Pages

mardi 23 septembre 2014

WATU WASIOJULIKANA WAJARIBU KUIBA MAITI ZILIZO OKOTWA KATIKA MTO RWERU


Wakati kukiwa na mswali chiungu nzima kuhusu maiti zilizo okotwa katika mto Rweru kwenye eneo la mpaka wa burundi na Rwanda, kundi la watu waliokuwa kwenye mitumbwi yenye kutumia injini, walivuka maji na kujaribu kuiba miili ya watu waliozikwa upande wa Burundi majuma matatu yaliopita.

Tukio hili limekuja kuchochea moto zaidi wakati huu burundi na Rwanda zimekuwa zikitupiana lawama kila mmooja akimtuhumu mwenzie kuhusika.

Watu hao waliojaribu kuiba miili hiyo walishindwa kutekeleza azma yao baada ya mlinzi wa mitiumbai upande wa burundi kuona mwanga wa Tochi na haitimae kuanza kupiga kelele na hatimae watu hao wakakimbia huku wakiacha vipao na mifuko ambayo viongozi wa serikali ya Burundi wanasema mifuko hiyo ingeliwasaidia kuweka miili ya watu hao iwapo wangelifaulu operesheni hiyo chafu.

Kutokana na tukio hilo Rwanda imeanza kukodoleaa macho licha ya hapo awali kukanusha kwamba watu hao hawakutoka nchini Rwanda, wakati huu shinikizo limeongezeka kuzitaka pande mbili yaani Birindi na Rwanda kuanzisha uchunguzi wa haraka kubaini watu hao ni kutoka Rwanda au Burundi.


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...