Pages

mercredi 24 décembre 2014

MAHAKAMA YA KENYA YAKATAA KUSITISHA SHERIA KUHUSU USALAMA


mahakama kuu jijini nairobi hapo jana imetupilia mbali ombi la muunganbo wa upinzani nchini humo kutaka kutoa amri ya kusitisha utekelezwaji wa sheria tata zihusuzo usalama.

Muungano wa upinzani nchini Kenya Cord hapo jana ulikuwa umeitaka mahakama nchini humo kufuta sheria mpya iliodhinishwa na bunge hivi karibuni kuhusu usalama, sheria ambayo wakili wa upinzani James Orengo amesema ipo kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Mbali na kuwa kinyume na katiba ya nchi hiyo wakili huyo amesema imeidhinishwa katika mazingira tatanishi bungeni na kuitaka mahakama kusitisha utekelezwaji wa sheria hiyo kabla ya kutathminiwa upya.

Jaji mkuu wa mahakama Isaac Lenaola ametupilia mbali ombi hilo la upinzani na kudai kuwa umauzi wa kusitisha utelekezwaji wa sheria hiyo utakuwa kinyume cha sheria kutokana na upinzani kukosa sababu maalum za kuifanya mahakama kusitisha sheria hiyo.


jeudi 18 décembre 2014

BURUNDI, TUME HURU YA UCHAGUZI KULIKONI?

Tume ya Uchaguzi nchini Burundi CENI imekiri dhahiri shahiri kuwepo kwa kasoro zilizojitokeza wakati wa zoezi la kuorodhesha raia kwenye daftari la wapiga kura na kusisitIza kwamba ukiukwaji huo wa taratibu hautokani na uamuzi wa dhati wa Tume hiyo.

Mapema juma hili, vyama vya upinzani nchini humo vimeiomba tume hiyo kujiuzulu ambapo vyama 18 vimeituhumu Tume hiyo kuandika majina ya wapigakura hewa kusaidia chama tawala katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Vyama hivyo 18 vya upinzani nchini humo vinatishia kuendesha maandamano iwapo madai yao hayatopatiwa jawabu. Vyama hivyo vinaiomba tume ya uchaguzi Ceni pawepo na mazungumzo kuhusu matokeo ya zoezi la kuorodhesha raia wataopiga kura hapo mwakani na pia tume ya uchaguzi Ceni ijiuzulu kwa kuwa si huru.

Kumekuwa na hofu ya kutokea mvutano wa kisiasa nchini Burundi kutokana na hali hii ambayo tume ya Uchaguzi imeendelea kupuuzia madai ya wansiasa wa upinzani, jambo ambalo linaweza kukwamisha mchakato mzima wa uchaguzi kama ilivyoshuhudiwa katika chaguzi zilizopita.

Mbali na ukimya wa wa tume huru ambayo licha ya kukiri kuwepo na dosari imeendelea kusisitiza kwamba kasoro zilizojitokeza zinaweza kurekebishwa, rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza pia alitakiwa kuingilia kati kuhusu swala hili ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unashirikisha pande zote, ili baadae ataeangukia pua kwenye uchaguzi akose sababu.

Upinzani wao unaona kuwa kukaa kimya kwa viongozi wa chama tawala ni kutokana na jambo hili kukinufaisha.

Lakini pia Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, mashirika mbalimbali ya kimataifa yameendelea kukaa kimya kutokana na tuhuma hizi za uwepo wa udanganyifu katika zoezi hili la kuwaorodhesha wananchi katika dafatari la wapiga kura.

Kama kweli tume huru yenyewe inakiri uwepo wa kasoro nyingi tu katika zoezi hilo, kwanini madai ya upinzani yasifanyiwe kazi? Mwenyekiti wa tume hiyo CENI Pierre Claver Ndayicariye alisikika akisema kwamba chaguzi zilizopita kulikuwepo na dosari kama hizo, lakini zilirekebishwa, hivi hali ilivyokuwa kipindi hicho ndivyo ilivyo kwa sasa?

Wachambuzi wa siasa wanajiuliza wapo wapi watetezi wa Burundi? Wanasubiri moto uwake ili waje kuuzima wakati kuna uwezekano mkubwa wa kuuzima kabisa usiwake?

Kwa vyovyote vile hakuna ataefaidi iwapo vurugu zitatokea ikiwa chanzo itakuwa na swala hili ambalo baadhi wanalichukulia kuwa la kawaida wakati wengine walichukulia kuwa la msingi.

Tusubiri tuone.

UMOJA WA MATAIFA KUCHUNGUZA KUHUSU TUHUMA DHIDI JENERALI JEAN BOSCO KAZURA

Umoja wa Mataifa umeanza kufikiria na kujadili tuhuma zinazomkabili aliyekuwa Mkuu wa majeshi ya Umoja huo ya kulinda amani nchini Mali - MINUSMA- Jenerali Jean Bosco Kazura kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita nchini Rwanda.


Mwezi Desemba mwaka 2013, mwandishi wa habari wa Canada Judi Rever alimtuhumu jenerali Kazura kutekeleza vitendo vya wa uhalifu wa kivita nchini Rwanda mwaka 1994 akiwa afisa mwandamizi wa Rwanda Patriotic Army Rwanda cha rais Paul Kagame.


Tangu tuhuma hizo zitolewe mwaka uliopita, Umoja wa Mataifa umekaa kimya lakini ple Jenerali Kazura ajiuzulu ukimya huo umeanza kuvunjwa na tuhuma kujadiliwa kwenye Idara ya Oparesheni za Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa.

mercredi 17 décembre 2014

MBIVU NA MBICHI HAPO KESHO BUNGENI NCHINI KENYA

Wabunge nchini Kenya hapo kesho alhamisi wanatarajiwa kuyapigia kura mapendekezo mapya ya sheria kuhusu usalama, mapendekezo ambayo serikali ya nchi hiyo inasema yatasaidia kupambana na maswala ya Ugaidi.

Hata hivyo mapendekezo hayo yanapingwa vikali na upinzani ambao umesema unataka yabadilishwe la sivyo watapiga kura ya hapana.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na kuwazuia washukiwa wa Ugaidi kwa kipindi kirefu bila kupelekwa mahakamani, wanahabari kupata idhini ya polisi kabla ya kuchapisha picha au habari kuhusu Ugaidi.

Mbali na wabunge wa Upinzani wanahabari pia nchini humo wanapinga mapendekezo hayo na kutaka yabadilishwe.

Hivi karibuni rais wa nchi Uhuru Kenyatta alisikika akisikitishwa na mvutano wa wabunge kuhusu swala la Usalama, ambapo waheshimiwa hao walifikia hatuwa ya kuvutana mashati.

BAN KI MOON KUZURU NCHI ZA AFRIKA MAGHARIBI HIVI KARIBUNI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon anataraji kuzuru hivi karibuni katika nchi nne za ukanda wa Afrika Magharibi zilizo athiriwa na mlipuko wa Ebola. Ziara hii inakuja wakati nchi ya Sierra Leone ikiongeza muda wa kampeni ya nyumba kwa nyumba kuhusu Ebola.
Kulingana na duru za kidiplomasia kutoka Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon atatembelea nchini Liberia, Guinea, Sierra Leone na Mali katika tarehe mbayo haijatajwa.
Ebola ambayo ilianza kuzungumziwa kusini mwa Guinea mwezi Desemba mwaka jana, tayari imegharimu maisha ya watu 6.900 dhidi ya jumla ya watu watu 18.500 waliodaiwa kuambikizwa virusi ikiwa ni sawa na asilimia 99 nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea ikiwa ni takwimu za hivi karibuni za shirika la Afya duniani WHO.
Nchini Mali ambako watu saba wameripotiwa kiupoteza maisha kutokana na Ebola, hali hali bado ni tete licha ya kuondolewa kwa hali ya uchunguzi dhidi ya watu wanakisiwa kuwa karibu na wahanga wa Ebola kukutwa hawana virusi hivyo
hayo yanajiri wakati viongozi wa Sierra Leone wakitangaza kuongeza muda wa kampeni ya nyumba kwa nyumba juu ya kuhamasisha kuhusu virusi vya Ebola ambapo kampeni hiyo iliobatizwa "Western Area Surge" itaendelea hadi Desemba 31.


RAIS WA TCHAD AYATUHUMU MATAIFA YA MAGHARIBI KUZUA UGAIDI KWA KUMUUWA GADAFI NCHINI LIBYA

Baada ya mazungumzo ya siku mbili jijini Dakar, katika jukwa la kwanza la kimataifa kufanyika juu ya Amani na Usalama barani Afrika jukwa ambalo liliandaliwa kwa ushirikiano na diplomasia ya Ufaransa, jambo ambalo halijapokelewa vizuri na Umoja wa Afrika AU.

Licha ya wajumbe wote walioshiriki katika mkutano huo kuridhishwa na mazungumzo, swala la Ugaidi nchini Libya limeonekana kugusa hisia za viongozi wengi mkutanaoni na kuzua mjadala mkali kuhusu jukumu la majeshi ya kujihami ya nchi za magharibi Nato katika kuuangusha utawala wa hayati kanali Muamar Gadafi


Rais wa TChad Idriss Deby Itno amesisitiza kuwa Lengo kuu la majeshi ya Nato nchini Libya ilikuwa ni kutekeleza mauaji ya rais Gaddafi na si vinginevyo na kwa hiyo NATO pamoja na Umoja wa Mataifa vinatakiwa kuwajibika kurejesha amani nchini Libya. 

URUSI YASEMA TUNAUWEZO WAKUKIDHI MAHITAJI YETU

Waziri mkuu wa Urusi Dimitri Medvedev amesema kwamba Urusi inauwezo wa kutosha kutatua matatizo yake ya kifedha ilionayo kwa sasa yatokana na kuanguka kwa sarafu yake ya Ruble bila hata hivyo kudhoofisha kanuni za uchumi wa soko.

Medvedev amesisitiza kwamba nchi yake ina rasili mali za kifedha ambazo zinaweza kuisaidia serikali kufikia malengo yake ya kiuchumi na Pia ina bidhaa zinazo hitajika ili kuhakikisha mahitaji yanakwenda sambamba

Waziri mkuu huyo ameyasema hayo katika mkutano wa dharura kwenye runinga ya taifa na mawaziri wake kutoka katika sekta ya uchumi na wawakilishi ma wamakapuni yanayo safirisha bidhaa kwenda nje ya nchi hiyo na kutupilkia mbali kanuni iliozidi uhusuyo soko.

ANGALIA PICHA ZA WASANII WATAOSHIRIKI KATIKA TAMASHA LA IKOH EVENT BUJUMBURA

Hii sio ya kukosa kabisa,  moja miongoni mwa tamasha kubwa la mwisho wa mwaka jijini Bujumbura. Hakuna caption ndefu picha zenyewe zinajitosheleza.

















lundi 20 octobre 2014

WANANCBHI WA BENI HAWANA IMANI NA VIONGOZI WAO BAADA YA KUTOKEA MAUAJI

wananchi wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo DRC, hawanaimani na kauli za viongozi wa eneo hilo baada ya kutokea kwa mauaji ya raia wasiokuwa na hatia, chini ya mkono wa kundi la waasi wa Uganda wa ADF-Nalu.
Licha ya wito uliotolewa na mea wa jiji la Beni Nyoni Masumbuko kuwataka kusalia kuwa watulivu katika kipindi hiki jeshi la serikali likifuatilia kwa ukaribu zaidi swala la Usalama, wananchi wengi wameendelea kuutoroka mji huo.

Kundi la ADF-Nalu limeendelea kutekeleza mashambulizi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia yoyote licha ya jeshi la serikali kutangaza kuwa limewadhibiti kwa asilimia kubwa waasi hao.

Wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakihoji kuhusu uwezo wa kundi hilo kuingia hadi katika eneo ambalo linawakaazi wengi wakiwemo wanajeshi wa serikali na kutekeleza mauaji kwa kuwakata watu kwa mapanga na kufaulu kutoroka bila wasiwasi yoyote.

Hayo yanajiri wakati huu wafungwa katika jela la Butemba masharik wa DRCongo wakifaulu kutoroka, na kuzua mtafaruku mkubwa katika eneo hilo.

mardi 7 octobre 2014

KUNDI LILILO ASI CHAMA CHA FNL LAKIRI KUHUSIKA KATIKA SHAMBULIO LA JESHI LA BURUNDI


Kundi moja la waasi nchini Burundi, limejigamba hapo jana kuhusika katika shambulio dhidi ya kituo kimoja cha kijeshi nchini humo karibu na mpaka na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na kukiri kuwauwa wanajeshi sita katika shambulio hilo, idadi iliokanushwa na jeshi la taifa hilo.

Msejaji wa jeshi la Burundi kanali Gaspard Baratuza amefahamisha kwamba kulikuwa na makabiliano na kundi la wahuni, na kukanusha taarifa ya kupoteza wanajeshi, badala yake kuthibitisha kuwa wamemuua muasi mmoja katika shambulio hilo.

Kundi hilo la waasi linasadikiwa kuwa ni miongoni mwa wafuasi wa chama cha FNL walioasi na kuanzisha uasi. Kulingana na msemaji wa kundi hilo Felix Jean Ntahonguriye amethibitisha kwamba walishambulia kituo cha jeshi kilichopo katika tarafa ya Gihanga kwenye umbali wa kilometa zaidi ya Ishirini na jiji la Bujumbura na baadae kutokomea katika msitu wa Rukoko karibu na DRCongo.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kundi hilo limekuwa likijigamba kuhusika na mashambulizi kadhaa ambapo kulingana na msemaji wa kundi hilo wataendelea kutekeleza mashambulizi dhidi ya vituo vya jeshi la Burundi hadi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.


msemaji wa jeshi la Burundi Gaspard Baratuza amepuuzia kitisho hicho na kusema kwamba ni kundi la wahuni waliopoteza dira na haliwezi kupambana na jeshi la serikali.

HERVE LADSOUS KUHUDHIRIA SHEREHE ZA KUAGWA KWA MIILI YA WANAJESHI WA UN JIJINI BAMAKO


Herve Ladsous naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anaye husika na opersheni za kulinda amani yupo nchini Mali ambako atahudhuria sherehe za kuiaga miili ya wanajeshi tisa wa Nigeria waliouawa katika shambulio liliotokea siku ya Ijuma juma lililopita.

Miili ya wanajeshi hao tisa wa kulinda amani kutoka nchini Nigeria itawekwa nje kwenye makao makuu ya vikosi vya kulinda amani jijini Bamako ambako mawaziri Abdoulaye Diop, wa mambo ya ndani nchini Mali pamoja na waziri wa Ulinzi Meja Kanali Bah Ndaw wanatahudhiria

Upande wa Minsuma, mbali na Herve Ladsous atakuwepo pia Arnaud Acodjénou naibu kiongozi wa opersheni za Umoja wa Mataifa, ambao wamekuja kutowa heshima za mwishi kwa wanajeshi hao waliojitolea kwa ajili ya amani barani Afrika. Herve Ladsous atatumia fursa hiyo kukutana na rais wa Mali Ibrahima Bubakar keita.


Herve Ladsous atajadili pia kuhusu swala la wanajeshi wa kulinda amani kutoka nchini Tchad ambao wanatishio kurejea nyumbani baada ya kupoteza mara kadhaa wanajeshi wake kutokana na bomu za kutegwa ardhini zilizo tengwa na wanamgambo.

WAZIRI WA ULINZI WA ZAMANI AIKOSOA SERA YA OBAMA KUOPAMBANA NA ISLAMIC STATE


Waziri wa zamani wa ulinzi wa serikali ya Marekani Leon Paneta na kiongozi wa zamani wa idara ya ujasusi, ambaye kitabu chake Worthy Fights kinazinduliwa hii leo, ameikosoa sera ya rais Obama kupambana na Ugaidi nchini Iraq na Syria, na kuonya kwamba kwa hali ilivyo vita hivyo vinaweza kudumu miaka 30.


wakati vita dhidi ya kundi la IS ikipamba moto, huku wanajihadi wa hao wakiendelea kumudu kwenye uwanja wa mapambano dhidi ya mashambulizi ya majeshi ya muungano, waziir wa ulinzi wa zamani amejitokeza na kuvunja ukimya kwa kutowa kauli ambayo imeighadhabisha Ikulu ya Marekani ya White House.

lundi 6 octobre 2014

MPIGA PICHA RAIA WA MAREKANI AREJESHWA NYUMBANI BAADA YA KUAMBUKIWA NA EBOLA LIBERIA


Mpiga picha raia wa marekani aliepata mambukizi ya virus vya Ebola nchini Liberia amesafirishwa kuondoka jijini Monrovia, duru za mashirika ya kibinadamu zimearifu.

Ashoka Mukpo mwenye umri wa miaka 33 mpiga picha na ambaye aliajiriwa hivi karibuni na kituo cha Marekani cha NBC aliwekwa katika hali ya hatari tangu jumatano juma lililopita katika kituo cha shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka.


Mwenyekiti wa kituo cha NBC Deborah Turness alifahamisha tangu siku ya Ijumaa iliopita kwamba mpiga picha huyo atasafirishwa hadi kwenye kituo kingine kwa ajili ya matibabu zaidi, huku wengine ambao hawaonyeshi dalili zozote za virusi vya Ebola watarejeshwa nyumbani na kuwekwa kqenye hali ya hatari kwa kipindi cha siku 21 kama inavtogizwa.

KUNDI LA MUJAO LAJIGAMBA KUHUSIKA KATIKA SHMBULIO LA VIKOSI VYA UN


Mpiganaji mmoja wa kijihadi wa kundi la Mujao, moja miongoni mwa makundi yalio kalia eneo la kaskazini mwa Mali amejigamba kuhusika na shambulio la kujitowa muhanga dhidi ya Kikosi cha Umoja wa mataifa nchini Humo.

Shambulio la siku ya Ijumaa dhidi ya kikosi cha Umoja wa Mataifa cha majeshi kutoka nchini nigeria lilisababisha vifo vya watu 9.

Uongozi wa kikosi cha Kulinda amani cha Umoja wa Mataifa Minusma, umesema hili ni shambulio kubwa kuwahi kutokea tangu kutumwa kwa majeshi ya Umoja wa Mataifa tangu kutumwa kwake Julay 2013.


AL SHABAB WAPOTEZA NGOME YAO MUHIMU


Askari wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) na jeshi la Somalia wamefanikiwa siku ya Jumapili kuuteka mji wa Barawe, ngome ya mwisho ya wanamgambo wa Al-Shebab na bandari kuu ambayo ilikuwa bado iko mikononi mwao.


Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa hatua hii ni pigo kwa wanamgambo wa Al-Shabab ambao walikuwa wanatumia bandari hii kupitisha chakula, kuuza mkaa pamoja na kupokea wapiganaji wake wa kigeni wanaoingia nchini humo.


Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa hatua hii ni pigo kwa wanamgambo wa Al-Shabab ambao walikuwa wanatumia bandari hii kupitisha chakula, kuuza mkaa pamoja na kupokea wapiganaji wake wa kigeni wanaoingia nchini humo.

mardi 23 septembre 2014

WATU WASIOJULIKANA WAJARIBU KUIBA MAITI ZILIZO OKOTWA KATIKA MTO RWERU


Wakati kukiwa na mswali chiungu nzima kuhusu maiti zilizo okotwa katika mto Rweru kwenye eneo la mpaka wa burundi na Rwanda, kundi la watu waliokuwa kwenye mitumbwi yenye kutumia injini, walivuka maji na kujaribu kuiba miili ya watu waliozikwa upande wa Burundi majuma matatu yaliopita.

Tukio hili limekuja kuchochea moto zaidi wakati huu burundi na Rwanda zimekuwa zikitupiana lawama kila mmooja akimtuhumu mwenzie kuhusika.

Watu hao waliojaribu kuiba miili hiyo walishindwa kutekeleza azma yao baada ya mlinzi wa mitiumbai upande wa burundi kuona mwanga wa Tochi na haitimae kuanza kupiga kelele na hatimae watu hao wakakimbia huku wakiacha vipao na mifuko ambayo viongozi wa serikali ya Burundi wanasema mifuko hiyo ingeliwasaidia kuweka miili ya watu hao iwapo wangelifaulu operesheni hiyo chafu.

Kutokana na tukio hilo Rwanda imeanza kukodoleaa macho licha ya hapo awali kukanusha kwamba watu hao hawakutoka nchini Rwanda, wakati huu shinikizo limeongezeka kuzitaka pande mbili yaani Birindi na Rwanda kuanzisha uchunguzi wa haraka kubaini watu hao ni kutoka Rwanda au Burundi.


vendredi 19 septembre 2014

POLISI YA TANZANIA YAWADHIBITI WAFUASI WA CHADEMA WAKATI MWEMNYEKITI WAKE AKIRIPORI MAKAO MAKUU YA POLISI


Polisi nchini Tanzania hapo jana imekabiliana na wafuasi wa mpinzani wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, baada ya mwenyekiti wa chama hicho Freeeman Mbowe kuwasili katika ofisi za makao makuu ya polisi kutokana na tuhuma zinazo mkabili za uchochezi kuhusu kauli yake ya kuitisha maandamano nchi nzima.

Polisi nchini Tanzania ililazimika kufunga barabara inayoelekea kwenye ofisi za makao makuu ya polisi kutokana na wafuasi wa Chadema waliokuwa wamefurika kwa wingi katika eneo hilo, jambo ambalo linadaiwa kuwa kinyume.

Hata hivyo waandishi wa habari ambao walikuwa wamejielekeza katika eneo hilo kwa ajili ya kuripoti habari hawakurahisishiwa na polisi na kujikuta polisi ikikabiliana nao kuwafurusha katika eneo hilo, huku wengine wakidai kunyanyaswa na Polisi.




jeudi 18 septembre 2014

WIKI YA KUMBUKUMBU YA SHAMBULIO LA WESTGATE NCHINI KENYA


Manusura na mashuhuda wa shambulio la kigaidi katika eneo la kibiashara la Westgate nchini Kenya wanaendelea kutowa ushuhuda kwa kile walichokiona wakati wa shambulio hilo, wakati huu Kenya ikifanya wiki ya kumbukumbu ya mashambulizi hayo.

Eneo hilo la kibiashara ambalo lilikuwa muhimu katika uchumi wa Kenya, lilishambuliwa mwaka mmoja uliopita na kundi la watu wenye silaha na kuwauawa watu 67 kulingana na duru za serikali, tukio ambalo lilidaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa Al Shabab baada ya kujigamba kwamba wanalipiza kisase kutokana na vikosi vya Kenya kufanya mashambulizi katika ngome zao nchini Somalia.

Inahofiwa huenda watu zaidi 67 walipoteza maisha katika tukio hilo mbaya kuwahi kutokea nchini Kenya.

Hayo yanajiri wakati huu Polisi nchini Kenya ikiimarisha Usalama katika maeneo mbalimbali huhu kukiwa na minong'ono miongoni mwa wananchi kuhusu mwenendo wa polisi nchini humo kwa raia.

Msemaji wa Polisi Masood Mwinyi anaona kuwa ushirikiano wa polisi na raia wa Kawaida ni muhimu katika kupambana na wahalifu.

KIONGOZI WA BARAZA LA SENETI NCHINI RWANDA AJIUZULU


Kiongozi wa baraza la Senete nchini Rwanda ametangaza kujiuzulu nafasi yake juma hili kwa kile alichodai ni sababu binafsi lakini vyombo vya habari nchini humo vimedai ni kwasababu ya wabunge wenzake kuitisha kura ya kuwa na imani nae.

Jean-Damascene Ntawukuliryayo alikuwa akishikilia wadhifa huo toka mwaka 2011 ambapo kujiuzulu kwake kumeelezwa kunatokana na hofu ya kisiasa iliyotanda nchini Rwanda wakati huu baadhi ya wapinzani wakikamatwa.
Jean-Damascene anatoka chama cha pili kikubwa cha upinzani cha The Social Democratic PSD ambacho kinashirikiana na serikali ya rais Paul Kagame.

Baadhi ya wabunge wa Seneti walihoji utendaji kazi wa Jean-Damascene na kutaka kupigw akura ya kutokuwa na imani nae.

UPINZANI NCHINI LIBYA WAKATAA KULITAMBUA BARAZA LA MAWAZIRI


Abdullah al-Thani
Waziri mkuu wa Libya anayetambiliwa na Jumuiya ya Kimataifa hapo jana amewasilisha baraza lake la mawaziri kwa bunge la nchi hiyo, wakati huu hofu ya kiusalama ikitanda baada upinzani kukataa kulitambua baraza hilo.

Utawala wa Libya chini ya waziri mkuu, Abdullah al-Thani pamoja na bunge la kitaifa lilihamia kwa muda mjini Tobruk mwezi August mwaka huu kwa sababu za kiusalama baada ya maeneo mengi ya jiji la Libya kushikiliwa na wapiganaji wa kiislamu.

Haya yanajiri wakati huu ambapo wanadiplomasia wanakutana mjini Madrid Uhispania kujadili hali ya usalama nchini Libya pamoja na kusaka suluhu ya mzozo wa kisiasa kwenye taifa hilo.


Makundi ya wapiganaji nchini humo hayakutuma wawakilishi wao kwenye mkutano huo unaohudhuriwa na nchi 16, ikiwemo Umoja wa mataifa na umoja wa nchi za kiarabu.

mardi 16 septembre 2014

MAREKANI YATEKELEZA MASHAMBULIZI KARIBU NA MJI MKUU WA IRAQ BAGDAD

Marekani imeshambulia kwa mara ya kwanza ngome za kundi la IS zilizo karibu karibu na mji mkuu Bagdad nchini Iraq. Duru za kuaminika zimearifu kuwa mashambulizi 160 tayari yametekelezwa katika eneo la kusini magharibi mwa Mji huo.

Kulingana na taarifa ya uongozi wa jeshi la Marekani katika ukanda mashariki ya kati Mashambulizi hayo yamelenga ngome za kundi la Islamic State katika eneo la kaskazini magharibi na yalilenga kulisaidia jeshi la Iraq katika mapambano dhidi ya wanamgambo hao.
Mashambulizi mengine ya anga yametekelezwa pia katika eneo la kaskazini karibu na mji wa Sinjar na kuharibu magari sita ya kijeshi ya kundi la IS.

Tangu Agosti 8 mwaka huu jeshi la Marekani linaendesha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa kundi la Islamic State ambao wameendelea kuwa tishio kwa usalama wa ukanda wa mashariki ya kati na ambo wamekalia maeneo kadhaa ya Iraq na Syria.

Rais Obama alitangaza hibi karibuni kuwa tayari kutekeleza mashambulizi dhidi ya ngome za IS nchini Syria huku akitupilia mbali hatuwa yoyote ya ushirikiano wa Marekani na serikali ya Damascus ambayo amesema imepoteza uhalali katika kulipiga vita kundi hilo. Hadi leo hakuna shambulizi lolote lililotekelezwa na Marekani dhidi ya kundi hilo nchini Syria.

Hayo yanajiri wakati jumuiya ya kimataifa katika kikao kilichofanyika jijini Paris nchini Ufaransa ikikubaliana na mpango wa Marekani kuungana katika kuisaidia Irak kwa njia zote zikiwemo za kijeshi katika harakati zake za kupambana na wanajihadi wa kundi la Islamic State bila hata hivyo kutaja hatuwa zilizochukuliwa dhidi ya kundi hilo.

RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA AZITUHUMU NCHI ZA MAGHARIBI KUSUASUA KUHUSU JANGA LA EBOLA


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezituhum nchi za magharibi kwa kushindwa kuchukuwa hatuwa za haraka kukomesha janga la Ebola na badala yake zina suasua katika kuchukua mikakati madhubuti ya kulipiga vita janga hili.
Rais Kenyatta ameyasema hayo kutokana na kile kinachoendelea katika nchi za ukanda wa Afrika magharibi zinazo kabiliwa na maradhi hayo, na kudai kuwa iwapo maradhi hayo yangeliripotiwa barani Ulaya au Marekani hatuwa madhubuti zingechukuliwa.
Rais Kenyatta amesema iwe kwenye upande wa kupamabana na maradhi hayo ya Ebola, au vita dhidhi ya Ugaidi, ushirikiano wa nchi za Afrika unahitajika kuweka fuko la pamoja kwa ajili ya kukabiliana na hali za dharura zinazo jitokeza barani Afrika na hapo ndipo Afrika itakuwa tayari kupata suluhu kwa tatizo la Afrika na sio kusubiri nchi za magharibi.
Uhuru Kenyatta aliyasema hayo wakati wa ghafla maalum ya kukabidhi tuzo ya kimataifa ya UNESCO mjini Malabo nchini Guinea Eqweta.
Viongozi wa Afrika walioshiriki katika ghafla hiyo walikutana kwa dharura kujadiliana kuhusu ushirikiano juu ya kutafuta uwezo wa kifedha katika kupambana na virus vya Ebola barani Afrika.
Janga la Ebola linalilikumba eneo la ukanda wa Afrika Magharibi tayari limegharimu maisha ya watu 2400. nchi ziliguswa sana ni pamoja na Sierra Leone, Guinea na Liberia. Janga hili limeripotiwa pia nchini Nigeria, Guinea, Senegal na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Tangu kipindi kadhaa serikali ya Kenya ilisitisha safari zake katika nchi za ukanda wa Afrika Magharibi.
Mbali na hayo, Kenya pia ilizuia habiria kutoka katika nchi zinazo kabiliwa na maradhi hayo kuingia nchini Kenya.

RADIO ZA MASHIRIKA YA KIRAIA NCHINI BURUNDI KUSUSIA MKUTANO WA WASEMAJI WA WIZARA ZA SERIKALI

Mkurugenzi mkuu wa radio Bonesha FM Patrick Nduwimana

Radio za mashirika ya kiraia nchini Burundi, ikiwa ni pamoja na Radio Bonesha FM, Radio ya Umma RPA, Radio Isanganiro, Radio Rennaissence FM NA Gazeti la Iwacu zimebaini maskitiko yake baada ya hatuwa ya mahakama kuu nchini Burundi kuamuwa kusalia jela kwa mwanaharakati mtetezi wa haki za binadamu Pierre Claver Mbonimpa.
Mahakama hiyo imechukuwa uamuzi huo licha ya hali ya afya kuwa mbaya, ambapo ma daktari wamethibitisha. Mahakama hiyo imeendelea kuziba maskiao kutokana na wito wa kimataifa na kitaifa wa kuitaka mahakama hiyo  kumuacha huru kwa dhamana kwa mujibu wa sheria za kimataifa za haki ya binadamu.
Kutokana na hali hiyo, Radio Bonesha FM, Radio ya Umma RPA, Radio Isanganiro, Radio Rennaissence FM NA Gazeti la Iwacu zimetangaza kuwa zitasusia mkutano wa waemaji wa wizara mbalimbali nchini humo na vyombo vya habari unaotarajiwa kufanyika Septemba 19 mwaka 2014.

lundi 15 septembre 2014

ALIYEKUWA MKURUGENZI WA HIFADHI YA JAMII NCHINI RWANDA AKAMATWA



Polisi nchini Rwanda imefahamisha kumkamata aliyekuwa mkurugenzi wa hifadhi ya jamii Angelique Kantengwa ambaye aliachiswa kazi mwanzoni mwa mwaka huu. Polisi inamtuhumu kosa la matumizi mabaya ya pesa za serikali.

Akizungungumza mbele ya bunge siku ya ijumaa juma lililopita, rais wa Rwanda Paul Kagame amesema inashangaza kuona wezi wa pesa za walipa kodi wanapotakiwa kuweka bayana matumizi ya pesa za serikali wanadai kuwa wananynayaswa kisiasa. Kagame amevitaka vyombo vya sheria kuwahukumu na pesa walisopora zirejeshwe. Hata hivyo rais Kagame hakutaja jina la mkurugernzi wa zamani wa kifahdi ya jamii.

Angélique Kantengwa ambaye kwa sehemu kubwa amekuwa akifany akazi katika banki na taasisi za kifedha za uma. Duru kutoka jijin Kigali zimearifu kuwa, Kabla ya kukamatwa kwake hakuna aliyefikiria kwamba anaweza kuhususishwa na kashfa hiyo. Polisi nchini Rwanda inasema inaendelea na uchunguzi huku akisalia korokoroni.

Mshauri wa zamani wa maswala ya uchumi wa rais Kagame, David Himbara aliekimbilia uhamishoni, anakituhumu chama tawala cha RPF ubadhirifu wa pesa za pensheni ya wanyarwanda. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kiongozi huyo wa zmanai amekuwa akiikososa serikali ya raia Kagame kupitia mitandano ya kijamii kuhusika katika ubadhirifu wa fedha za hifadhi ya jamii na benki kuu ya Rwanda.

Kanali Tom Byabagamba na jenerali mstaafu Frank Rusagara ambao mmoja ni shemeji na mwingine ni kaka wa David Himabara wote walikamatwa wiki kadhaa zilizopita kwa tuhuma za kuchochea vurugu. Rwanda limekuwa taifa linalo sifika sana kutokanana na usimamizi wake mzuri wa fedha, jambo linalofanya wafadhili na wawekezaji kuwa na iamani sana na serikali.

WASI WASI BADO INAENDELEA KUHUSU UKWELI JUU YA MSHUKIWA WA MAUAJI YA WATAWA WATATU WATATU NCHINI BURUNDI


Jumapili Septemba 7, watawa watatu wenye asili ya italia waliuawa nchini Burundi wakiwa katika makaazi yao yaliopo kwenye kaskazini mashariki mwa mji mkuu Bujumbura. Leo hii kumekuwa na maswali mengi kuhusumauaji hayo hususan kuhusu mshukiwa aliyekmatwa na polisi na ambaye anaelezwa kuwa mpugnufu wa akili.

Polisi nchini Burundi ilifaulu kumkamata mshukiwa wa mauaji ya watawa hao watatu raia wa italia, ikiwa ni siku mbili baada ya kutokea kwa mauaji hayo. Lakini siku mbili baada ya kutiwa ngubuni kwa mshukiwa huyo, moja miongoni mwa vituo
vya radio jijini Bujumbura lilitowa taarifa za mashuhuda wakidai kwamba mtuhumiwa huyo ni mpungufu wa akili.

Kulingana na taarifa ya RFI, polisi jijini Bujumbura ilijaribu kumfanyia vipimo vya akili mshukiwa huyo baada ya taarifa hizo. Daktati wa kituo kinachopima akili aliomba vipimo hivyo vifanyike bila uwepo wa polisi, jambo ambalo polisi ilipinga katu katu na kuamuwa kuondoka naye.

Jambo hili limezua mkanganyiko jijini Bujumbura ambapo wananchi wa jiji hilo wamekuwa hawaamini kwamba mtu aliye wasilishwa kwenye runinga kuwa ndiye aliyepanga mauaji. Polisi imeendelea kusisitiza kuwa inamshikilia mshukiwa ma mauaji na atawalishwa mbele ya vyombo vya sheria ambavyo vitatowa taarifa ya kwamba mshukiwa huyo ni mpungufu wa akili au la.

MAHAKAMA NCHINI BURUNDIA KUAMUWA KUHUSU KUACHIWA HURU KWA DHAMAN AU LA KWA PIERRE CLAVER MBONIMPA


Mahakama nchini Burundi inatarajiwa hii leo kuamua ikiwa mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu Pierre Claver Mbonimpa ataachiwa huru kwa dhamana hii leo au la, kama ilivyoombwa na mawakili wake juma lililopita.

Mtetezi huyo wa haki za binadamu nchini Burundi alikamatwa na kufungwa jela mwezi Juni baada ya kutowa taarifa za uwepo wa vijana wa chama tawala nchini humo wa Imbonerakure kupiga kambi mashariki mwa DRCongo wakipewa mafunzo ya kijeshi, jambo ambalo amekuwa akisisitiza kuwa na ushahidi wa kutosha.
  
Pierre Claver Mbonimpa ana umri wa miaka 66 na anasumbuliwa na magonjwa ya Sukari na shinikizo la damu ambapo hivi sasa yupo katika hospitali moja mjini Bujumbura kupatiwa matibabu baada ya kuzidiwa mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

UMOJA WA MATAIFA WACHUKUWA JUKUMU RASMI HII LEO LA ULIZNI WA AMANI NCHINI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI


Umoja wa Mataifa unachukuwa rasmi uongozi wa kikosi cha kulinda amani nchini jamhuri ya Afrika ya kati Misca, jukumu lililokuwa chini ya uongozi wa vikosi vya Muungano wa nchi za Afrika ya kati Misca.

Sherehe maalum zimepangqwa kufanyika hii leo katika uwanja wa ndege wa jijini Bangui ambapo viongozi wa Misca watakabidhi uongozi kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa Misca kitachoendelea na jukumu la kulinda amani ambacho hadi sasa kinasaidiwa na kikosi cha ufaransa katika operesheni Sangaris na kikosi cha Umoja wa Ulaya nchini jamhuri ya afrika ya kati Eufor.


Wanajeshi kutoka Pakistan, Bangladesh na Morocco watajiunga na kikosi hicho, kitachofikisha jumla ya askari 7,500 ambao kwa kushirikiana na askari hao wa Afrika watakuwa na kibarua cha kurejesha usalama nchini humo chini ya uongozi wa Jenerali Babacar Gaye.

vendredi 22 août 2014

NAVI PILLAYALAUMU UDHAIFU ULIOPO KWENYE BARWZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA


Kamishna wa haki za binadamu kwenye Umoja wa mataifa ambaye anaachia ngazi, amelaumu jana kuhusu udhaifu wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa kushindwa kkumaliza mgogoro katika maeneo kadhaa dunianikwa sababu ya kiwango cha maambukizi ya maslahi ya taifa.

Navy Pillay amesema Wanachama wa baraza la Usalama wanashindwa mara kadhaa kuchukuwa maamuzi na kuwawajibisha viongozi wanaohusika na mizozo, ameendelea kusisitiza hivo kiongozi huyo wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa aliyejiuzulu na ambaye anataraji kuondoka rasmi kwenye uongozi huu katika siku za hivi karibuni.

Navy Pilay amesema anafkiri kwamba maamuzi sahihi ya baraza la usalama ndio yanayoweza kuokoa maisha ya mamia ya watu duniani wanaokabiliwa na hali duni wakati huu kutokana na mizozo inayo wakumba katika nchi zao.

Kiongozi huyo raia wa Afrika Kusini amesema kuwa matumizi ya kura ya turufu kwenye barqaza la Usalama la umoja wa mataifa limekuwa kikwazo kikubwa kwa mataifa mengine kuchukuwa maamuzi.


MAREKANI YASISITIZA AZMA YAKE YA KULISHAMBULIA KUNDI LA ISLAMIC STATE



Serikali ya marekani imeendelea kushikilia uamuzi wake wa kuchukua hatua dhidi ya wanajihadi wa Dola laa Kiislamu linalo onekana kuwa hatari, na kuahidi kuendeleza mashambulizi nchini humo licha ya tishio la kundi hilo lawatu wenye msimamo mkali kutishia kumchinja mateka mwengine wa marekani baada ya kutekeleza kitendo hicho kwa muandishbi wa habari James Foley.

Mjini Geneva, Kamishna wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, Navi Pillay amelaumu kuhusu hatuwa ya kupooza kwa kushughuli za Jumuiya ya kimataifa, jambo ambalo linalo chochea kuibuka kwa wauaji, waharibifu na watesaji katika nchi za Syria na Iraq.


wakati Jumuiya ya kimataifa ikizuia kutowa msaada wa kupatikana kwa suluhu katika mzozo unaondelea nchini Syria, washington na baadhi ya washirika wake wamewapa silaha waasi wa kikurdi ili kupambana na kundi la dola la kiislam na kuandaa mkakati wa kudumu ili kujaribu kulitokomeza kabisa kundi hili lililoitwa kama Kansa ya dunia na rais Barack Obama.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...