Mkurugenzi mkuu wa radio Bonesha FM Patrick Nduwimana |
Radio za
mashirika ya kiraia nchini Burundi, ikiwa ni pamoja na Radio Bonesha
FM, Radio ya Umma RPA, Radio Isanganiro, Radio Rennaissence FM NA
Gazeti la Iwacu zimebaini maskitiko yake baada ya hatuwa ya mahakama
kuu nchini Burundi kuamuwa kusalia jela kwa mwanaharakati mtetezi wa
haki za binadamu Pierre Claver Mbonimpa.
Mahakama hiyo imechukuwa uamuzi huo licha ya hali ya afya kuwa
mbaya, ambapo ma daktari wamethibitisha. Mahakama hiyo imeendelea kuziba maskiao kutokana na wito wa kimataifa
na kitaifa wa kuitaka mahakama hiyo kumuacha huru kwa dhamana kwa mujibu wa
sheria za kimataifa za haki ya binadamu.
Kutokana
na hali hiyo, Radio Bonesha FM, Radio ya Umma RPA, Radio Isanganiro,
Radio Rennaissence FM NA Gazeti la Iwacu zimetangaza kuwa zitasusia
mkutano wa waemaji wa wizara mbalimbali nchini humo na vyombo vya
habari unaotarajiwa kufanyika Septemba 19 mwaka 2014.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire