Pages

lundi 18 juillet 2016

AU WAJADILI USALAMA WA SUDANI KUSINI NA BURUNDI

Viongozi wa Umoja wa Afrika wanajdili kuhusu usalama wa Sudani Kusini na Burundi ambako mzozo wa kisiasa umeendelea kutokota katika nchi hizo, na ambapo mwenyekiti wa Umoja huo amewatolea wito viongozi wa mataifa hayo kuheshemu makubaliano na mikataba mbalimbali iliofikiwa.

wakati huo huo rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na makamu wake wa kwanza wa Rais Riek Machar, wamekubali kukutana kwa mazungumzo, ili kusaka muafaka wa kurejesha amani nchini humo, baada ya mapigano yaliyoshuhudiwa juma moja lililopita.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume inayosimamia utekelezwaji wa mkataba wa amani uliotiwa saini na viongozi hao kumaliza vita nchini humo, Festus Mogae, amethibitisha Rais Kiir kuzungumza kwa njia ya simu na Riek Machar na kukubaliana kukutana, wakati huu pia jumuiya ya nchi za IGAD, ikifikiria kutuma wanajeshi elfu 14 nchini Sudan Kusini kulinda amani.

Viongozi Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika, wanaotarajiwa kutamatisha kikao chao hivi leo jijini Kigali, Rwanda, wanatarajiwa kutoka na maazimio kuhusu kinachoshuhudiwa kwenye nchi hiyo.

Hata hivyo maswali bado ni mengi ikiwa kweli wakuu hawa wa nchi wana nia ya dhati ya kumaliza machafuko Sudan Kusini, na kama watatoka na maazimio mahsusi kumaliza mgogoro wa nchi hiyo.


Haji Kaburu ni mchambuzi wa siasa za kimataifa, akiwa jijini Dar es Salaam, Tanzania na hapa anaeleza mtazamo wake.

lundi 14 décembre 2015

MAREKANI YAWATAKA RAIA WAKE KUONDOKA BURUNDI

Serikali ya Marekani imewataka raia wake wanaoeshi nchini Burundi kuondoka mara moja nchini humo kufuatia kuendelea kuhatarishwa kwa hali ya usalama nchini humo tangu pale lilipofeli jaribio la mapinduzi mwezi Mei mwaka huu lililofuatiwa na machafuko na mzozo wa kisiasa.

Katika taarifa ya wizara ya mambo ya nje wa Marekani hapo jana imewataka raia wa Marekani wasiokuwa na shughuli muhimu kuondoka nchini humo na familia zao na kuwataka raia wote wa Marekani kutoelekea Burundi, na wale waliopo nchini humo kuondoka haraka iwezekanavyo.

Zaidi ya watu 90 wameuawa siku ya Ijumaa Juma lililopita baada ya kutokea kwa mashambulizi ya kambi tatu za kijeshi nchini humo, ambapo taarifa za jeshi la nchi hiyo ziliarugu kuuawa kwa waasi 79 na wanajeshi 8.

Jumamosi asubuhi maiti kadhaa zilizshuhudiwa katika mitaa ilioendesha maandamao ya kupinga muhula wa 3, ambapo wengi wa waliouwawa ni vijana. Mashuhuda nchini humo wamevituhumu vikosi vya Usalama kuwashikilia vijana waliokutana nao baada ya shambulio la kambi za kijeshi na kuwauwa, ambapo maiti kadhaa zilionekana zikifungwa kamba mikononi.

Kulingana na taarifa ya pamoja ua mjumbe wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini na kamishna wa ushirikiano wa kimataifa Neven Mimica wameomba ukweli uwekwe wazi kuhusu mauaji haya yanayotokea katika karne hii.


vendredi 11 décembre 2015

HALI YA SINTOFAHAM YAENDELEA KURIPOTIWA NCHINI BURUNDI BAADA YA KUTOKEA SHAMBULIO LA KAMBI YA KIJESHI









Hali ya sintofahamu yaebdelea kushuhudiwa jijini Bujumbura ambapo vyombo vya usalama vimezingira maeneo kadhaa ya jiji la Bujumbura.

kwa Mujibu wa msemaji wa jeshi Kanali Gaspard Baratuza, Kundi la watu waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito, wametekeleza mashambulizi mfululizo katika kambi mbili za jeshi jijini Bujumbura, Burundi, ambapo wapiganaji 12 wameuawa na wengine zaidi ya 24 wametiwa mbaroni, huku wanajeshi wa serikali wanaokadiriwa kufikia watano nao wakiuawa wakati wa makabiliano.

Mashambulizi haya yakupangwa, ni mabaya zaidi kutekelezwa toka kulipofanyika jaribio la mapinduzi lililoshindikana mwezi May mwaka huu.

Wapiganaji hao walivamia kambi ya jeshi ya Nagara kaskazini mwa mji wa Bujumbura pamoja na kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Iscam, kilichoko kusini mwa nchi hiyo, baada ya kupora silaha katika kambi moja eneo hilo mashambulizi yaliyoanzwa kutekelezwa alfajiri ya hii leo na kudumu kwa zaidi ya saa nne

Kuliripotiwa pia makabiliano ya risasi katika viunga kadhaa vya jiji la Bujumbura, hali inayozidisha hofu ya kiusalama kwenye taifa hilo, wakati huu ambapo inadaiwa kuwa rais Pierre Nkurunziza amefanya kikao cha dharura na mawaziri wake kuizungumzia hali hiyo.

Shughuli zimesimama jijini Bujumbura, hakuna mawasiliano ya watu kutoka katika mtaa mmoja kuelekea mtaa mwingine, hali ambayo inalalamikwa na wananchi wa kaazi wa jiji la Bujumbura baada ya kukosa chakula kutokana na kuzuiliwa kwa barabara zote kuu

Polisi na wanajeshi nchini Burundi, wanasema wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hili pamoja na kuendesha msako wa wapiganaji zaidi walioripotiwa kukimbia baada ya mashambulizi haya.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na mashambulizi ya hivi leo, lakini Serikali inasisitiza kuwa ni makundi ya waasi wanaotaka kuipindua Serikali.

vendredi 20 novembre 2015

RAIS MPYA NCHINI TANZANIA AHUTUBIA BUNGE, WAPINZANI WAONDOKA UKUMBUNI

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John pombe Magufuli, hii leo kwa mara ya kwanza amelihutubia bunge huku akiahidi kuwa serikali yake itafanya kazi kwa weledi, wakati huu pia akimwapisha waziri mkuu mpya, Majaliwa Kassim Majaliwa.


Ni sauti yake waziri mkuu mpya wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati akila kiapo hii leo mjini dodoma katika ikulu ndogo ya Chamwino, sherehe ambayo mbali na kuhudhiriwa na rais wa Zanzibar na viongozi wastaafu, wabunge na wageni mbalimbali nao walihudhuria.


Baada ya sherehe za kuapishwa kwa waziri mkuu, baadae wabunge walirejea bungeni ambako rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli aliwahutubia, ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo toka alipoteuliwa kuwa rais baada ya uchaguzi wa October 25 mwaka huu.


Kwenye hotuba yake rais Magufuli, aliwashukuru wananchi kwa mara nyingine kwa kumuamini na kumchagua, ambapo ameahidi kuwa kiongozi atakayewatumikia watu wote bila kubagua, na kwamba lengo lake ni kuhakikisha nchi ya tanzania inasonga mebel kimaendeleo.


Rais Magufuli pia kwenye hotuba yake pia akaeleza malalamiko aliyoyapokea kwa wananchi ambayo yeye anaona ni kero kwa wananchi, maeneo ambayo anasema ni lazima yashughulikiwe ipasavyo ili kuleta uaminifu kwa wananchi.



Kuhusu Uchumi rais Magufuli amesema kuwa serikali yake itakuwa ni serikali ya viwanda itakayosimamia sheria na kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unasimama kwa kujenga na kuendelea viwanda ili kutengeneza ajira zaidi.



katika hotuba yake pia, rais magufuli hakuacha kugusia suala la katiba mpya, ambapo amesema atahakikisha serikali yake inasimamia mchakato huo na kwamba safari hii utakamilika kwa wakati.


Rais Magufuli pia akagusia suala la muungano pamoja na hali ya kisiasa visiwani zanzibar ambapo amesema yeye ni muumini mkubwa wa muungano uliopo na kwamba anaamini mgogoro wa zanzibar uliojtokeza unatatuliwa kwa amani.


Kabla ya kuanza kwa hotuba yake bungeni, rais Magufuli alishuhudia vioja vya upinzani ambao walikuwa wakipiga kelele wakati viongozi wa zanzibar walipokuwa wakiingia bungeni bungeni, ambapo baadae spika wa bunge Job Ndugai alilazimika kutumia kiti chake kuwafukuza nje ya ukumbi wa bunge ili kupisha hotuba ya rais kuanza, jambo ambalo upinzani ulitii na kutoka nje.

OFISI YA ICGLR KUHAMISHWA KWA MUDA NCHINI ZAMBIA

Ofisi za Jumuiya ya nchi za maziwa makuu ICGLR yenye makao makuu mjini Bujumbura, Burundi, zitahamishia kwa muda shughuli zake mjini Lusaka, Zambia, kwa kile maofisa wake wanachosema kuwa ni hali tete ya kiusalama nchini humo.


ICGLR inasema kuwa kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Burundi, ofisi hiyo itahamishia kwa muda shughuli zake nchini Zambia, wakati mzozo wa nchi hiyo ukiendelea kutatuliwa na taasisi husika ikiwemi ICGLR, Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika.

MASHIRIKA 6 KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAOMBA KIKAO CHA DHARURA KUHUSU BURUNDI

Mashirika sita ambayo yote yamesajiliwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi wananchama, juma hili yamewasilisha hoja kwa spika wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakimtaka aitishe mkutano wa dharura wa wabunge na kutoa tamko kuhusu machafuko yanyoendelea kushuhudiwa nchini Burundi.

Mashirika hayo, yanatoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti na za haraka kushughulikia mzozo wa kisiasa na hali ya kibinadamu nchini Burundi, wakati huu mashirika hayo yakidai kuwa hali imezidi kuwa mbaya kwenye taifa hilo hukuviongozi wa Burundi wakikaidi maazimio kadhaa ya wakuu wa nchi za Afrika mashariki na Umoja wa Afrika.

Katika hoja yao, mashirika hayo yanataka kuwekewa vikwazo kwa viongozi wa Burundi, kupelekwa kwa waangalizi wa kimataifa pamoja na wanajeshi wa Umoja wa Afrika watakaolinda usalama wa raia.


Spika wa bunge la Afrika Mashariki, Dan Kidega amepokea hoja ya mashirika hayo, na kusema kuwa imekuja wakati muafaka kwakuwa hali inayoendelea kushuhudiwa nchini Burundi, haiwezi kuendelea kutazamwa bila ya kuchukuliwa hatua.


WAPIGANAJI 2 WADAIWA KUUWA NCHINI MALI KATIKA HOTELI WALIKOVAMIA





Taarifa za hivi punde zinaeleza kwamba washambuliaji wawili waliokuwa miongoni mwa watu waliosambulia na kuwateka watu katika Hoteli moja jijini Bamakao wameuawa wakati wa operesheni za uokozi.

Hayo yanajir wakati huu Wizara ya mambo ya ndani nchini Ufaransa, imethibitisha kupelekwa kwa kikosi maalumu cha wanajeshi wa kukabiliana na ugaidi na hali ya hatari nchini Mali, ambako wanamgambo wenye silaha wanashikilia mateka wat zaidi ya 150 kwenye hoteli moja mjini Bamako.

Zaidi ya wanajeshi 40 wa kikosi maalumu cha Ufaransa cha GIGN wanaelekea nchini Mali kutoa msaada kwa vikosi vya Mali kujaribu kuwaokoa mateka wanaoshikiliwa kwenye hoteli ya Radisson Blu, hoteli inayowahifadhi wageni na maofisa kadhaa wa Umoja wa Mataifa.

Hatua hii ya Ufaransa imekuja ikiwa ni saa chache tu zimepita toka wapiganaji wenye silaha kuvamia hoteli hiyo na kuwashikilia mateka wageni waliofikia kwenye hoteli hiyo.


KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...