Pages

lundi 12 mai 2014

WAHAMIAJI HARAMU KUTOKA AFRIKA MAGHARIBI WAPOTEZA MAISHA HUKO LIBYA


Takriban wahamiaji haramu 36 wamepoteza maisha na wengine 42 hawajulikani walipo baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya libya.
Duru kutoka polisi nchini Libya zimearifu kuwa Boti hilo limezama kwenye umbali wa kilometa 4 katika pwani ya Garabuli, kilometa 50 mashariki mwa Libya, na watu 52 wameokolewa na miili 36 imeokotwa huku watu wengine 42 hawajulikani walipo.
Msemaji wa kikosi cha majiji Kanali Ayoub Kassem amesema wahamiaji hao ni kutoka katika mataifa mbalimbali barani Afrika akiwemo mama mjamzito miongozni mwa walipoteza maisha.
Kanali Ayoub Kassem ameongeza kuwa Mashahidi wanasema boti hilo lilikuwa limebabe watu 130 kutoka katika mataifa ya Mali, Sénégal, Gambia, Cameroun, Burkina Faso, na mataifa mengine barani Afrika.

PICHA YA KWANZA YA VIDEO YA WASICHANA WALIOTEKWA NCHINI NIGERIA YAONYESHWA NA BOKO HARAM



Kiongozi wa kundi la Boko Haram Aboubakar Shekau ameweka wazi mkanda wa video unaowanyesha wasichana zaidi ya mia moja ambao wanashukiwa kuwa wanafunzi waliotekwa hivi karibuni na kundi hilo kaskazini mwa Nigeria na kuthibitisha kwa wote wamesilimu na kuwa waislam.

Katika mkanda huo wenye dakika 27, Abubakar Shekau ameomba wafungwa wote kutoka kundi la Boko Haram waachiwe huru kabla ya kuwaacha wasichana hao ambao ametishia kuwaoza kwa bei kubwa, huku wasichana hao wakionekana wote wamevaa hijabu na kuendelea kusoma Coran katika hali tulivu.

Imekuwa vigumu kujuwa eneo walipo wasichana hao. Jumla wasichana 276 ndio wanaoshikiliwa na kundi hilo tangu April 14 huko Chibok katiks Jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria ambako kunaeshi wa kristo wengi. Polisi inasema wasichana 223 hawajulikani walipo.

Mkandao huo wa video unawaonyesha takriban wasichana 130 waliovalia hijabu nyeusi na yenye rangi ya kijivu, wakifunika nyuso zao wakikaa chini eneo linalo fanana na msituni huku wakisoma Coran.

Hadi sasa inekuwa vigumu kujuwa ni wapi walipo wasichana hao, licha ya jumuiya ya kimataifa kutuma wataalam wa ujasusi kwa ajili ya kuwasaka walipo.

vendredi 9 mai 2014

SALVA KIIR NA RIEK MACHAR WAKAUTANA JIJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi ambaye pia alikuwa makamu wa rais Riek Machar wanakutana kwa mara ya kwanza ana kwa ana jijini Addis Ababa Ethiopia, kujaribu kupata mwafaka wa kumaliza machafuko yanayoendelea katika taifa lao kwa miezi mitano sasa.

 Kukutana kwa viongozi hawa chini ya wasuluhishi wa mgogoro huo kutoka Mataifa ya Afrika Mashariki IGAD wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn kumewapa wananchi wa Sudan Kusini matumaini ya kurejea kwa usalama katika taifa lao.

OSCAR PISTORIUS AUZA NYUMBA YAKE

Oscar Pistorius mwanariadha mlemavu kutoka nchini Afrika Kusini anayetuhumiwa kumuua mpenzi wake kwa kumpiga risasi mwaka uliopita, amelazimika kuuza nyumba yake aliikomuulia mpenzi wake ili kuwalipa mawakili wake. 

Imebainika kuwa Pistorious ameuza nyumba yake Dola laki nne na elfu themanini, ili kuweza a kuwalipa mawakili wake dola elfu tisa kila siku.


