Mpiganaji
mmoja wa kijihadi wa kundi la Mujao, moja miongoni mwa makundi yalio
kalia eneo la kaskazini mwa Mali amejigamba kuhusika na shambulio la
kujitowa muhanga dhidi ya Kikosi cha Umoja wa mataifa nchini Humo.
Shambulio
la siku ya Ijumaa dhidi ya kikosi cha Umoja wa Mataifa cha majeshi
kutoka nchini nigeria lilisababisha vifo vya watu 9.
Uongozi
wa kikosi cha Kulinda amani cha Umoja wa Mataifa Minusma, umesema
hili ni shambulio kubwa kuwahi kutokea tangu kutumwa kwa majeshi ya
Umoja wa Mataifa tangu kutumwa kwake Julay 2013.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire