Abdullah al-Thani |
Waziri
mkuu wa Libya anayetambiliwa na Jumuiya ya Kimataifa hapo jana
amewasilisha baraza lake la mawaziri kwa bunge la nchi hiyo, wakati
huu hofu ya kiusalama ikitanda baada upinzani kukataa kulitambua
baraza hilo.
Utawala
wa Libya chini ya waziri mkuu, Abdullah al-Thani pamoja na bunge la
kitaifa lilihamia kwa muda mjini Tobruk mwezi August mwaka huu kwa
sababu za kiusalama baada ya maeneo mengi ya jiji la Libya
kushikiliwa na wapiganaji wa kiislamu.
Haya
yanajiri wakati huu ambapo wanadiplomasia wanakutana mjini Madrid
Uhispania kujadili hali ya usalama nchini Libya pamoja na kusaka
suluhu ya mzozo wa kisiasa kwenye taifa hilo.
Makundi
ya wapiganaji nchini humo hayakutuma wawakilishi wao kwenye mkutano
huo unaohudhuriwa na nchi 16, ikiwemo Umoja wa mataifa na umoja wa
nchi za kiarabu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire