Herve
Ladsous naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anaye husika na
opersheni za kulinda amani yupo nchini Mali ambako atahudhuria
sherehe za kuiaga miili ya wanajeshi tisa wa Nigeria waliouawa katika
shambulio liliotokea siku ya Ijuma juma lililopita.
Miili
ya wanajeshi hao tisa wa kulinda amani kutoka nchini Nigeria itawekwa
nje kwenye makao makuu ya vikosi vya kulinda amani jijini Bamako
ambako mawaziri Abdoulaye Diop, wa mambo ya ndani nchini Mali pamoja
na waziri wa Ulinzi Meja Kanali Bah Ndaw wanatahudhiria
Upande
wa Minsuma, mbali na Herve Ladsous atakuwepo pia Arnaud Acodjénou
naibu kiongozi wa opersheni za Umoja wa Mataifa, ambao wamekuja
kutowa heshima za mwishi kwa wanajeshi hao waliojitolea kwa ajili ya
amani barani Afrika. Herve Ladsous atatumia fursa hiyo kukutana na
rais wa Mali Ibrahima Bubakar keita.
Herve
Ladsous atajadili pia kuhusu swala la wanajeshi wa kulinda amani
kutoka nchini Tchad ambao wanatishio kurejea nyumbani baada ya
kupoteza mara kadhaa wanajeshi wake kutokana na bomu za kutegwa
ardhini zilizo tengwa na wanamgambo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire