Siku
moja baada ya tume ya taifa ya uchaguzi nchini Burundi kupendekeza
tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge na ule wa urais, ikulu ya
Bujumbura hii leo imethibitisha rasmi kuwa uchaguzi wa wabunge
utafanyika June 29 na ule wa urais utafanyika July 15 kama
ilivyopendekezwa na tume.
Kusogezwa
mbele kwa uchaguzi huu kumeenda sambamba na maazimio ya wakuu wa nchi
za Afrika Mashariki na kati ambao walitaka uchaguzi usogezwe mbele
ili kupisha kufanyika kwa mazungumzo kati ya upinzani na Serikali ili
kusaka muafaka kuhusu muhula watatu wa rais Pierre Nkurunziza.
Tangazo
hili la ikulu linatolewa ikiwa ni siku moja tu imepita toka msemaji
wa rais Nkurunziza atangaze kuwa suala la kuwania muhula wa tatu kwa
rais Nkurunziza ni suala ambalo halina mjadala.
Tangazo
hili la Serikali pia limetupilia mbali uwezekano mwingine wa
kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu nchini humo kinyume na tarehe
zilizotangazwa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire