Mpiga
picha raia wa marekani aliepata mambukizi ya virus vya Ebola nchini
Liberia amesafirishwa kuondoka jijini Monrovia, duru za mashirika ya
kibinadamu zimearifu.
Ashoka
Mukpo mwenye umri wa miaka 33 mpiga picha na ambaye aliajiriwa hivi
karibuni na kituo cha Marekani cha NBC aliwekwa katika hali ya hatari
tangu jumatano juma lililopita katika kituo cha shirika la madaktari
wasiokuwa na mipaka.
Mwenyekiti
wa kituo cha NBC Deborah Turness alifahamisha tangu siku ya Ijumaa
iliopita kwamba mpiga picha huyo atasafirishwa hadi kwenye kituo
kingine kwa ajili ya matibabu zaidi, huku wengine ambao hawaonyeshi
dalili zozote za virusi vya Ebola watarejeshwa nyumbani na kuwekwa
kqenye hali ya hatari kwa kipindi cha siku 21 kama inavtogizwa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire