Polisi
nchini Tanzania hapo jana imekabiliana na wafuasi wa mpinzani wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, baada ya mwenyekiti wa chama hicho Freeeman Mbowe kuwasili katika ofisi za makao makuu ya polisi kutokana na tuhuma
zinazo mkabili za uchochezi kuhusu kauli yake ya kuitisha maandamano
nchi nzima.
Polisi
nchini Tanzania ililazimika kufunga barabara inayoelekea kwenye ofisi
za makao makuu ya polisi kutokana na wafuasi wa Chadema waliokuwa
wamefurika kwa wingi katika eneo hilo, jambo ambalo linadaiwa kuwa
kinyume.
Hata
hivyo waandishi wa habari ambao walikuwa wamejielekeza katika eneo
hilo kwa ajili ya kuripoti habari hawakurahisishiwa na polisi na
kujikuta polisi ikikabiliana nao kuwafurusha katika eneo hilo, huku
wengine wakidai kunyanyaswa na Polisi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire