Shirika
la afya duniani WHO linasema kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na
virusi vya ugonjwa wa Ebola kwenye nchi za Afrika Magharibi imefikia
watu 467 na kuonya kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka.
Kwenye
taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusu mwenendo wa ugonjwa huo
uliozikumba nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone, WHO inasema kuwa
mpaka sasa wamebaini kuwepo kwa maambukizi mapya zaidi ya 759 kwenye
ukanda huo hali inayoogofya kuhusu kuendelea kusambaa kwa virusi
hivyo.
Idadi
hii mpya inafanya kufikia kiwango cha asilimia 38 cha maambukizi
mpaya ukilinganisha na kiwango cha asilimia 27 mwezi April mwaka huu
wakati shirika la Afya duniani lilipotoa takwimu za mwisho kuonesha
mwenendo wa ugonjwa huo ambao ulionekana kana kwamba umedhibitiwa.
Takwimu
hizi zimetolewa wakati wa mkutano unaowakutanisha mawaziri wa afya
toka mataifa kumi na moja ya ukanda wa Afrika Magharibi, mkutano
unaofanyika nchini Ghana ukilenga kutafuta mbinu mpya za kukabiliana
na maambukizi zaidi ya virusi vya Ebola.
Virusi
vya Ugonjwa wa Ebola huweza kuambukizwa kwa njia ya hewa na kugusana
hii ni kwa mujibu wa ripoti ya WHO, ambapo umetajwa kuwa miongoni mwa
magonjwa hatari zaidi duniani, ugonjwa ambao mpaka sasa haujapatiwa
tiba.
Mtu
aupatapo ugonjwa huu huweza kuwa na homa kali, maumivu ya viungo,
kutapika na kuhara na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi kwa
baadhi ya ogani za mwili na kutokwa damu mfululizo.