Pages

mardi 16 septembre 2014

RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA AZITUHUMU NCHI ZA MAGHARIBI KUSUASUA KUHUSU JANGA LA EBOLA


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezituhum nchi za magharibi kwa kushindwa kuchukuwa hatuwa za haraka kukomesha janga la Ebola na badala yake zina suasua katika kuchukua mikakati madhubuti ya kulipiga vita janga hili.
Rais Kenyatta ameyasema hayo kutokana na kile kinachoendelea katika nchi za ukanda wa Afrika magharibi zinazo kabiliwa na maradhi hayo, na kudai kuwa iwapo maradhi hayo yangeliripotiwa barani Ulaya au Marekani hatuwa madhubuti zingechukuliwa.
Rais Kenyatta amesema iwe kwenye upande wa kupamabana na maradhi hayo ya Ebola, au vita dhidhi ya Ugaidi, ushirikiano wa nchi za Afrika unahitajika kuweka fuko la pamoja kwa ajili ya kukabiliana na hali za dharura zinazo jitokeza barani Afrika na hapo ndipo Afrika itakuwa tayari kupata suluhu kwa tatizo la Afrika na sio kusubiri nchi za magharibi.
Uhuru Kenyatta aliyasema hayo wakati wa ghafla maalum ya kukabidhi tuzo ya kimataifa ya UNESCO mjini Malabo nchini Guinea Eqweta.
Viongozi wa Afrika walioshiriki katika ghafla hiyo walikutana kwa dharura kujadiliana kuhusu ushirikiano juu ya kutafuta uwezo wa kifedha katika kupambana na virus vya Ebola barani Afrika.
Janga la Ebola linalilikumba eneo la ukanda wa Afrika Magharibi tayari limegharimu maisha ya watu 2400. nchi ziliguswa sana ni pamoja na Sierra Leone, Guinea na Liberia. Janga hili limeripotiwa pia nchini Nigeria, Guinea, Senegal na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Tangu kipindi kadhaa serikali ya Kenya ilisitisha safari zake katika nchi za ukanda wa Afrika Magharibi.
Mbali na hayo, Kenya pia ilizuia habiria kutoka katika nchi zinazo kabiliwa na maradhi hayo kuingia nchini Kenya.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...