Umoja
wa Mataifa unachukuwa rasmi uongozi wa kikosi cha kulinda amani
nchini jamhuri ya Afrika ya kati Misca, jukumu lililokuwa chini ya
uongozi wa vikosi vya Muungano wa nchi za Afrika ya kati Misca.
Sherehe
maalum zimepangqwa kufanyika hii leo katika uwanja wa ndege wa jijini
Bangui ambapo viongozi wa Misca watakabidhi uongozi kwa kikosi cha
Umoja wa Mataifa Misca kitachoendelea na jukumu la kulinda amani
ambacho hadi sasa kinasaidiwa na kikosi cha ufaransa katika
operesheni Sangaris na kikosi cha Umoja wa Ulaya nchini jamhuri ya
afrika ya kati Eufor.
Wanajeshi
kutoka Pakistan, Bangladesh na Morocco watajiunga na kikosi hicho,
kitachofikisha jumla ya askari 7,500 ambao kwa kushirikiana na askari
hao wa Afrika watakuwa na kibarua cha kurejesha usalama nchini humo
chini ya uongozi wa Jenerali Babacar Gaye.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire