Pages

lundi 4 mai 2015

WATU WAWILI WAUAWA KATIKA MASHINDANO YA KUCHORA VIBONZO VYA MTUME MUHAMAD JIJINI TEXAS


Watu wawili wanaodaiwa kuwa huenda walikuwa wamebeba mabomu wameuawa kwa kupigwa risasi, na polisi mmoja kujeruhiwa nje ya ukumbi ambao kulikuwa kunafanyika mashindano ya kuchora kikaragosi cha Mtume Muhammed mjini Texas, Marekani.

Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo kutoka taasisi ya Marekani ya kulinda uhuru wa kutoa maoni, wamesema kuwa watu hao waliuawa baada ya kurusha risasi kuelekea sehemu ambayo shindano hilo lilikuwa linafanyika na ndipo polisi walipolazimika kutumia nguvu kuwakabili.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hili, wanasema kuwa wakati shindano hilo likiendelea, watu wawili waliokuwa na silaha na vifaa vinavyodaiwa kuwa ni mabomu walianza kusogea kwenye eneo la tukio na kabla ya kufika waliwafyatulia risasi polisi walipkuwa jirani na kuwalenga baadhi ya watu waliohudhuria kabla ya kuuawa na kikosi maalumu cha Polisi wanajeshi.

Polisi mjini Texas wanasema wanaendelea kufanya uchunguzi kubaini sababu iliyowafanya watuhumiwa hao kuwafyatulia risasi waandaaji wa shindano hilo, ingawa baadhi ya watu wamewakosoa watu walioandaa shindano hilo wakijua fika kuwa lazima lingewakera baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu.

Waumini wa dini ya kiislamu wamelaani shambulio hili lakini wakawakosoa waandaaji wa shindano hilo ambalo mshindi alizawadia dola za Marekani elfu 10 kwa kuchora kibonzo wa kinachomuonesha Mtume Muhammad.

Tukio hili linajiri ikiwa ni miezo michache tu imepita toka kushambuliwa kwa ofisi za gazeti la Charlie Hebdo nchini Ufaransa ambalo lilichapisha kibonzo cha mtume Muhammed, ambapo watu wenye silha waliwashambulia wafanyakazi wake na kuua watu 16.

MAANDAMANO YASHUHUDIWA TENA JIJINI BUJUMBURA KULAANI MUHULA WA 3 WA RAIS NKURUNZIZA

Waandamanaji wamerejea barabarani katika baadhi ya mitaa za manispaa ya jiji la Bujumbura mapema leo asubuhi baada ya Makataa ya saa 48 yaliyotolewa na waandamanaji nchini Burundi kumpa nafasi Rais Nkurunziza kufikiria upya uamuzi wake wa kugombea muhula wa tatu kinyume na katiba na azimio la Arusha kufikia mwisho.

Taarifa kutoka Bujumbura zaeleza kuwa waandamanaji katika mitaa ya Buterere, Musaga, Nyakabiga, Bwiza wamechoma ma tyri barabarani huku katika tarafa ya buterere risase zikisikika kwa wingi, na huko Kinama vipeperushi vimesambazwa vinavyo wartia hofu waandamanaji kwamba ataeandamana basi watakiona cha moto

Tangu kuanza kwa maandamano hayo April 26 mwaka huu, watu 10 wameuawa wakati wa maandamano na ambapo shughuli za mazishi kwa baadhi ya wahanga hao zikifanyika hapo jana ambapo rais wa zamani wa Burundi Domitien Ndayizeye alisisitiza kuheshimiwa kwa katiba ya nchi.


Wakati hayo yakijiri, Mkuu wa jeshi nchini humo, Jenerali Prime Niyongabo akisoma tangazo maalum la jeshi, amerejelea kauli ya waziri wa Ulinzi Nchini Humo Brigadia Jenerali Pontien Gaciyubwenge siku ya jumamosi, ambapo amelisifu jeshi nchini humo kwa weledi wake katika kipindi chote cha maandamano hayo na kulionya kutokuwa na upande wowote.

Wataalamu wanaona kwamba taarifa ya jeshi ya kutaka viongozi kuheshimu katiba na mkataba wa Arusha ni ujumbe wa moja kwa moja kwa rais Nkurunziza ambae kulingana na Upinzani na wanaharakati wa mashirika ya kirai, anataka kuvunja makubaliano ya Arusha.

Kumekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na hali inayoendelea nchini Burundi wakati huu polisi ikiendelea kuwatisha raia kutoandamana, jambo ambalo linalowafanya raia kuwoana polisi kama adui.


Jumuiya ya Kimataifa imeonya Burundi kuhusu hali inayoendelea kushuhudiwa nchini humo na kwamba iwapo hatua hazitachukuliwa mapema huenda taifa hilo likaingi kwenye machafuko.

mardi 21 avril 2015

MAREKANI YALAANI MASHAMBULIZI DHIDI YA WAGENI NCHINI AFRIKA KUSINI


Mfalme Goodwill Zwelithini wa jamii ya waZulu nchini Afrika kusini aliyetuhumiwa kuwa chanzo cha vurugu dhidi ya wageni amekanusha kuhusika kwake na matukio hayo.

Katika mkutano wa hadhara Zwelithini amekanusha kuhusika katika vurugu hizo na kudai kuwa ametafsiriwa vibaya baada ya kauli yake ya kuomba wageni kufungasha virago na kuondoka nchini humo.

Mkutano wa dharura wa viongozi wa kijadi nchini humo akiwepo mfalme huyo pamoja na mkutano baina yake na mawaziri wa Mambo ya Ndani na wa Usalama yaonekana kuwa chachu ya kukomesha mashambulizi hayo ambapo Mfalme Zwelithini amesema kuwa mashambulizi dhidi ya wageni ni aibu kubwa kwa taifa.

Serikali ya Marekani imelaani jana machafuko ya ubaguzi dhidi ya wageni yanayoshuhudiwa nchini Afrika Kusini na kuwatolea wito viongozi wa nchi hiyo kuchukuwa hatuwa madhubuti kukomesha mashambulizi dhidi ya wageni.

Machafuko hayo yaliwalenga raia wa kigeni waishio nchini Afrika Kusini na kusababisha vifo vya watu 7 na maelfu wengine kukimbia katika miji ya Durban na Johanesbourg.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Marie Harf amesema Marekani kama vile mataifa mengine pamoja na mashirika ua kiraia wanalaani vikali mauaji dhidi ya wageni yanayo shuhudia nchini Afrika Kusini.


Hayo yanajiri wakati huu mataifa kadhaa barani Afrika yakiendelea kujiandaa kuwarejesha nyumbani raia wake waishio nchini Afrika Kusini. Miongoni mwa mataifa hayo ni pamoja na, Malawi, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe na Tanzania.

SERIKALI YA BURUNDI YATISHIA KUTUMIA JESHI KUZIMA MAANDAMANO


Serikali ya Burundi imetishia jana kulitumia jeshi iwapo maandamano ya kupinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza yatagubikwa na ghasia wakati huu nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais.

Waziri wa ulinzi nchini humo jenerali Pontien Gaciyubwenge amesema iwapo itahitajika na kamanda wa majeshi ambae ni rais wa jamuhuri jeshi lake litajiunga na vikosi vingine katika swala zima la ulinzi dhidi ya wanataka kuyumbisha amani.

Upande wake waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana amesema vikosi vya Usalama na utawala vipo makini na vitachukuw ahatuwa stahiki ili kuwafikisha mahakamani wahusika wote wa maandamano.


Hayo yanajiri wakati huu wanasiasa wa Burundi waliokimbilia ugenini wakimtaka rais Nkurunziza kutumia uamuzi wa busara na kutowa uhuru kwa wote kwa ajili ya maandalizi thabiti ya uchaguzi.

lundi 20 avril 2015

SERIKALI YA AFRIKA KUSINI YAWAONYA WACHOCHEZI WA VURUGU DHIDI YA WAGENI



Serikali ya Afrika Kusini imeahidi hapo jana kuwahukumu wahusika wa machafuko dhidi ya raia wa Kigeni nchini humo yaliosababisha vifo vya watu takriban saba tangu mwanzoni mwa mwezi April wakati huu Malawi na Zimbabwe zikijiandaa kuwarejesha nyumbani raia wake.

Waziri wa mambo ya ndani nchini Afrika Kusini Malusi Gigaba amesema jana katika mkutano na waandhishi wa habari kwamba wametuma ujumbe mzito kwa wale waliohusika na machafuko hayo kwamba watakamatwa na watakiona cha moto.

Kulingana na waziri huyo watu 307 wametiwa nguvuni tangu mwanzoni mwa machafuko hayo yalioanza mwishoni mwa mwezi March na ambayo yanawalenga raia wa Kigeni walioomba hifadhi nchini Afrika Kusini.


Licha ya kupungua kwa ghasia hizo, katika usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili kumeshuhudiwa mashambulizi mengine dhidi ya raia wa kigeni katika miji ya Johanesbourg na D

MAANDAMANO MAPYA YAITISHWA TENA LEO JUMATATU NA UPINZANI NCHINI BURUNDI


Upinzani nchini Burundi imetowa wito wa maandamano tena leo Jumatatu April 20 mwaka 2015 katika jiji kuu la Bujumbura. Wito huu umetolewa na mmoja kati ya viongozi wa upinzani wa chama cha UPD-Zigamibanga Chauvino Murwengezo ambae amewataka wafuasi wa upinzani na wale wote wanaopinga muhula wa 3 wa rais Pierre Nkurunziza.

Hayo yanajiri wakati mwishoni mwa Juma mahakama kuu jijini Bujumbura ikiwafungulia Mashtaka waandamanaji 65 waliokamatwa wakati wa maandamamno ya kumshinikiza rais Piere Nkuzrunziza kutowania urais kwa muhula wa tatu.


Siku ya Ijumaa juma lililopita shughuli zilizorota kutokana na vurugu za maandamano ambapo Polisi wa Usalama waliwasambaratisha waandamanaji ambao walidai kuandamana kwa amani na utulivu.

Kidole cha lawama kinaelekezwa kwa vyombo vya Usalama nchini humo ambavyo vimeonekana kuegemea upande mmoja, kwani wafuasi wa rais Nkurunziza wanaounga mkono muhula wa 3 wanapoafanya maandamano hupewa ulinzi mkali wa polisi.

Kiongozi mmoja wa upinzani amesema iwapo machafuko yatatokea au vurugu, zinasababishwa na polisi na wao ndio wataulizwa kupitia viongozi wao ambao hawataki kutowa haki sawa kwa wote.

Hali hii ya wasiwasi inayo shuhudiwa kwa sasa nchini Burundi imesababisha watu zaidi ya elfu nane kukimbilia nchini Rwanda na DRCongo kwa hofu ya kuzuka kwa machafuko.

Upinzani pamoja na Mataifa ya Magharibi yanamtaka rais Nkurunziza kuheshimu katiba na kutowania wadhifa huo wakati wa Uchaguzi wa urais mwezi Juni.

Nkurunzinza mwenyewe hajajitokeza na kutangaza ikiwa atawania au la.



MAREKANI NA ETHIOPIA WALAANI MAUAJI YA ISLAMIC STATE DHIDI YA WA CHRISTO

Serikali ya Ethiopia imelaani vikali mkanda wa Video uliochapishwa na kundi la Islamic State ukionyesha watu 28 wakiuawa kwa kukatwa vichwa na ambao waliwasilishwa na kundi hilo kama raia wa Ethiopia.

Mbali na Ethiopia, serikali ya Marekani pia imetowa taarifa ambamo pia imelaani mauaji hayo ambayo imeyaita ya kinyama.

Kundi hilo la IS kitengo cha Libya limeoyesha mkanda huo ikiwa ni miezi miwili baada ya kuonyeshwa kwa mauaji mengine ya watu 21 wachristo waumini wa Copte kutoka Misri, hali iliozua ghadhabu kwa serikali ya Misri iliojibu tukio hilo kwa mashambulizi ya kijeshi katika ngome za kundi hilo nchini Libya

mkanda huo wa video wenye dakika 29 inaonyesha makundi mawili ya watu waliowasilishwa kama waumini wa kanisa la Ethiopia ambalo wamesema ni adui.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...