Marekani
imeshambulia kwa mara ya kwanza ngome za kundi la IS zilizo karibu
karibu na mji mkuu Bagdad nchini Iraq. Duru za kuaminika zimearifu
kuwa mashambulizi 160 tayari yametekelezwa katika eneo la kusini
magharibi mwa Mji huo.
Kulingana
na taarifa ya uongozi wa jeshi la Marekani katika ukanda mashariki ya
kati Mashambulizi hayo yamelenga ngome za kundi la Islamic State
katika eneo la kaskazini magharibi na yalilenga kulisaidia jeshi la
Iraq katika mapambano dhidi ya wanamgambo hao.
Mashambulizi
mengine ya anga yametekelezwa pia katika eneo la kaskazini karibu na
mji wa Sinjar na kuharibu magari sita ya kijeshi ya kundi la IS.
Tangu
Agosti 8 mwaka huu jeshi la Marekani linaendesha mashambulizi dhidi
ya wapiganaji wa kundi la Islamic State ambao wameendelea kuwa tishio
kwa usalama wa ukanda wa mashariki ya kati na ambo wamekalia maeneo
kadhaa ya Iraq na Syria.
Rais
Obama alitangaza hibi karibuni kuwa tayari kutekeleza mashambulizi
dhidi ya ngome za IS nchini Syria huku akitupilia mbali hatuwa yoyote
ya ushirikiano wa Marekani na serikali ya Damascus ambayo amesema
imepoteza uhalali katika kulipiga vita kundi hilo. Hadi leo hakuna
shambulizi lolote lililotekelezwa na Marekani dhidi ya kundi hilo
nchini Syria.
Hayo
yanajiri wakati jumuiya ya kimataifa katika kikao kilichofanyika
jijini Paris nchini Ufaransa ikikubaliana na mpango wa Marekani
kuungana katika kuisaidia Irak kwa njia zote zikiwemo za kijeshi
katika harakati zake za kupambana na wanajihadi wa kundi la Islamic
State bila hata hivyo kutaja hatuwa zilizochukuliwa dhidi ya kundi
hilo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire