Pages

vendredi 4 juillet 2014

WAHANGA WA MAUAJI YA AJALI YA SANGE KIVU YA KUSINI WAKUMBUKWA



Wahanga wa mauaji ya ajali ya moto uliotokana na kuteketea kwa lori la mafuta katika kijiji cha Sange Mkoa wa Kivu ya Kusini kwenye umbali wa kilometa takriban 70 na mji wa Biukavu, wamekumbukwa hapo jana. Ajali hiyo ilitokea miaka minne iliopita Julay 2 mwaka 2010 na kugharimu maisha ya watu zaidi ya 220.

Lori hilo la mafuta lilipata ajali katika kijiji hicho, ambapo mafuta yalivuka, na ndipo wananchi wa eneo hilo wakasogea kwa ajili ya kuchota mafuta, jamboo ambalo lilikuwa hatari sana kwako.

Baada ya muda kadhaa, lori hilo lililipuka na kusababisha maafa hayo makubwa ya wananchi na hata nyumba mali na vitu vilivyokuwa karibu vyote viliteketea. Rais wa taifa hilo Joseph Kabila siku mbili baada ya kutokea kwa ajali hiyo mbaya kuwahi kutokea alizuru katika eneo hilo na kutangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa.

jeudi 3 juillet 2014

VIONGOZI WA KIDINI JIJINI BANGUI WAYATUHUMU MAKUNDI YA WAASI KUWA CHANZO CHA USALAMA MDOGO


Maaskofu wa makanisa mbalimbali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wameyatuhumu makundi ya Seleka na Anti-Balaka kuwa chanzo cha kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama kwenye taifa hilo ambalo linakabiliwa na changamoto za kiusalama kufuatia mauaji ya kidini.

Viongozi hao wa kidini wanadai kuwa makundi kama vile ya Seleka, Anti-Balaka, na kundi la LRA la nchini Uganda yamekuwa yakijichukulia sheria mkononi kwa kutekeleza mauaji dhidi ya raia wanaowakamata.

Licha ya sehemu kubwa ya mauaji ya kudhibitiwa mjini Bangui, bado maeneo mengine ya nchi yemeendelea kushuhudia uwepo wa matukio ya unyanyasaji, mateso na mauji dhidi ya raia yanayofanywa na makundi haya, ambapo viongozi wa dini sasa wanataka makundi hayo kukomesha vitendo vya kikatili.

NAIBU BALOZI WA LIBYA NCHINI TANZANIA ISMAIL NWAIRAT AJIPIGA RISASE NA KUFA


Polisi nchini Tanzania imeanza uchunguzi kuhusu tukio la kujipiga risasi na kufa kwa kaimu balozi wa Libya nchini humo, Ismail Nwairat.

Kamishna wa kanda maalumu ya dar es Salaam, Suleimani Kova amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tayari kikosi cha askari wa upelelezi wameanza uchunguzi kuhusiana na tukio hili.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje nchini humo na mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Assa Mwambene, amesema balozi Nwairat alijipiga risasi mwenyewe akiwa kwenye chumba cha ofisi yake ambapo wafanyakazi wa ubalozi walilazimika kuvunja mlango ili kujua kilichotokea.

Ubalozi wa Libya nchini Tanzania umethibitisha kifo cha kaimu balozi wake na kuongeza kuwa mipango imeanza ya kuusafirisha mwili wake kwenda mjini Tripoli.

mercredi 2 juillet 2014

WANAJESHI WA MAREKANI WALIOTUMWA IRAQ KUPEWA UWEZO WA KUTUMIA NDEGE


Zaidi ya wanajeshi 500 wa Marekani waliotumwa nchini Iraq kulinda ubalozi wake wameelezwa kuwa watakuwa na uwezo wa kutumia ndege za kivita pamoja na zile zisizo na rubani kwaajili ya usalama mjini Baghdadi, Pentagon imesema.

Jumatatu ya wiki hii rais Barack Obama aliagiza kuongezwa kwa wanajeshi 200 zaidi nchini Iraq kuhakikisha maofisa wake wa Ubalozi wanakuwa salama wakati huu vikosi vya Serikali ya Iraq vikiendelea kukabiliwa na upinzani toka kwa waasi wa kiislamu wa ISIL.

Jeshi la Iraq limezidisha mashambulizi kwenye mji wa Tikrit alikozaliwa marehemu Saddam Hussein, mji ambao unakaliwa na wapiganaji hao ambao wametangaza utawala wa kiislamu.

WAKIMBIZI ZAIDI YA LAKI NANI WAKABILIWA NA KITISHO CHA NJAA

Antonio Guterres, mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na wakimbizi UNHCR

Zaidi ya wakimbizi wanaokadiriwa kufikia milioni moja barani Afrika, wanakabiliwa na baa la njaa wakati huu mashirika ya misaada ya kimataifa yakiendelea kukabiliana na changamoto ya kupata chakula cha msaada, Umoja wa Mataifa umesema.

Idadi hii imeongezeka kutokana na mashirika ya Umoja wa Mataifa kama vile UNHCR na shirika la mpango wa chakula duniani WFP kuanza kusitisha na kupunguza ugawaji wa chakula cha kila siku kwa maelefu ya wakimbizi duniani kutokana na kukabiliwa na uhaba wa chakula.

Mashirika haya yanasema kuwa ili kunusu hali kuwa mbaya zaidi yanahitaji kupata kiasi cha dola za Marekani milioni 225 ili kuwawezesha kupata chakula cha kila siku kwa wakimbizi na kuondoa kabisa mpango wao wa kupunguza ugawaji wa chakula.

MAWAZIRI WA NCHI 11 ZA UKANDA WA AFRIKA MAGHARIBI WAKUTANA KUJADILI KUHUSU MARADHI YA EBOLA



Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwenye nchi za Afrika Magharibi imefikia watu 467 na kuonya kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka.

Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusu mwenendo wa ugonjwa huo uliozikumba nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone, WHO inasema kuwa mpaka sasa wamebaini kuwepo kwa maambukizi mapya zaidi ya 759 kwenye ukanda huo hali inayoogofya kuhusu kuendelea kusambaa kwa virusi hivyo.

Idadi hii mpya inafanya kufikia kiwango cha asilimia 38 cha maambukizi mpaya ukilinganisha na kiwango cha asilimia 27 mwezi April mwaka huu wakati shirika la Afya duniani lilipotoa takwimu za mwisho kuonesha mwenendo wa ugonjwa huo ambao ulionekana kana kwamba umedhibitiwa.

Takwimu hizi zimetolewa wakati wa mkutano unaowakutanisha mawaziri wa afya toka mataifa kumi na moja ya ukanda wa Afrika Magharibi, mkutano unaofanyika nchini Ghana ukilenga kutafuta mbinu mpya za kukabiliana na maambukizi zaidi ya virusi vya Ebola.

Virusi vya Ugonjwa wa Ebola huweza kuambukizwa kwa njia ya hewa na kugusana hii ni kwa mujibu wa ripoti ya WHO, ambapo umetajwa kuwa miongoni mwa magonjwa hatari zaidi duniani, ugonjwa ambao mpaka sasa haujapatiwa tiba.

Mtu aupatapo ugonjwa huu huweza kuwa na homa kali, maumivu ya viungo, kutapika na kuhara na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi kwa baadhi ya ogani za mwili na kutokwa damu mfululizo.

ADF-NALU YAWEKEWA VIKWAZO NA UMOJA WA MATAIFA


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamuwa kuliwekea vikwazo kundi la waasi wa Uganda la ADF lililopiga kambi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Vikwazo hivyo vitawahusu viongozi wa kundi hilo kuwazuia kusafiri na kuhodhi fedha zao.

Vikwazo hivyo vilipendekezwa na mataifa ya Ufaransa, Marekani na Uingereza. ADF linaongozwa tangu mwaka 2007 na Jamil Mukulu ambaye alikuwa mkristo kabla ya kuslim kuwa muislam pamoja na kiongozi wa kijeshi Hood Lukwago ambao wamewekwa katika orodha ya viongozi wa makundi ya kigaidi na Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya.

Kundi la ADF ambalo pia linatambulika kwa jina la ADF-NALU linatuhumiwa kuwasajili watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 katika kundi hilo na kutekeleza mauaji lakini pia ubakaji dhidi ya kinamama na watoto na kuwashambulia wanajeshi wa kulinda amani nchini DRCongo Monusco.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...