Manusura
na mashuhuda wa shambulio la kigaidi katika eneo la kibiashara la
Westgate nchini Kenya wanaendelea kutowa ushuhuda kwa kile
walichokiona wakati wa shambulio hilo, wakati huu Kenya ikifanya wiki
ya kumbukumbu ya mashambulizi hayo.
Eneo
hilo la kibiashara ambalo lilikuwa muhimu katika uchumi wa Kenya,
lilishambuliwa mwaka mmoja uliopita na kundi la watu wenye silaha na
kuwauawa watu 67 kulingana na duru za serikali, tukio ambalo
lilidaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa Al Shabab baada ya kujigamba
kwamba wanalipiza kisase kutokana na vikosi vya Kenya kufanya mashambulizi katika ngome zao nchini Somalia.
Inahofiwa huenda watu zaidi 67 walipoteza maisha katika tukio hilo mbaya kuwahi kutokea nchini Kenya.
Hayo yanajiri wakati huu Polisi nchini Kenya ikiimarisha Usalama katika maeneo mbalimbali huhu kukiwa na minong'ono miongoni mwa wananchi kuhusu mwenendo wa polisi nchini humo kwa raia.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire