Mahakama
nchini Burundi inatarajiwa hii leo kuamua ikiwa mwanaharakati wa
kutetea haki za binadamu Pierre Claver Mbonimpa ataachiwa huru kwa
dhamana hii leo au la, kama ilivyoombwa na mawakili wake juma
lililopita.
Mtetezi
huyo wa haki za binadamu nchini Burundi alikamatwa na kufungwa jela
mwezi Juni baada ya kutowa taarifa za uwepo wa vijana wa chama tawala nchini humo wa Imbonerakure kupiga kambi mashariki mwa DRCongo wakipewa mafunzo ya kijeshi, jambo ambalo amekuwa akisisitiza kuwa na ushahidi wa kutosha.
Pierre
Claver Mbonimpa ana umri wa miaka 66 na anasumbuliwa na magonjwa ya
Sukari na shinikizo la damu ambapo hivi sasa yupo katika
hospitali moja mjini Bujumbura kupatiwa matibabu baada ya kuzidiwa
mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire