Licha
ya upinzani na maandamano yanayoendelea kushuhudiwa nchini Burundi,
Serikali ya Bujumbura inasema kuwa suala la rais Pierre Nkurunziza
kuwania urais kwa muhula wa tatu, ni suala ambalo halina mjadala, na
kwamba kiongozi huyo hana nia ya kubadili uamuzi wake.
Akizungumza
kwenye kituo kimoja cha redio, msemaji wa Serikali Philippe
Nzobonariba, amesisitiza kuwa uamuzi wa rais Nkurunziza kuwania
uongozi kwa muhula wa tatu, ni uamuzi ambao hauna mjadala, kauli
inayozima kabisa madai ya upinzani ambao unataka rais Nkurunziza
kutowania tena urais.
Philippe
Nzobonariba, ameongeza kuwa mapendekezo yaliyotolewa na tume ya taifa
ya uchaguzi kutaka kusogeza mbele baadhi ya chaguzi nchini humo, ni
uamuzi wa mwisho na kwamba hata uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika
July 15 huenda ukasogezwa mbele.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire