Pages

mardi 3 février 2015

WATU 8 WASHIKILIWA KUHUSIKA NA KUWATUMA VIJANA NCHINI SYRIA NA IRAQ


Polisi nchini Ufaransa, inawashikilia watu 8 wanaotuhumiwa kujihusisha na mtandao wa kusafirisha vijana kwenda nchini Syria na Iraq kupigana vita sambamba na makundi ya kiislamu, wizara ya mambo ya ndani nchini humo imethibitisha.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve amewaambia waandishi wa habari kuwa watu hao wamekamatwa kutoka kwenye maeneo mbalimbali ya jiji la Paris na kusini mwa mji wa Lyon.

Kukamatwa kwa watu hawa kumekuja ikiwa imepita wiki moja tu, toka polisi nchini humo watangaze kuwakamata watu 5 kwenye mji mdogo wa Lunel kusini mwa nchi hiyo, eneo ambalo vijana wengine 20 wanadaiwa walisafiri kwenda nchini Syria.

Mwezi mmoja uliopita kwenye hotuba yake, waziri mkuu Manuel Valls alisema kuwa vijana kati ya 1400 ambao wanaishi Ufaransa wamejiunga ama walikuwa wamepanga kujiunga na makundi ya wapiganaji wa kiislamu nchini Syria na Iraq.

Nchi ya Ufaransa hivi karibuni imefanya msako maalumu uliolenga kuwakamata watu wenye uhusiano na makundi ya kiislamu, hatua inayokuja baada ya mwezi mmoja uliopita vijana wawili kutekeleza shambulio jijini Paris na kuua watu 17.

MAANDAMANO YA WAANDISHI WA HABARI NCHINI BURUNDI YATAMATIKA BILA VURUGU YOYOTE


Zaidi ya waandishi wa habari 150 pamoja na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini Burundi, hii leo wameandamana kushinikiza kuachiwa huru kwa Bob Rugurika mkurugenzi wa kituo cha redio ya RPA anayeshikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watawa watatu raia wa Italia.

Bob Rugurika mkurugenzi wa kituo cha redio cha RPA alikamatwa kati kati ya mwezi January mwaka huu saa chache baada ya kituo chake kurusha mahojiano ya mtu mmoja aliyedai kuwa ni miongoni mwa watu waliohusika na mauaji ya watawa hao.

Waandamanaji hao walikusanyika nje ya majengo ya mahakama kuu mjini Bujumbura, Burundi walikaidi amri ya meya wa jiji aliyewataka wasifanye maandamano hayo, lakini katika hatua ya kushangaza polisi waliwaacha waandamanaji hao wakusanyike.

Patrick Nduwimana mmoja wa waandishi wa habari na mwanachama wa muungano wa chama cha waandishi wa habari nchini humo, amesema kuwa lengo la maandamano yao ni kuendelea kudai haki na kushinikiza kuachiwa kwa Rugurika.

Kukamatwa kwa mkurugenzi wa kituo hiki kumeendelea kuzusha hofu ya kiusalama hasa kwa waandishi wa habari na wanaharakati ambao wameendelea kukamatwa na vyombo vya dola nchini humo kwa tuhuma mbalimbali, hali ambayo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa ni kutaka kuminya uhuru wa watu kutoa maoni yao wakati huu nchi hiyo ikijiandaa kufanya uchaguzi wake mkuu.

lundi 2 février 2015

JESHI LA UGANDA LAFANYA UCHUNGUZI KUHUSU VINASABA VYA MTU ANAESHUKIWA KUWA OKT ODHIAMBO


Jeshi la Uganda limefahamisha kwamba litafanya uchunguzi kupitia vinasaba vya mwili wa mtu aliezikwa hivi karibuni kubaini iwapo ni kiongozi numba mbili wa kundi la waasi wa Lord Resistence Army LRA anedaiwa kuawa mwaka mmoja uliopita.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Uganda Paddy Ankunda viongozi wa Uganda wanahisi kuwa wamelipata kaburi alipozikwa Okt Odhiambo mtu wa karibu sana na kiongozi wa LRA Joseph Kony.

Pandi akunda amesema tayari vinasaba hivyo wamevipata, na sasa wanafanya uchunguzi wa DNA ili kubaini iwapo kweli ni kiongozi huyo. Hata hivyo msemaji huyo wa majeshi ya Uganda amaketaa kusema ni eneo gani walipogundua kaburi hilo linalo sadikiwa ndiko alikozikwa mmoja kati ya viongozi wa kundi la RLA.

Uganda na Marekani zilibaini mwezi Februari mwaka jana uwezekanao wa kutokea kwa kifo cha Odhiambo ambae alikuw amiongoni mwa wanaotafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC kutokana na vitendo vya ujunjifu wa haki za binadamu vinavyotekelezwa na wapiganaji wa kundi hilo. Iwapo itathitishwa kifo cha kiongozi huyo, basi Joseph Kony atakuwa ni kiongozi pekee wa kundi hilo ambae bado anatafutwa.


SERIKALI MPYA YA TUNISIA YATANGAZWA YASUBIRI BARAKA ZA BUNGE JUMANNE


Waziri mkuu wa Tunisia Habib Essid ametangaza serikali yake ya muungano iliowajumuisha wajumbe wa chama cha Ennahda na ambayo asilimiua kubwa ni wajumbe kutoka chama kilichoshinda viti vingi bungeni cga Nidaa Tunes.
Serikali hiyo mpya ya kwanza kabisa tangu kufanyika kwa uchsguzi mkuu wa bunge na wa rais mwezi Ocotba mwaka jana, itahitaji baraka kutoka bungeni katika kikao kinachotarajiwa kufanyika hapo kesho.
Mbali na wafuasi wa chama cha Nidaa Tunes chenye wajumbe 86 na kile cha Ennahda chenye wajumbe 69, vyama vingine viwili vimewakilishwa bungeni ikiwa ni pamoja na kile cha UPL chenye wajumbe 16 pamoja na kile cha Liberal chenye wajumbe 8 bungeni. Hivyo serikali inaimani ya kupt uungwji mkono kutoka kwa wabungr 179 dhidi ya 217 wanaounda bunge la nchi hiyo.

NDOTO YA KUELEKEA IKULU YAZIMWA NA SASA MAHAKAMANI


Kesi ya kumiliki danguro na kunua wasichana wa umri mdogo kushiriki nao kimapenzi dhidi ya mkuu wa zamani wa shirika la fedha duniani IMF, Dominique Strauss-Kahn imeanza kusikilizwa tena hii leo kwenye mahakama moja mjini Lille.

Strauss-Kahn, mchumi mwenye umri wa miaka 65 hivi sasa amepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya jiji la Lille akituhumiwa kuwa kiini cha kundi la watu wenye fedha wanaonunua wasichana kwaajili ya kuwatumia kwenye sherehe zao mjini Brussels, Paris na Washington.

Kesi hii inayotarajiwa kudumu kwa majuma matatu, itashuhudia kiongozi huyu ambaye wakati fulani alitajwa kuwa kinara wa mbio za urais nchini Ufaransa, akisimama kizimbani sambamba na mameneja wa hoteli, polisi, freemasons pamoja na kaka yake anayefahamika kwa jina la Dodo the Pimp.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa iwapo Dominique Strauss-Kahn atapatikana na hatia ya makosa yanayomkabili huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 10 au kulipa faini inayokadiriwa kufikia dola za Marekani milioni 1 na laki 7.

Awali mwendesha mashtaka kwenye kesi hii alitaka kufutwa kwa kesi hiyo kwa kile alichodai kukosekana kwa ushahidi wa kutosha dhidi yake, ombo ambalo hata hivyo mahakama ililikataa na kuagiza kesi hiyo kuendelea.

HUKUMU YA KIFO DHIDI YA WATU 183 YATHIBITISHWA NCHINI MISRI


Mahakama moja nchini Misri imethibitisha hukumu ya adhabu ya kifo kwa zaidi ya raia 183 waliopatikana na hatia ya mauaji ya polisi 13 jirani na mji wa Cairo August mwaka 2013.

Hukumu hii inafuatia uamuzi wa mahakama hiyo iliyoufanya mwezi December mwaka jana ambapo iliwakuta na hatia zaidi ya raia 188 kwa tuhuma za mauaji ya polisi, ambapo kwenye hukumu ya hii leo, mahakama hiyo imewaachia huru watuhumiwa wawili huku mwingine akihukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela.

Kufutiwa mashtaka kwa watuhumiwa hawa wawili kumekuja baada ya mahakama kubaini kuwa watuhumiwa hao wamefariki, ambapo kuthibitishwa kwa hukumu hii kumetokana na uamuzi wa mufti mkuu wa nchi hiyo kukubaliana na uamuzi wa awali wa mahakama.

Watuhumiwa hawa ambao 143 kati yao walikuwa wanashikiliwa na polisi, walipatikana na hatia ya kuhusika na vurugu za mwezi August mwaka 2013 ambapo wanadaiwa kuwa walivamia kituo cha polisi cha Kerdassa na kuua askari 13 wa kituo hicho.

Toka kuangushwa madarakani kwa utawala wa Mohamed Morsi mwezi July mwaka 2013, watu wanaokadiriwa kufikia elfu 1 na 400 wameuawa na polisi wakati wa maandamano.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameelezwa kuguswa na hukumu hizi ambazo zimekuwa zikitolewa na mahakama yakidai kuwa nyingine zimechochewa kisiasa.

HRW YAONYA KUWA MASHAMBULIZI DHIDI YA FDLR HAYAWEZI KULITOKOMEZA FDLR



Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Right Watch limesema kuwa nguvu za kijeshi pekee hazitatosha kumaliza uasi wa kundi la waasi wa kihutu wa Rwanda wa FDLR ambalo wapiganaji wake wameendelea kujificha msituni licha ya kutakiwa kujisalimisha.

Kwenye taarifa yake, Human Right inasema kuwa, mbali na kutumika kwa nguvu za kijeshi dhidi ya wapiganaji hao, hatua nyingine pia zinapaswa kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwasaka viongozi wa kundi hilo, kubaini maeneo walikojificha na kuwashawishi wapiganaji wake kuendelea kujisalimisha.

Ida Sawyer ni mmoja wa viongozi wa shirika la Human Right Watch kwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, kauli za viongozi haipashwaji kusalia pekee kwenye mashambulizi, lazima mbinu nyingine zitumike.


Kauli hii ya Human Right Watch inatolewa wakati huu ambapo mwishoni mwa juma jeshi la Serikali ya DRC tayari limeanza operesheni maalumu ya kuwasaka na kuwasambaratisha wapiganaji wa FDLR ambao walikataa kujisalimisha.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...