Jumapili
Septemba 7, watawa watatu wenye asili ya italia waliuawa nchini
Burundi wakiwa katika makaazi yao yaliopo kwenye kaskazini mashariki
mwa mji mkuu Bujumbura. Leo hii kumekuwa na maswali mengi
kuhusumauaji hayo hususan kuhusu mshukiwa aliyekmatwa na polisi na
ambaye anaelezwa kuwa mpugnufu wa akili.
Polisi
nchini Burundi ilifaulu kumkamata mshukiwa wa mauaji ya watawa hao
watatu raia wa italia, ikiwa ni siku mbili baada ya kutokea kwa
mauaji hayo. Lakini siku mbili baada ya kutiwa ngubuni kwa mshukiwa
huyo, moja miongoni mwa vituo
vya radio
jijini Bujumbura lilitowa taarifa za mashuhuda wakidai kwamba
mtuhumiwa huyo ni mpungufu wa akili.
Kulingana na
taarifa ya RFI, polisi jijini Bujumbura ilijaribu kumfanyia vipimo
vya akili mshukiwa huyo baada ya taarifa hizo. Daktati wa kituo
kinachopima akili aliomba vipimo hivyo vifanyike bila uwepo wa
polisi, jambo ambalo polisi ilipinga katu katu na kuamuwa kuondoka
naye.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire