Pages

mardi 5 août 2014

OBAMA AWATAKA VIONGOZI WA AFRIKA KUHESHIMU MUDA WA KUSALIA MADARAKANI


Serikali ya Marekani imewataka viongozi wa bara la Afrika kuheshimu tofauti za kisiasa zilizoko nchini mwao na kuwa na uvumilivu wa kisiasa ambao ndio nguzi kuu ya kuwa na demokrasia ya kweli katika kufikia mafanikio ya muda mrefu.

Rais Obama amewataka ma rais walipo madarakani bara Afrika kuheshimi muda waliopewa na katiba kukaa madarakani

Wito huu umetolewa wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya viongozi hao na rais Barack Obama, ambaye alitumia siku ya kwanza ya mkutano huu, kusisitiza masuala ya usalama, biashara na demokrasia kama msingi mkuu utakaoshuhudia nchi za Afrika zikipata maendeleo ya haraka.


Kuhusu biashara, rais Obama amesema kuwa haoni shida nchi ya China kuwa mwekezaji mkubwa barani Afrika lakini akaonya kuhusu uwekezaji unaofanywa na taifa hilo na kuwataka viongozi hao kuwa makini na rasilimali ambazo China imekuwa ikizilenga kwenye bara hilo.

MAPIGANO YACHACHA WAKATI MAZUNGUMZO YA AMANI YAKIZINDULIWA NCHINI SUDANI KUSINI



Mazungumzo ya amani kuhusu kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini yameanza Jumatatu ya wiki hii mjini Addis Ababa, huku kukishuhudiwa mapigano makali kwenye baadhi ya maeneo.

Wakati huu wajumbe wa mazungumzo haya wakiendelea kuwasili mjini Addis Ababa, makundi ya wapiganaji wenye silaha kwenye jimbo la Upper Nile wamekabiliana na wanajeshi walioasi kwa siku ya pili huku kukishuhidiwa mfanyakazi mmoja wa shirika la misaada akiuawa kutokana na mapigano haya.

Tume ya Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS imesema kwenye taarifa yake, kuwa inaguswa na hali ya kuendelea kushuhudiwa kuzorota kwa usalama nchini humo hasa kwenye miji ya Bunj na jimbo la Upper Nile ambako kuna zaidi ya wakimbizi laki 1 na elfu 25 wanaotoka Sudan.

Kwenye mazungumzo yaliyofunguliwa jana Jumatatu, wapatanishi wa mzozo huo wamewaonya viongozi wanaohasimiana kuhusu hatua ambazo zitachukuliwa dhidi yao iwapo mapigano hayatakomeshwa.

Jumuiya ya maendeleo ya nchi za Afrika mashariki IGAD ambayo ndio inayosimamia mazungumzo haya imeweka makataa ya hadi kufikia tarehe 10 ya mwezi huu kwa viongozi hawa kufikia makubaliano kuhusu serikali ya mpito.


Mazungumzo ya mwisho kati ya rais Salva kiir na aliyekuwa makamu wake wa rais Riek Machar yalikwama mwezi June mwaka huu baada ya kila upande kumtuhumu mwenzake kwa kukiuka mkataba waliotiliana saini.

lundi 4 août 2014

UMOJA WA MATAIFA WALAANI MAKOMBORA YA ISRAEL KATIKA SHULE LA UMOJA WA MATAIFA


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani makombora yaliyorushwa kwenye shule moja ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumapili na kusababisha mauaji ya raia wa kiPalestina wapatao kumi katika shambulio lililotekelezwa na askari wa Israeli.

Shambulio hilo limedhihirisha wazi ukiukwaji mwingine wa sheria za kimataifa ambapo pande zote mbili zililazimika kulinda usalama wa raia hao wa Palestina, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na majengo ya Umoja huo, amesema msemaji wa Katibu Mkuu katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Aidha, msemaji huyo amesisitiza kuwa lazima Makazi ya Umoja wa Mataifa yawe sehemu rasmi ya kukimbilia na si eneo la mapambano kama ilivyojitokeza mara kadhaa na kuwa lazima wahusika wa mashambulio hayo wachunguzwe na kuwajibishwa.

Katibu Mkuu Ban Ki Moon ameelezea kusononeshwa na ukiukwaji huo wa sheria za kimataifa na kubainisha kuwa serikali ya Israeli, licha ya kuwa imefahamishwa maeneo ambapo Umoja wa Mataifa umepiga kambi, askari wake wanaendelea kutekeleza vitendo vya uhalifu ambavyo Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa havikubaliki.


Tangu uvunjwaji wa Makubaliano ya kusitisha mashambulizi ya tarehe mosi Agosti, mamia ya raia wa Palestina tayari wameuwawa kutokana na mashambulizi hayo huku hali ya kibinadamu ikiendelea kuwa mbaya zaidi katika Ukanda wa Gaza, wakati ambapo Ban Ki-moon akitoa wito wake kwa pande zote kusitisha mapigano mara moja na kurejelea meza ya mazungumzo mjini Cairo, Misri.

MAWASILIANO YA SIM YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI JOHN KERRY YANASWA


Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika gazeti moja nchini Ujerumani, mawasiliano ya sim ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry yalifanyiwa udukuzi na nchi mbili ikiwemo Marekani.

Taarifa inakumbusha kashafa kama hiyo ya udukuzi wa mawasliano ya sim ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel na kituo cha Usalama wa taifa cha Marekani NSA, ambapo sasa vyombo vya habari nchini Ujerumani na hata kwenye mitandao ya kijamii.

Gazeti la kila wiki la Der Spiegel limeariku kuwa mawasiliano ya simu ya John kerry yalinaswa na idara ya usalama ya Israel katika kipindi chaote hiki cha majadiliano kati yake na Israel pamoja na Palestina ambayo yalifeli hivi karibuni .

Hata hivyo gazeti hilo la Spigiel halikuthibitisha iwapo mawasiliano ya kiongozi huyo wajuu nchini Marekani yalinaswa wakati huu wa mapigano mjini Gaza.

WAGENI WAENDELEA KUIKIMBIA LIBYA


Shuguhuli za uzinduzi wa bunge jipya nchini Libya zimeitishwa kufanyika jumatatu hii katika miji wa Tobrouk na upande wa chama cha wazalendo na tripoli na chama cha waislam wakati huu mauaji yakiendelea huku wageni na raia wa kawaida wakiendelea kuikimbia nchi hiyo kutokana na mapigano


katika mji mkuu Tripoli mapigano yaliozuka tangu Julay 13 yanaendelea kushuhudiwa huku watu 22 wakipoteza maisha na wengine 72 wakijeruhiwa katika mapigano ya mwishoni mwa juma baina ya makundi hasimu.


Takwimu zinaonyesha kuwa watu 124 ndiuo ambao wameuawa hadi sasa huku wengine zaidi ya mia tano wakijeruhiwa tangu kuanza kwa mapigano Julay 13 mjini Tripoli. Duru za kitabibu zimearifu kuwa huenda idadi ya waliopoteza maisha na kujeruhiwa ikawa kubwa zaidi kwani taarifa ya serikali haizingatii watu waliouawa na kujeruhiwa katika viunga vya jiji la Tripoli hususan katika mji wa Misrata.



SERIKALI YA KENYA YASISITIZA KUHUSU MPANGO WA KUWAPOKONYA ARDHI WANAOZIMILIKI KINYUME CHA SHERIA


Makamu wa rais wa Kenya, William Ruto ameendelea kusisitiza msimamo wa Serikali ya nchi hiyo kuhusu hatua waliyoitangaza juma moja lililopita ya kuwapokonya ardhi watu binafsi na makampuni yanayodaiwa kunyakua ardhi kwa nguvu kwenye mji wa Lamu pwania ya Kenya.

Kauli ya makamu wa rais, Ruto ameitoa akijibu hoja zinazotolewa na upinzani ambao unataka Serikali kuachana na mpango huo na kwamba utachukua hatua za kisheria kupinga uamuzi wa Serikali, msimamo ambao naibu wa rais Ruto anasema serikali yake haitorudi nyuma wala kutishika.

Makamu wa rais William Ruto anasema kuwa ni kitendo cha kustaajabisha na kilichopitwa na wakati kuona viongozi wa upinzani wanatumia muda mwingi kutoa vitisho dhidi ya Serikali na kuongeza kuwa vitisho hivi havisaidii.

Makamu wa rais Ruto, aanatoa kauli hii wakati ambapo hii leo tume ya ardhi nchini humo inatarajiwa kuanza kutekeleza agizo la rais Uhuru Kenyatta kuchukua ardhi inayokadiriwa kufikia hekari laki 5ambayo ilikuwa inamilikiwa kinyume cha sheria.

MKUTANO WA MAREKANI NA AFRIKA KUANZA LEO JIJI WASHINGTON


Rais wa Marekani, Barack Obama, hii leo anatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa kati yake na viongozi toka barani Afrika, mkutano uliolenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi yake na bara la Afrika.

Mkutano huu unafanyika wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo umasikini uliokithiri kwenye baadhi ya mataifa pamoja na janga la ugonjwa wa virusi vya Ebola ambao unatishia kusambaa hata kwenye mataifa ya Magharibi.

Rais Obama anatarajiwa kutumia mkutano huu kuwaeleza viongozi wa Afrika mkakati wa nchi yake katika kuimarisha biashara na nchi hizo, pamoja na namna itakavyoendelea kushirikiana na viongozi hao katika vita dhidi ya kuondoa umasiki na vitendo vya ugaidi.


Takariban viongozi kutoka nchi 50 ndio wanaohudhuria mkutno huo, ispokuwa pekee Jamhuri ya Afrika ya kati, Sudani, Eritrea na Zimbabwe ambazo hazikupewa mualiko, huku Liberia na Guinea zikiahirisha kutokana na kukabiliwa na gonjwa na Ebola.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...