Kundi
moja la waasi nchini Burundi, limejigamba hapo jana kuhusika katika
shambulio dhidi ya kituo kimoja cha kijeshi nchini humo karibu na
mpaka na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na kukiri kuwauwa
wanajeshi sita katika shambulio hilo, idadi iliokanushwa na jeshi la
taifa hilo.
Msejaji
wa jeshi la Burundi kanali Gaspard Baratuza amefahamisha kwamba
kulikuwa na makabiliano na kundi la wahuni, na kukanusha taarifa ya
kupoteza wanajeshi, badala yake kuthibitisha kuwa wamemuua muasi
mmoja katika shambulio hilo.
Kundi
hilo la waasi linasadikiwa kuwa ni miongoni mwa wafuasi wa chama cha
FNL walioasi na kuanzisha uasi. Kulingana na msemaji wa kundi hilo
Felix Jean Ntahonguriye amethibitisha kwamba walishambulia kituo cha
jeshi kilichopo katika tarafa ya Gihanga kwenye umbali wa kilometa
zaidi ya Ishirini na jiji la Bujumbura na baadae kutokomea katika
msitu wa Rukoko karibu na DRCongo.
Tangu
mwanzoni mwa mwaka huu, kundi hilo limekuwa likijigamba kuhusika na
mashambulizi kadhaa ambapo kulingana na msemaji wa kundi hilo
wataendelea kutekeleza mashambulizi dhidi ya vituo vya jeshi la
Burundi hadi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.
msemaji
wa jeshi la Burundi Gaspard Baratuza amepuuzia kitisho hicho na
kusema kwamba ni kundi la wahuni waliopoteza dira na haliwezi
kupambana na jeshi la serikali.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire