Polisi
nchini Rwanda imefahamisha kumkamata aliyekuwa mkurugenzi wa hifadhi
ya jamii Angelique Kantengwa ambaye aliachiswa kazi mwanzoni mwa
mwaka huu. Polisi inamtuhumu kosa la matumizi mabaya ya pesa za
serikali.
Akizungungumza
mbele ya bunge siku ya ijumaa juma lililopita, rais wa Rwanda Paul
Kagame amesema inashangaza kuona wezi wa pesa za walipa kodi
wanapotakiwa kuweka bayana matumizi ya pesa za serikali wanadai kuwa
wananynayaswa kisiasa. Kagame amevitaka vyombo vya sheria kuwahukumu
na pesa walisopora zirejeshwe. Hata hivyo rais Kagame hakutaja jina
la mkurugernzi wa zamani wa kifahdi ya jamii.
Angélique
Kantengwa ambaye kwa sehemu kubwa amekuwa akifany akazi katika banki
na taasisi za kifedha za uma. Duru kutoka jijin Kigali zimearifu
kuwa, Kabla ya kukamatwa kwake hakuna aliyefikiria kwamba anaweza
kuhususishwa na kashfa hiyo. Polisi nchini Rwanda inasema inaendelea
na uchunguzi huku akisalia korokoroni.
Mshauri wa
zamani wa maswala ya uchumi wa rais Kagame, David Himbara
aliekimbilia uhamishoni, anakituhumu chama tawala cha RPF ubadhirifu
wa pesa za pensheni ya wanyarwanda. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu,
kiongozi huyo wa zmanai amekuwa akiikososa serikali ya raia Kagame
kupitia mitandano ya kijamii kuhusika katika ubadhirifu wa fedha za
hifadhi ya jamii na benki kuu ya Rwanda.
Kanali Tom
Byabagamba na jenerali mstaafu Frank Rusagara ambao mmoja ni shemeji
na mwingine ni kaka wa David Himabara wote walikamatwa wiki kadhaa
zilizopita kwa tuhuma za kuchochea vurugu. Rwanda limekuwa taifa
linalo sifika sana kutokanana na usimamizi wake mzuri wa fedha, jambo
linalofanya wafadhili na wawekezaji kuwa na iamani sana na serikali.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire