Serikali
ya Marekani imewataka raia wake wanaoeshi nchini Burundi
kuondoka mara moja nchini humo kufuatia kuendelea kuhatarishwa kwa
hali ya usalama nchini humo tangu pale lilipofeli jaribio la
mapinduzi mwezi Mei mwaka huu lililofuatiwa na machafuko na mzozo wa
kisiasa.
Katika
taarifa ya wizara ya mambo ya nje wa Marekani hapo jana imewataka
raia wa Marekani wasiokuwa na shughuli muhimu kuondoka nchini humo na
familia zao na kuwataka raia wote wa Marekani kutoelekea Burundi, na
wale waliopo nchini humo kuondoka haraka iwezekanavyo.
Zaidi
ya watu 90 wameuawa siku ya Ijumaa Juma lililopita baada ya kutokea
kwa mashambulizi ya kambi tatu za kijeshi nchini humo, ambapo taarifa
za jeshi la nchi hiyo ziliarugu kuuawa kwa waasi 79 na wanajeshi 8.
Jumamosi
asubuhi maiti kadhaa zilizshuhudiwa katika mitaa ilioendesha
maandamao ya kupinga muhula wa 3, ambapo wengi wa waliouwawa ni
vijana. Mashuhuda nchini humo wamevituhumu vikosi vya Usalama
kuwashikilia vijana waliokutana nao baada ya shambulio la kambi za
kijeshi na kuwauwa, ambapo maiti kadhaa zilionekana zikifungwa kamba
mikononi.
Kulingana
na taarifa ya pamoja ua mjumbe wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini
na kamishna wa ushirikiano wa kimataifa Neven Mimica wameomba ukweli
uwekwe wazi kuhusu mauaji haya yanayotokea katika karne hii.