa mpakani baada ya viongozi wa mpakani kukataa vibali walivyopewa kutoka ubalozi wa Angola jijini Kinshasa.


HAMAS YAWAUWA WAPALESTINA 18 KWA KOSA LA UHAINI


Kituo cha televishieni cha kundi la Hamas katika ukanda wa gaza kimefahamisha kwamba Watu 18 wamenyongwa katika ukanda wa Gaza baada ya kutuhumiwa kushirikiana na Israel. Miongoni mwao, sita wamenyongwa hadharani, baada ya salama ya Jumaa, tukio lilotekelezwa na watu walivalia sare ya wapiganaji wa Brigade Ezzedine al Qassam tawi la kijeshi la kundi la Hamas.

Watu hao wanatuhumiwa kutowa taarifa kwa jeshi la Israel kuhusu wapi walipokuwa viongozi watatu wakijeshi wa kundi la Ezzedine al Kassam waliouawa katika shambulio, huku kiongozi mkuu wa kundi hilo akinusurika kifo katika shambulio lililogharimu maisha ya watu 3 wa familia yake.

Hayo yanajiri wakati huu kiongozi muu wa jumuiya ya waislam Amir wa nchini Qatar akikutana kwa mara ya pili katika kipindi cha saa 24 na kiongozi wa mamlaka ya wa Palestina na kiongozi wa Hamas Khaled Mechaal wakati huu mashmbulizi ya Israel yakiendelea kushuhudiwa katika ukanda wa Gaza.


Takriban watu 4 wamepoteza maisha ijumaa hii kufuatia mashambuliz ya vikosi vya Israel katika ukanda wa Gaza, ikiwa ni siku ya 46 ya mashambulizi kati ya kundi la Hamas na vikosi vya Hamas.

vendredi 15 août 2014

MSANII WA UGANDA BOBI WINE ANYIMWA VISA KUINGIA UINGEREZA


Rapa maharufu wa Uganda Bobi Wine amenyimwa visa ya kuingia nchini Uingereza kwa sababu ya matamshi ya kuhusu ushoga ambapo raia wa Uingereza wamelaumu katika pingamizi lililosainiwa na zaidi ya watu 600.

Bobi Wine ambaye alipanga kuzuru maeneo ya Goodbye Buckingham Palace, Big Ben na Westminster Abbey na ambako alifanya tamasha katika eneo hilo, amekataliwa kupewa visa baada ya kutuhumiwa kuwa na matamshi mabaya dhidi ya watu wanafanya mapenzi ya jinsi moja.

Katika moja ya sentesi ya wimbo wake Bobi Wine anaweka wazi msimamo wake kuhusu ushoga ambapo anawatolea wito wanancni wa Uganda kuwateketeza bila kuwataja watu aliowaita wapungufu wa akili.

Wanaharakati watetezi wa haki za mashoga walizindua kampeni online kupiga marufuku tamasha za msanii huyo nchini Uingereza



jeudi 14 août 2014

CHANZO CHA MOTO ULIOTEKETEZA MUSIKITI WA MTAMBANI NCHINI TANZANIA CHAELEZWA KUWA NI HITILAFU YA UMEME

Hapo jana usiku nchini Tanzania katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, moto mkubwa uliwaka katika eneo la juu la shule ya Sekondari ya kiislam ya Mivumono (Mivuno Islamic Secondary) iliyopo ndani ya msikiti wa Mtambani Kinondoni B, jijini Dar es Salaam.

Moto huo uliteketeza eneo lililokuwa likitumika kama mabweni ya wanafunzi wa shule hiyo, maabara na ofisi za walimu, eneo hilo limeteketea kabisa kiasi kwamba hakuna kilichoweza kuokolewa.

Chanzo cha moto huo kinadaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme iliyokuwepo kwenye bweni la wasichana wanafunzi wa shule hiyo ila hadi moto huo unafanikiwa kuzimwa hakuna mtu yeyote aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa.

mercredi 13 août 2014

WAASI WA KIHUTU WA FDLR WAKATAA KWENDA KISANGANI


Waasi wa Kihutu waliopiga kambi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa FDLR wamekataa kuondoka katika kambi ya Kanyabayonga iliotengwsa kuwakusanya kuelekea mjini Kisangani.

Mashirika ya kiraia na shirika la Umoja wa Mataifa nchini DRCongo yamesema kuguswa sana hatuwa hiyo ya wapiganani hao wa FDLR ambao wanatakiwa kuondolewa katika maeneo ya kivu kaskazini na na Kivu Kusini na kuepelekwa mjini Kisangani kabla ya kuondolewa katika ardhi ya DRCongo.

waasi hao wanasema hawakuwa na taarifa ya kuondoka wakati tayari Umoja wa Mtaifa nchini DRCongo ulikuwa umetenga malori yatayo wasafirisha kuelekea kisangani wakati ambapo Umoja wa Mataifa unasema tangu mapema taarifa ya kuondoka kuelekea Kisangani inafahamika kitambo.


Hata hivyo katribu mtendani wa kundi hilo la FDLR Wilson Irategeka amesema wananchi wa aKisangani na mashrika ya kiraia ndio yamekataa kuwaona mjini Kisangani, jambo ambalo limekanushwa na mwenyekiti wa mashirika ya kiraia katika Mkoa wa Kivu Thomas d'Aquin.

WAIGIZAJI WAWILI WAPIGWA MARUFUKU KURIKODI KATIKA STUDIO ZA HOLLY WOOD


Penelope Cruz na Javier Bardem Ni waigizaji wakubwa katika industry ya filamu nchini Marekani, wamepigwa marufuku kurikodi katika baadhi ya stdio za Hollywood nchini Marekani kutokana na kuonyesha msimamo wao kuhusu mzozo wa Israel na Gaza.

Waigizaji hawa, wamepinga kile kilichotekelezwa na Israel katika Ukanda wa Gaza, hatua iliopelekea wao kupigwa marufuku.

MAREKANI YAONGEZA WANAJESHI 130 NCHINI IRAQ

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuk Hagel na rais Barack Obama

Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuk Hagel amefahamisha kwamba washauri wengine 130 wa kijeshi watatumwa nchini Iraq katika mji wa Erbil mji mkuu wa Kurdistan kutathimini zaidi mahitaji ya watu wa kabila la wa Yazid waliofukuzwa hivi karibuni katika makaazi yao na wapiganaji wa kiislam wanataka kuunda taifa la Kiislam.

Kulingana na taarifa ya jeshi la Marekani, washauri hao wa kijeshi watakuwa na jukumu la kupanga na kuratibu miradi ya kibinadamu kwa wananchi hao wachacha wa kabila la Yazid.

Wanajeshi hao wanakamilishai idadi ya washauri mia tatu wa kijeshi ambao rais Barack Obama alitangaza mwezi Juni kuwatuma nchini Iraq kusaidia serikali ya Iraq kuzuia mashambulizi ya kundiu la Isil lililokuwa likiendelea kuiteka miji kadhaa nchini humo.


katika hatuwa nyingine vikosi vya Marekani tayari vimefanya operesheni 17 tangu siku ya Ijumaa kuzuia kundi la Isil kuendelea kusonga mbele kwenye uwanja wa mapambano.

SERIKALI MPYA YASUBIRIWA NCHINI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI


Wakati wananchi wa jamhuri ya Afrika ya kati wakisubiri kutangazwa kwa baraza jipya la mawaziri, wachambuzi wa mambo wanaonakuwa baraza hilo jipya litakabiliwa na chamgamoto kubwa hususan kupatikana kwa misaada ya kibinadamu na kuwaunganisha wananchi wa taifa hilo waliogawanyika kwa misingi ya kikabila na kidini.
Idadi ya watu waliotoroka makwao kutokana na machafuko yalioikumba nchi hiyo imeonekana kupungua kidogo ukilinganisha na mwezi Januari mwaka huu ambapo idadi hiyo ilifikia zaidi ya watu milioni moja. Wakimbizi waliokimbia katika maeneo ya misitu wakati huu wanakabiliwa na matatizo chungu nzima hususan ukosefu wa misaada ya kibinadamu huku wengine wakieshi katika mazingira yenye usalama mdogo.


Mbali na wakimbizi hao wa ndani kuna idadi nyingine ya raia wa jamhuri ya Afrika ya kati waliokimbilia nje ya taifa hilo hususan nchini Tchad na Camaroun ambapo mashirika ya kimisaada yanakadiria kufikia wakimbizi laki nne ambao wapo nje ya nchi na ambao wengi wao ni waislam waliokimbia machafuko ya wanamgambo wa Anti Balaka.

mardi 12 août 2014

RAIS OBAMA APONGEZA HATUWA YA KUTEULIWA KWA WAZIRI MKUU MPYA NCHINI IRAQ


Rais wa Marekani Barack Obama amepongeza jana hatuwa ya kuteuliwa kwa aliyekuwa naibu spika wa bunge Haidar al Abadin kuwa waziri mkuu mpya nchini Iraq katika hotuba yake ambayo ililenga pia kutowa ujumbe kwa waziri mkuu alieondolewa madarakani licha ya kutomtaja moja kwa moja na ambaye ameonyesha nia ya kutoachia madaraka.

Akizungumza akiwa katika kisiwa cha Martha's Vineyard katika jimbo la Massachusetts kaskazini mashariki ambako yupo likizo na familia yake, Obama amefahamisha kwamba ameahidi uungwaji wake mkono kwa waziri mkuu mpya Haïdar al-Abadin na amewatolea wito viongozi wote wa kisiasa nchini Irak kufanyakazi kwa mshikamano.

Rais Obama amesisitiza kuhusu hatuwa ya kuunda baraza la mawaziri hara iwezekanavyo itayo shirikisha pande zote kwa manufaa ya wananchi wote wa irak na ambayo itapambana na kundi la wapiganaji wa kiislam la Isil.

Hapo jana waziri mkuu wa zamani Nuri Al Malik ambaye utawala wake umekuwa ukikosolewa vikali na Marekani tangu kipindi kadhaa, amemtuhumu rais wa nchi hiyo kwa kuvunja katiba baada ya kuchukuwa hatuwa ya kumteuwa waziri mkuu mpya wakati muhula wake bado haujatamatika.

lundi 11 août 2014

MSHUKIWA WA EBOLA NCHINI RWANDA AZUILIWA JIJINI KIGALI


Serikali ya Rwanda imetangaza jana kwamba mtu mmoja anaeonyesha dalili za maradhi ya Ebola amewekwa mahali pa pekeake mjini Kigali huku uchunguzi ukiendelea zaidi kubaini iwapo ni maradhi ya Ebola au ni homa ya kawaida.

Kulingana na ujumbe wa waziri wa Afya Agnes Binagwaho kwenye mtandao wake wa Twitter mtu huyo raia a Ujerumani amwekwa katika eneo la pekeake kwenye Hospital ya mfalme Faisal ambaye anaonyesha dalili za mardhi ya Ebola na matokeo yatafahamishwa kwa muda saa 48 zijazo.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kuwepo kwa mshukiwa wa kwanza wa maradhi ya Ebola nchini Rwanda, maradhi yanayo sumbuwa na kutikisa nchi za Afrika Magharibi tangu mwanzoni mwa mwaka.

Mwanafunzi huyo raia wa Ujerumani alikuwa nchini Liberia kabla ya kuwasili nchini Rwanda.

WAZIRI MKUU WA IRAQ ATANGAZA KUMFUNGULIA MASHTAKA RAIS WA NCHI HIYO


Wakati hali ikiendelea kuwa mbaya kwenye uwanja wa mapambano nchini Iraq kufuatia kundi la Isil kuendelea kujizatiti katika miji kadhaa kaskazini mwa nchi hiyo, mvutano wa wazi umeibuka kati ya rais Fouad Masoum na waziri mkuu Nuri al Malik ambaye ametangaza jana kuwa atamfunuglia mashtaka rais,

Muda mfupi baada ya waziri mkuu wa Iraq Nuri al Malik kutangaza hatuwa yake ya kumfungulia mashtaka rais wa nchi hiyo Fouad Masoum, kwa tuhuma za kukiuka katika ya nchi hiyo, askari wengi wameshuhudiwa katika maeneo muhimu ya jiji la Bagdad.

Duru kutoka jijini Bagdad zimearifu kuwa kwa hali isiokuwa ya kawaida, askari wengi wameonekana katika maeneo ya taasisi za serikali huku barabara kadha za jiji zikifungwa, saa chache baada ya waziri Malik kutangaza ghafla kuwa anaenda kufunguwa mashartaka dhidi ya rais.

Serikali ya Marekani kupitia ujumbe wa Twitter, naibu waziri wa mambo ya nje anayehusika na maswala ya Iraq Brett McGurk, imesema itaendelea kumuunga mkono rais wa nchi hiyo Fouad Masoum ambaye ndiye mlinzi halali wa taasisi za serikali pamoja na waziri mkuu ataye kubalika na pande zote.

Nuri al Malik kutoka jamii ya ma shia ambaye alishinda uchaguzi mwezi April 30 iliopita na ambaye analenga kuwania muhula mwingine wa tatu, amekuwa akikosolewa sana na sera yake ambayo wengi wanasema ni ya kibaguzi dhidi ya watu wa chache wa jamii ya wa Sunni.

Bunge la taifa nchini humo ambalo lilitakiwa kukutana jana kujadili kuhusu swala la kupatikana kwa waziri mkuu anaye kubalika na pande zote, imeahirisha kikao chake hadi Agosti 19 baada ya kutotimia kwa idadi.






VIONGOZI WA SUDANI KUSINI WASHINDWA KUUNDA SERIKALI YA MUUNGANO WA KITAIFA


Licha ya vitisho vya Umoja wa Mataifa vya kutiliwa vikwazo kwa viongozi wa Sudani Kusini, Pande mbili zinazo zozana nchini Sudani Kusini zimeshindwa kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa kama ilivyoagizwa katika mazungumzo yaliowakutanisha rais wa Sudani Kusini Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar na ambapo muda wa mwisho ulikuwa jana.

Mei 9 mwaka huu, Salva Kiir na mpizani wake ambaye aliwa makam wake wa rais Riek Machar walifikia makubaliano chini ya shinikizo la Jumuiya Kimataifa kugawana madaraka yalioagiza kuunda serikali ya muungano wa kitaifa kwa kipindi cha siku 60.

machafuko na mauaji yenye misingi ya kikabila yameendelea kushuhudiwa nchini humo tangu desemba mwaka 2013 huku takwimu zikionyesha kuwa watu zaidi ya milioni moja na nusu wameyatoroka ma kwao kutokana na machafuko hayo.


Wananchi wa Sudani Kusini walikuwa na matumaini baada ya kufikiwa kwa makubaliano hayo, lakini matumaini yameanza kufifia baada ya pande mbili kushindwa kuweka kando tofauti zao na kutekeleza makubaliano yao.

MAPIGANO MAPYA YAZUKA NCHINI LIBYA


Mapigano yamezuka tena upya nchini Libya baada ya kushuhudiwa ukimya wa siku kadhaa wakati huu ujumbe wa Umoja wa Mataifa UN ukifanya ziara jijini Tripoli kwa ajili ya kuwaleta pamoja mahasimu na kupatikana kwa usitishwaji wa mapigano.

Milipuko na milio ya risase imesikika katika mapigano mapya baina ya makundi mawili hasimu yakiwania kuudhibiti uwanja wa ndege wa jijini Tripoli.


Hakuna matumaini yoyote ya kupatikana kwa usitishwaji wa mapigano hayo yanayo lenga kuwaondowa kwenye uwanja wa ndege wapiganaji wa makundi la Kiislam wenye asili ya miji wa Misrata, Gharyan na Zawiya.

vendredi 8 août 2014

RAIS WA KENYA ASISITIZA KUWA WANAJESHI WA KENYA WATASALIA SOMALIA


Siku moja baada ya kuhitimishwa kwa mkutano wa kimataifa kati ya Marekani na viongozi wa Afrika ambapo suala la usalama kwenye bara hilo lilijadiliwa kwa kina na viongozi hao, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameendelea kusisitiza nchi yake kutoondoa majeshi yake Somalia.

Rais Kenyatta amesema kuwa kamwe serikali yake haitavirudisha nyumbani vikosi vyake vilivyoko Somalia mpaka pale nchi yake itakapo hakikisha kuwa Somalia ina Serikali yenye nguvu na inayoweza kusimamia mipaka yake.


Kauli hii ameitoa wakati akijibu maswali ya raia wa nchi hiyo wanaoishi Marekani ambapo walitaka kufahamu ni hatua gani Serikali ya Kenya inachukua kunusuru mashambulizi ya Al-Shabab ambao wanataka wanajeshi wao kuondoka Somalia.

WANADIPLOMASIA WA UMOJA WA UALAYA WATIWA WASI WASI NA HATUWA YA KUZIULIWA KWA MPINZANI JIJINI KISHASA


Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya walioko mjini Kinshasa- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameelezea wasiwasi wao baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Jean Bertrand Ewanga, Mbunge na Katibu mkuu wa chama cha upinzani cha UNC cha bwana Vital Kamerhe siku ya Jumanne tarehe 5 mwezi Agosti mwaka huu.


Mabalozi hao, Luc Hallade wa Ufaransa, Michel Latshenko wa Ubelgiji, na Naibu Balozi wa Uingereza, John Lamb, kwa pamoja wamebaini wasiwasi wao kwa spika wa Bunge nchini DRC Aubin Minaku na kutoa wito kwa serikali ya Congo kuchukua hatua mahususi ili kutowa uhuru na haki ya kujieleza

NCHI ZA AFRIKA MAGHARIBI ZATANGAZA HALI YA HATARI KWA KUZIDIWA NA IDADI YA VIFO KUTOKANA NA EBOLA


Nchi za Afrika Magharibi zimetangaza hali ya hatari kwa kuzidiwa na idadi ya vifo kutokana na Ugonjwa wa Ebola ambapo watu wapatao elfu moja sasa wanaripotiwa kufa kwa maambukizi ya virusi hivyo.

Hali hiyo imetangazwa wakati Bunge la nchi ya Liberia limekutana kwa dharura kupitisha sheria ya kuweka vizuwizi vya barabarani na kikomo cha usafiri kwa watu wanaoelekea mji mkuu wa Monrovia nchini humo na kuridhia siku 90 ya hali ya hatari.

Aidha, miji miwili mashariki mwa nchi ya Sierra Leone, Kailahun na Kenema, imewekwa chini ya hali ya tahadhari kufwatia kauli ya msemaji wa serikali siku ya Alhamis kuamuru shughuli za vilabu vya usiku na sehemu za burudani na starehe kufungwa.

Madaktari wa sekta ya umma nchini Nigeria kwa upande wao wamesitisha mgomo wao wa mwezi mmoja kwa hofu ya ongezeko la maambukizi katika nchi ambayo ni ya kwanza barani Afrika kwa idadi ya wakazi wake na ambapo vifo vya watu wawili na maambukizi ya watu watano vimeripotiwa mjini Lagos.

Wakati hayo yakijiri, Shirika la Afya duniani WHO linatarajiwa hii leo kujadili ikiwa litatangaza hali ya "hatari ya afya kimataifa" katika mkutano wake wa dharura mjini Geneva- Uswisi, pamoja na hatua mpya ikiwa ni pamoja na vikwazo vya kusafiri kimataifa, hasa baada ya serikali ya Uhispania kutuma helikopta ya kijeshi kumrejesha nchini humo daktari Juliana Bonoha Bohe ambaye alifanya kazi katika hospitali moja mjini Monrovia.

IDADI YA VIVO ITOKANAYO NA EBOLA YAONGEZEKA


Idadi ya vifo inayotokana na maradhi ya virusi vya Ebola inaelezwa kufikia zaidi ya watu elfu 1 wakati huu kukiwa na hofu kuwa huenda nchi ya Nigeria ikawa ni taifa jingine ambalo linakabiliwa na hatari ya kukumbwa na janga hili wakati huu mgonjwa wa pili akiripotiwa kufa nchini humo.

Kusambaa kwa virusi vya ebola kwenye mataifa ya Afrika na baadhi ya mataifa ya magharibi kunakuja wakati huu ambapo shirika la afya duniani linakutana na wataalamu wa afya duniani kuamua iwapo watangaze kuwa ugonjwa wa Ebola ni janga la dunia.


Zaidi ya watu elfu 1 na 700 kwenye nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone wamegunduliwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola wakati huu nchi za Marekani na Saudi Arabia nazo zikiripoti kuwa na wagonjwa wapya.

mercredi 6 août 2014

MKUTANO WA MAREKANI NA VIONGOZI WA AFRIKA KUTAMATIKA LEO


Ikiwa hii leo ndio kilele cha mkutano wa kimataifa kati ya viongozi wa bara la Afrika na Marekani, tayari mkutano huo umeza matunda ambapo rais Barack Obama ametangaza uwekezaji wa nchi yake barani Afrika unaofikia kiasi cha dola bilioni 33.

Rais Obama amesema kuwa wafanyabiashara nchi humo wametenga kiasi cha dola bilioni 14 kwenye uwekezaji wa maeneo tofauti huku kiasi kingine cha bilioni 12 kikitengwa kwaajili ya uwekezaji kwenye sekta ya nishati.


Akiwahutubia wajumbe wa mkutano huo, rais wa zamani wa Marekani Billy Clinton amesisitiza nchi ya Marekani kuwa rafiki wa karibu wa bara la Afrika kwenye shughuli za kimaendeleo na kwamba siku za usoni bara hilo litakuwa linategemewa na dunia.

WAZIRI WA KWANZA MWANAMKE KATIKA SERIKALI YA UINGEREZA AJIUZULU


Saa chache baada ya kujiuzulu kwa mmoja wa mawaziri kwenye ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya Uingereza na mwanamke wa kwanza muislamu kushika wadhifa huo, uamuzi wake umekosolewa na baadhi ya mawaziri wenzake.

Baroness Sayeeda Warsi waziri aliyekuwa akihusika na masuala ya imani na jamii kwenye serikali ya waziri mkuu David Cameroon, ametangaza uamuzi wake katika kile alichodai ni sera mbovu ya nchi hiyo kuhusu eneo la mashariki ya kati na has mzozo kati ya Israel na Palestina.


Umuzi wake umekosolewa vikali na waziri anayehusika na masuala ya hazina nchini humo George Osbone ambaye anaona kuwa umuzi wa haukuwa sahihi wala haukuwa na mantiki kwakuwa suala la mzozo wa Palestina lilikuwa linashughulikiwa kidiplomasia.

MAREKANI YASEMA WAASI WA FDLR LAZIMA WAJISALIMISHE


Serikali ya Washington imeonya kuwa waasi wa zamani wa kihutu kutoka Rwanda waliopiga kambi mashariki mwa DRCongo wa FDLR lazima wajisalimishe ili kuepuka kuchukuliwa hatuwa za kijeshi zenye lengo la kulisambaratisha kundi hilo.

Mjumbe maalum wa Marekani katika Ukanda wa maziwa makuu Russ Feingold amefahamisha kuwa viongozi wa nchi za ukanda wa maziwa makuu watakutana kwenye Umoja wa Mataifa siku ya alhamisi ili kujadili kuhusu hatuwa za kuchukuwa dhidi ya kundi la FDLR.

Kiongozi huyo amesema waasi hao wa zamani wanatakiwa kijisalimisha kwa wingi la sivyo hatuwa za kijeshi zitachukuliwa. Feingold anaona kuwa hakuna sababu zozote za kundi hilo kutaka majadiliano ya kisiasa na kundi hilo lazima livunjwe kabla ya mwisho w mwaka huu wa 2014.


wapiganaji takriban 200 wa kundi hilo walijisalmisha mwezi Mei, kwa sasa mchakato huo ambao ulitakiwa kuendelea lakini sasa umesimama. 

mardi 5 août 2014

VSV YATAKA KUACHWA HURU KWA WATU WALIOTEKWA JIJINI KINSHASA


Shirika lisilokuwa la kiserikali la Voix de sans Voix nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limsema Watu 11 akiwemo mtetezi wa haki za binadamu wametekwa nyara mwishoni mwa juma lililopita jijini Kinshasa na kundi la watu waliovalia sare za kawaida na wengine za jeshi

kwa mujibu wa shirika hilo la VSV tukio hilo limetekelwa na kundi la watu waliokuwa wamevalia sare mchanganyiko jeshi, polisi na za raia na walikuwa katika gari la polisi na kupelekwa katika eneo lisilojulikana bado.

Taarifa zaidi zinasema kuwa watu hao 11 walikuwa kanisani wakifanya maombi kwa ajili ya wagonjwa, na haijulikani lengo la tukio hilo, hata hivyo shirika hilo limesema mmoja kati ya watekaji nyara alisema kuwa wamepata kile walichokuwa wanatafuta.

Shirika hilo linaombwa kuachiwa huru kwa watu hao.



ISRAEL NA HAMAS WASITISHA VITA KWA SAA 72


Serikali ya Israel na kundi la Hamas la nchini Palestina wamekubaliana kimsingi kutoa muda wa saa 72 kusitisha mapigano kwenye eneo la ukanda wa Gaza baada ya kuongezeka kwa shinikizo toka jumuiya ya kimataifa kuzitaka pande hizo kusitisha vita iliyodumu kwa siku 29 sasa.

Makubaliano haya yamefikiwa mjini Cairo Misri, ikiwa ni siku tatu tu zimepita toka makubaliano ya awali ya kutoa siku tatu za kusitisha vita kushindikana kutokana na kila upande kuendelea na mapigano.


Marekani imepongeza uamuzi huo na kusisitiza kuwa ni kundi la Hamas pekee ndilo linalotakiwa kuheshimu makubaliano haya.

OBAMA AWATAKA VIONGOZI WA AFRIKA KUHESHIMU MUDA WA KUSALIA MADARAKANI


Serikali ya Marekani imewataka viongozi wa bara la Afrika kuheshimu tofauti za kisiasa zilizoko nchini mwao na kuwa na uvumilivu wa kisiasa ambao ndio nguzi kuu ya kuwa na demokrasia ya kweli katika kufikia mafanikio ya muda mrefu.

Rais Obama amewataka ma rais walipo madarakani bara Afrika kuheshimi muda waliopewa na katiba kukaa madarakani

Wito huu umetolewa wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya viongozi hao na rais Barack Obama, ambaye alitumia siku ya kwanza ya mkutano huu, kusisitiza masuala ya usalama, biashara na demokrasia kama msingi mkuu utakaoshuhudia nchi za Afrika zikipata maendeleo ya haraka.


Kuhusu biashara, rais Obama amesema kuwa haoni shida nchi ya China kuwa mwekezaji mkubwa barani Afrika lakini akaonya kuhusu uwekezaji unaofanywa na taifa hilo na kuwataka viongozi hao kuwa makini na rasilimali ambazo China imekuwa ikizilenga kwenye bara hilo.

MAPIGANO YACHACHA WAKATI MAZUNGUMZO YA AMANI YAKIZINDULIWA NCHINI SUDANI KUSINI



Mazungumzo ya amani kuhusu kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini yameanza Jumatatu ya wiki hii mjini Addis Ababa, huku kukishuhudiwa mapigano makali kwenye baadhi ya maeneo.

Wakati huu wajumbe wa mazungumzo haya wakiendelea kuwasili mjini Addis Ababa, makundi ya wapiganaji wenye silaha kwenye jimbo la Upper Nile wamekabiliana na wanajeshi walioasi kwa siku ya pili huku kukishuhidiwa mfanyakazi mmoja wa shirika la misaada akiuawa kutokana na mapigano haya.

Tume ya Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS imesema kwenye taarifa yake, kuwa inaguswa na hali ya kuendelea kushuhudiwa kuzorota kwa usalama nchini humo hasa kwenye miji ya Bunj na jimbo la Upper Nile ambako kuna zaidi ya wakimbizi laki 1 na elfu 25 wanaotoka Sudan.

Kwenye mazungumzo yaliyofunguliwa jana Jumatatu, wapatanishi wa mzozo huo wamewaonya viongozi wanaohasimiana kuhusu hatua ambazo zitachukuliwa dhidi yao iwapo mapigano hayatakomeshwa.

Jumuiya ya maendeleo ya nchi za Afrika mashariki IGAD ambayo ndio inayosimamia mazungumzo haya imeweka makataa ya hadi kufikia tarehe 10 ya mwezi huu kwa viongozi hawa kufikia makubaliano kuhusu serikali ya mpito.


Mazungumzo ya mwisho kati ya rais Salva kiir na aliyekuwa makamu wake wa rais Riek Machar yalikwama mwezi June mwaka huu baada ya kila upande kumtuhumu mwenzake kwa kukiuka mkataba waliotiliana saini.

lundi 4 août 2014

UMOJA WA MATAIFA WALAANI MAKOMBORA YA ISRAEL KATIKA SHULE LA UMOJA WA MATAIFA


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani makombora yaliyorushwa kwenye shule moja ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumapili na kusababisha mauaji ya raia wa kiPalestina wapatao kumi katika shambulio lililotekelezwa na askari wa Israeli.

Shambulio hilo limedhihirisha wazi ukiukwaji mwingine wa sheria za kimataifa ambapo pande zote mbili zililazimika kulinda usalama wa raia hao wa Palestina, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na majengo ya Umoja huo, amesema msemaji wa Katibu Mkuu katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Aidha, msemaji huyo amesisitiza kuwa lazima Makazi ya Umoja wa Mataifa yawe sehemu rasmi ya kukimbilia na si eneo la mapambano kama ilivyojitokeza mara kadhaa na kuwa lazima wahusika wa mashambulio hayo wachunguzwe na kuwajibishwa.

Katibu Mkuu Ban Ki Moon ameelezea kusononeshwa na ukiukwaji huo wa sheria za kimataifa na kubainisha kuwa serikali ya Israeli, licha ya kuwa imefahamishwa maeneo ambapo Umoja wa Mataifa umepiga kambi, askari wake wanaendelea kutekeleza vitendo vya uhalifu ambavyo Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa havikubaliki.


Tangu uvunjwaji wa Makubaliano ya kusitisha mashambulizi ya tarehe mosi Agosti, mamia ya raia wa Palestina tayari wameuwawa kutokana na mashambulizi hayo huku hali ya kibinadamu ikiendelea kuwa mbaya zaidi katika Ukanda wa Gaza, wakati ambapo Ban Ki-moon akitoa wito wake kwa pande zote kusitisha mapigano mara moja na kurejelea meza ya mazungumzo mjini Cairo, Misri.

MAWASILIANO YA SIM YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI JOHN KERRY YANASWA


Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika gazeti moja nchini Ujerumani, mawasiliano ya sim ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry yalifanyiwa udukuzi na nchi mbili ikiwemo Marekani.

Taarifa inakumbusha kashafa kama hiyo ya udukuzi wa mawasliano ya sim ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel na kituo cha Usalama wa taifa cha Marekani NSA, ambapo sasa vyombo vya habari nchini Ujerumani na hata kwenye mitandao ya kijamii.

Gazeti la kila wiki la Der Spiegel limeariku kuwa mawasiliano ya simu ya John kerry yalinaswa na idara ya usalama ya Israel katika kipindi chaote hiki cha majadiliano kati yake na Israel pamoja na Palestina ambayo yalifeli hivi karibuni .

Hata hivyo gazeti hilo la Spigiel halikuthibitisha iwapo mawasiliano ya kiongozi huyo wajuu nchini Marekani yalinaswa wakati huu wa mapigano mjini Gaza.

WAGENI WAENDELEA KUIKIMBIA LIBYA


Shuguhuli za uzinduzi wa bunge jipya nchini Libya zimeitishwa kufanyika jumatatu hii katika miji wa Tobrouk na upande wa chama cha wazalendo na tripoli na chama cha waislam wakati huu mauaji yakiendelea huku wageni na raia wa kawaida wakiendelea kuikimbia nchi hiyo kutokana na mapigano


katika mji mkuu Tripoli mapigano yaliozuka tangu Julay 13 yanaendelea kushuhudiwa huku watu 22 wakipoteza maisha na wengine 72 wakijeruhiwa katika mapigano ya mwishoni mwa juma baina ya makundi hasimu.


Takwimu zinaonyesha kuwa watu 124 ndiuo ambao wameuawa hadi sasa huku wengine zaidi ya mia tano wakijeruhiwa tangu kuanza kwa mapigano Julay 13 mjini Tripoli. Duru za kitabibu zimearifu kuwa huenda idadi ya waliopoteza maisha na kujeruhiwa ikawa kubwa zaidi kwani taarifa ya serikali haizingatii watu waliouawa na kujeruhiwa katika viunga vya jiji la Tripoli hususan katika mji wa Misrata.



SERIKALI YA KENYA YASISITIZA KUHUSU MPANGO WA KUWAPOKONYA ARDHI WANAOZIMILIKI KINYUME CHA SHERIA


Makamu wa rais wa Kenya, William Ruto ameendelea kusisitiza msimamo wa Serikali ya nchi hiyo kuhusu hatua waliyoitangaza juma moja lililopita ya kuwapokonya ardhi watu binafsi na makampuni yanayodaiwa kunyakua ardhi kwa nguvu kwenye mji wa Lamu pwania ya Kenya.

Kauli ya makamu wa rais, Ruto ameitoa akijibu hoja zinazotolewa na upinzani ambao unataka Serikali kuachana na mpango huo na kwamba utachukua hatua za kisheria kupinga uamuzi wa Serikali, msimamo ambao naibu wa rais Ruto anasema serikali yake haitorudi nyuma wala kutishika.

Makamu wa rais William Ruto anasema kuwa ni kitendo cha kustaajabisha na kilichopitwa na wakati kuona viongozi wa upinzani wanatumia muda mwingi kutoa vitisho dhidi ya Serikali na kuongeza kuwa vitisho hivi havisaidii.

Makamu wa rais Ruto, aanatoa kauli hii wakati ambapo hii leo tume ya ardhi nchini humo inatarajiwa kuanza kutekeleza agizo la rais Uhuru Kenyatta kuchukua ardhi inayokadiriwa kufikia hekari laki 5ambayo ilikuwa inamilikiwa kinyume cha sheria.

MKUTANO WA MAREKANI NA AFRIKA KUANZA LEO JIJI WASHINGTON


Rais wa Marekani, Barack Obama, hii leo anatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa kati yake na viongozi toka barani Afrika, mkutano uliolenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi yake na bara la Afrika.

Mkutano huu unafanyika wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo umasikini uliokithiri kwenye baadhi ya mataifa pamoja na janga la ugonjwa wa virusi vya Ebola ambao unatishia kusambaa hata kwenye mataifa ya Magharibi.

Rais Obama anatarajiwa kutumia mkutano huu kuwaeleza viongozi wa Afrika mkakati wa nchi yake katika kuimarisha biashara na nchi hizo, pamoja na namna itakavyoendelea kushirikiana na viongozi hao katika vita dhidi ya kuondoa umasiki na vitendo vya ugaidi.


Takariban viongozi kutoka nchi 50 ndio wanaohudhuria mkutno huo, ispokuwa pekee Jamhuri ya Afrika ya kati, Sudani, Eritrea na Zimbabwe ambazo hazikupewa mualiko, huku Liberia na Guinea zikiahirisha kutokana na kukabiliwa na gonjwa na Ebola.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...