|
Vijana wa Imbenerakure katika moja ya sherehe zao |
Miezi miwili
baada ya kuvuja kwa taarifa kutoka Umoja wa Mataifa kuhusu uwepo wa
shughuli za ugavi wa silaha kwa vijana wa chama tawala cha CNDD-FDD
nchini Burundi Imbonerakure, hatuwa iliopelekea kufukuzwa nchini humo
kwa mwanadiplomasia wa Umoja huo na ambayo imekuwa sababu ya kutiwa
nguvuni kwa mwanaharakati wa haki za binadamu na mtetezi wa haki za
wafungwa Pieere Claver Mbonimpa, mashrika ya kiraia nchini humo
yameomba uchunguzi ufanyike kuhusu taarifa hii.
Muungano wa
mashirika ya kiraia nchini humo umesaini waraka kwa raia wa Burundi
Pierre Nkurunziza na kwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na
Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kufanyika kwa uchunguzi kuhusu taarifa
hii.
|
Vital Nshimirimana mwenyekiti wa mashirika ya kiraia FORSC |
Mratibu wa
shughuli kwenye muungano wa mashirika ya kiraia Vital Nshimirimana
amesema lengo hasa ni kutaka kujuwa ukweli kuhusu taarifa hii kwani
serikali ya burundi haitaki kufanyika kwa uchunguzi ili kutowa mwanga
zaidi kuhusu taarifa za vijana wa chama tawala wanaopewa mafunzo ya
kijeshi katika ardhi ya Congo.
Lengo hasa
la waraka huu ni kuhakikisha zinakusanywa ma elfu ya sahihi kwa
kipindi cha majuma mawili kuishinikiza serikali ya burundi na jumuiya
ya kimataifa kuanzisha uchunguzi kuhusu taarifa hii ya kutatanisha.
|
Philippe Nzobonariba |
Upande
wake ya Burundi imetupilia mbali harakati hizo za masharika ya kiraia
nchini humo ya kupiga kampeni ili kukusanya saini kwa maelfu katika
wiki mbili zijazo, kuilazimisha kuanzisha mchakato wa kuchunguza
madai kwamba imegawa silaha kwa vijana wa chama tawala –
Imbonerakure.
Majibu
ya Serikali ya Burundi hayakuwa na kigugumizi wakati Msemaji wa
Serikali ya Burundi Philippe Nzobonariba ametuhumu mashrika ya kiraia
nchini humo kuendelea kuwa vibaraka wa vyama vya upinzani.