Kiongozi wa baraza la Senete nchini Rwanda ametangaza kujiuzulu nafasi yake
juma hili kwa kile alichodai ni sababu binafsi lakini vyombo vya
habari nchini humo vimedai ni kwasababu ya wabunge wenzake kuitisha
kura ya kuwa na imani nae.
Jean-Damascene
Ntawukuliryayo alikuwa akishikilia wadhifa huo toka mwaka 2011 ambapo
kujiuzulu kwake kumeelezwa kunatokana na hofu ya kisiasa iliyotanda
nchini Rwanda wakati huu baadhi ya wapinzani wakikamatwa.
Jean-Damascene
anatoka chama cha pili kikubwa cha upinzani cha The Social Democratic
PSD ambacho kinashirikiana na serikali ya rais Paul Kagame.
Baadhi
ya wabunge wa Seneti walihoji utendaji kazi wa Jean-Damascene na
kutaka kupigw akura ya kutokuwa na imani nae.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire