Pages

jeudi 15 juin 2017

WATU 6 WAPOTEZA MAISHBA KATIKA SHAMBULIO LA KUJITOA MUHANGA MJINI MOGADISHU

Watu sita wameripotiwa kufa na wengine mamia wamejeruhiwa baada ya mtu aliyejitoa muhanga kwa kutumia gari kulenga mgahawa mmoja maarufu ulioko mjini Mogadishu, Somalia wakati watu wakiwa wanakula futari.

Polisi mjini Mogadishu imethibitisha kutoke kwa tukio hilo ambalo imesema kuwa mtu aliyejitoa muhanga aliendesha gari lililokuwa na vilipuzi ndani ya jengo ambalo mgahawa wa Posh Treat ulikuwa umesheheni waumini wa dini ya kiislamu.

Afisa wa polisi Abukar Mohamed amethibitisha kuuawa kwa watu sita na wengine kadhaa kujeruhiwa na kuongeza kuwa operesheni ya kukagua jengo hilo imeendelea usiku kucha huku eneo lote la mgahawa huo likiwa limefungwa.

Kundi la Al-Shabab ambalo lina uhusiano na mtandao wa kigaidi wa AL-Qaeda kundi ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara mjini Mogadishu kuvilenga vikosi vya Serikali na vile vya kigeni, limekiri kuhusika kwenye shambulio hili.

Mara nyingi wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadan kundi la Al-Shaba limekuwa likizidisha mashambulizi yake nchini Somalia.


ICC YATAKA SEIF AL ISLAM AKAMATWE BAADA YA KUACHIWA JUMA LILILOPITA

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC ametoa wito wa kukamatwa na kujisalimisha kwa mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya marehemu kanali Muammar Gaddafi, Seif al-Islam aliyeachiwa juma lililopita kutoka kwenye gereza la Zintan alikokuwa anashikiliwa.

Mwendesha mashtaka Fatou Bensouda amesema kuwa hati ya kukamatwa kwa Seif al-Islam iliyotolewa na mahakama hiyo mwaka 2011 bado ni halali na viongozi wa Libya wanawajibika kumkamata licha ya msamaha wowote aliopewa nchini humo.

Seif al-Islam aliripotiwa kuachiwa huru Ijumaa ya wiki iliyopita na waasi wa eneo la Zintan, kundi ambalo lilikuwa likimshikilia kwa zaidi ya miaka mitano ambapo lilitangaza kumuachia huru kwa msamaha katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadan.

Hata hivyo ofisi ya mwendsha mashataka wa ICC iliyoko mjini Tripoli Libya ambako iko Serikali inayotambuliwa kimataifa, imesema kuwa msamaha huo hauwezi kumuhusu Seif al-Islam kwa sababu tu ya aina ya makosa anayotuhumiwa nayo.


Bensouda amesema Seif al-Islam anatakiwa na mahakama hiyo kwa tuhuma za makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na kwamba hivi sasa wanajaribu kujua mahali aliko.

WAKATI MZOZO WA QATAR NA NCHI ZA GHUBA UKIENDELEA MAREKANI YASAINI MKATABA WA KUIUZIA QATAR NDEGE ZA KIVITA

JIM MATTIS waziri wa Ulinzi wa Marekani
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu hapo jana amefanya mazungumzo na mfalme wa Qatar, mazungumzo ambayo yalilenga kuendelea kujaribu kutafuta suluhu kati ya nchi hiyo na mataifa mengine ya Ghuba wakati huu pia umoja wa Mataifa ukieleza kuguswa na hali inayoendelea.

Haya yanajiri wakati huu nchi ya Marekani kupitia kwa waziri wake wa mambo ya Kigeni Rex Tillerson akizikosoa nchi za Ghuba kwa kukitangaza chama cha Muslim Brotherhood kama kundi la kigaidi wakati kipo karibu kwenye nchi zote za Ghuba na baadhi ya wafuasi wake ni viongozi.

Miongoni mwa vikwazo vilivyotangazwa dhidi ya Qatar ni pamoja na nchi hiyo kutakiwa kuacha ufadhili wake kwenye chama cha Muslim Brotherhood.


Katika hatua nyingine waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis na mwenzake wa Qatar Khalid al-Attiyah wametiliana saini makubaliano ya nchi hiyo kuiuzia Qatar ndege za kivita zenye thamani ya dola bilioni 12.s

mardi 6 juin 2017

MSULUHISHI KATIKA MGOGORO WA BURUNDI BENJAMIN MKAPA AKIRI KUWEPO KWA CHANGAMOTO NYINGI KATIKA KUWALETA PAMOJA WANASIASA WA BURUNDI

Wakati mazungumzo ya kusaka amani nchini Burundi yakionekana kukwama, risala inayoonekana kuwa ya siri ya mratibu wa mazungumzo kwa viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki katika mkutano wa Mei 20, inatembea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Ali Bilali anatudokzea yaliomo kwenye hotuba hiyo.

Katika risala hiyo iliovuja, Benjamin Willima Mkapa ambae sio mara nyingi kuzungumzia shughuli zake katika mazungumzo ya Warundi, ametaja matatizo kadhaa anayo kabiliana nayo katika juhudi za kuwaleta pamoja wanasiasa wa Burundi.

Tangu kukabidhiwa jukumu zito la kuwaleta pamoja wanasiasa wa Burundi, mratibu wa mazungumzo Benjamin Mkapa, ameandaa vikao mara tatu mjini Arusha, vikao ambavyo havikuzaa matunda yoyote hadi sasa.

Mwaka mmoja tangu uteuzi huo msuluhishi katika mzozo huo hajafaulu kuzileta pamoja pande zote katika mgogoro wa Burundi, amekuwa akikutana nao kwa nayakati tofauti na ambapo wamekuwa wakimpa maoni ambayo inaonekana imekuwa vigumu kuyaweka pamoja.

Seriali ya Burundi inashikilia msimamo wake kwamba nchi ni tulivu, mazungumzo lazima yafanyike nchini Burundi na imeanza mchakato wa manadiliko ya katiba, jambo ambalo linatupiliwa mbali na upinzani unaodai kuwa usalama ni mdogo huku watu wakitiwa nguvuni kiholela, matukio ya utesaji, unyanyasaji, na watu wanaotoweka katika mazingira tatanishi.

Neno msuguano limerejea mara nyingi katika risala hiyo ambapo serikali imeelezwa kuwajibika katika kusuasua kwa mazungumzo hayo. Mratibu anawataka viongozi wa serikali kuonyesha dhamira ya dhati kwa kufuta waranti ya kukamatwa kwa viongozi wa upinzani na wa mahirika ya kiraia, kuwaacha huru wafungwa na kukubali kuzungumza na makundi yanayo shikilia silaha.

Katika kutamatisha risala hiyo ya siri, Benjamin Mkapa ameeleza ofisi yake imeathirika mara kadhaa na uvujishwaji wa taarifa. Na kukumbusha kwamba baadhi ya nyaraka huwasilishwa kwa sekretarieti ya jumuiya ya Afrika mashariki.



vendredi 22 juillet 2016

TANZANIA YAZUIA USAFIRISHAJI WA CHAKULA KUELEKEA NJE YA NCHI


Tanzania imezuia usafirishaji wa mazao ya vyakula nje ya nchi natayari madhara yake yameanza kushuhudiwa ndani na nje ya nchi.


Rusumo, Kabanga na Kobero kwenye mipaka baina ya Tanzania,Rwanda na Burundi kumeshuhudiwa utekelezwaji wa amri ya serikali ya Tanzania kutosafirisha mazao nje ya nchi. Bw Thabiti Chiwalo ni afisa afya ya mimea na mazao mpakani Kabanga amesema kwamba wamepokea taarifa kupitia idara ya ukaguzi wa mazoa kwamba mazao ya aina yoyote yasipite mpakani na zoezi hilo litandelea hadi pale utaratibu utapo badilika.


Kwa sasa hakuna huduma yoyote ya kutoa mazao yoyote kutoka Tanzania kuelekea Burundi. Thabiti amebainisha kuwa madhara ya usafirishaji mazao yameonekana zaidi kwenye mpaka wa Rusumo, anasema hali ni mbaya zaidi katika mpaka huo ambapo kuna malori zaidi ya 50 ambapo nafaka za chakula kama maharage, mahindi, mchele, kutoka na hatuwa hiyo inabidi malori hayo yarejea nchini Tanzania.


Hatuwa hiyo ya Tanzania, imesababisha ugumu wa maisha kwa wananchi wa Burundi hususan wa maeneoya mpakani ambao wanasema wameshuudiwa malori ya mizigo yakigeuza kurudu Tanzania kama ilivyo elekezwa na serikali.


Licha ya Tanzania kupiga marufuku usafirishaji wa mazao nje ya nchi na baadhi ya maafisa kusimamishwa kazi kwa kutoa vibali vya kusafirisha mazao nje, lengo kuu ikiwa ni kuhakiki akiba ya chakula nchini, baadhi ya maafisa wameiambia RFI kuwa mazao hayo yanasafirishwa kupitia njiazisizo halali. Julian Rubavu RFI.


lundi 18 juillet 2016

RAIS WA UTURUKI AAHIDI KUMALIZA KILE ALICHOKIITA VIRUSI

Mamlaka nchini Uturuki zimeendelea na operesheni ya kuwasaka na kuwakamata watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi lililoshindikana, dhidi ya Rais Racep Tayyip Erdogan, ambapo mpaka sasa watu zaidi ya elfu 6 wanashikiliwa, huku Serikali ikiapa kumaliza kile ilichokiita “Virusi”.

Hapo jana wakati rais Erdogan akihudhuria ibada maalumu ya mazishi kuwakumbuka raia na wanajeshi waliouawa wakati wa jaribio la mapinduzi, amesema kuwa nchi yake inafikiria upya kurejesha adhabu ya kifo, licha ya wasiwasi ulioneshwa na jumuiya ya Kimataifa.

Viongozi wa dunia, akiwemo Rais wa Marekani, Barack Obama, wamealaani jaribio la mapinduzi lililoshindikana Ijumaa ya wiki iliyopita na wanajeshi walioasi, ambapo kwa mujibu wa Serikali watu zaidi ya 300 waliuawa.

Hata hivyo kumekuwa na hofu ya kutekelezwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa watuhumiwa wa jaribio hilo, baada ya kuonekana kwa picha zikiwaonesha maofisa wa Serikali wakiwanyanyasa wanaodaiwa kuwa ni watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi.

Waziri wa sheria wa Uturuki, Bekir Bozdag, amesema kuwa watu wanaokadiriwa kufikia elfu 6 wamekamatwa katika operesheni maalumu ya kusafisha jeshi na taasisi za Serekali ambazo anadai zimevamiwa na watu wanaotaka kutekeleza mapinduzi, huku akionya kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka.


PADRI MALU MALU KUZIKWA LEO MJINI BUTEMBO

Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo CENI, padre Apolinaire Malu Malu Muholongu, umewasili katika mji wa Butembo mkoani Kivu ya kaskazini ambako unatarajiwa kuzikwa hivi leo.

Kabla ya kusafirishwa hadi Butembo, mwili wa kiongozi huyo uliagwa na umati wa watu mjini Kinshasa, wakiwemo wanasiasa na maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRC.


Katika kuithamini kazi yake na juhudi nyingi za kidiplomasia alizoongoza kwa niaba ya serikali ya nchi hiyo, Rais Joseph Kabila, amemtaja Malumalu kama shujaa, akifananisha yale aliyoyafanya na viongozi maarufu nchini humo kama, Emery Patrice Lumumba na marehemu Laurent Desire Kabila.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...