Kesi dhidi yake imekuwa ikiendelea kwa wiki kadhaa sasa na amekanusha kumuua mpenzi wake Reeva Stenkamp kwa makusudi. Tangu kuanza kwa kesi hii, Pistorius hajajihusisha na shughuli za zaidi ambazo zilikuwa zinampa kipato cha Dola laki tano kila mwaka.

ZIARA YA RAIS WA UFARANSA FRANCOIS HOLLANDE NCHINI UJERUMANI

Rais wa Ufaransa Francpis Hollande ameelekea nchini Ujerumani jioni hii katika mji wa Rügen na Stralsund karibu na bahari ya Baltique katika ngome ya Angela Merkel. Mzozo wa Ukraine, na siasa, Uchumi ndio maswali yanayotarajiwa kugubikwa mazungumzo hayo.

Mualiko wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa rais wa Ufaransa Francois Hollande katika eneo hilo la ufukwe wa bahari ya baltik ambako ni ngome ya Merkel, ni ishara ya kudumisha uaminifu wa uhusiano wa wakrito wa kidemokrasia na wa socialist baada kuaonekana kuwa mgumu hapo mwanzoni.

Kansela Merkel anapongeza hali ya maelewano ya ikulu ya Ufaransa na ahadi ya jukumu la Manuel Valls hali ambayo utawala wa Ujerumani unaonakuwa ni hatua nzuri na yenye mwelekeo sahihi.

Muungano mpya wa kisiasa unaovikutanisha vyama vya Sociodemokrate na wa liberali unaruhusu kupanua wigo wa kisiasa na kuonyesha nia ya kushirikiana kuhusu swala la mzozo wa Ukraine. Paris na Berlin wanaamini kwamba ni fursa nzuri ya kushirikiana kwa muda mrefu katika swala la vikwazo dhidi ya Urusi.

Hakuna kinachotarajiwa kuzungumziwa kuhusu kampuni ya Alstom, lakini mawaziri wa Ujerumani wa Uchumi Arnaud Montebourg na Siegmar Gabriel watakutana ili kuzungumzia swala hilo ambapo mfanyabiashar Siemens ameonyesha nia ya kununuwa kampuni hiyo.



BERLUSCONI AANZA KUTEKELEZA ADHABU ALIZOPEWA NA MAHAKAMA

Waziri mkuu wa zamani nchini Italie Sivlio Berlusconi ameanza leo Mei 9 kutekeleza adhabu aliopewa na mahakama ya kufanya kazi za Umma katika Hospitali moja ya kituo cha Cesano Boscone karibu na jiji la Milan. Ebby Shaban Abdallah na Maelezo zaidi.


Bilionea huyo wa Italia alihukumiwa na mahakama ya Italia kifungo cha mwaka mmoja jela kabla ya kusamehewa kifungo cha miaka minne na kutakiwa kufanya kazi za Umma, kufuatia tuhuma za kuhusika katika kashfa ya rushwa.

Berlusconi ameonekana mapema leo asubihi katika kituo cha Sacra Famiglia kabla ya kuingia katika majengo ya hospital ya San Pietro kwa ajili ya kutekeleza kazi za Umma kama alivyoagizwa na mahakama. Berlusconi amejizuia kuzungumza na Waandishi wa habari waliokuwepo katika eneo hilo.

Licha ya ulinzi mkali uliokuwa umedhaminiwa katika eneo hilo mwanaharakati mmoja alifaulu kupenya na kulaani hatuwa hiyo. Wafanyazi wengi nchini Italia wangpenda kumuona kiongozi huyo akizuiliwa katika jela kuu la San Vittore, jela la mji wa Milan badala ya kumpa adhabu hiyo ambayo wanasema ni ndogo.


Hukumu hiyo ilisababisha Berlusconi kufukuzwa kwenye baraza la seneti na kumzuia kupiga kura au kuwania uchaguzi

jeudi 8 mai 2014

CHAMA TAWALA CHA ANC KINAONGOZA KATIKA UCHAGUZI ULIOFANYIKA JANA

Nchini Afrika Kusini, chama tawala cha ANC kinaongoza wakati huu kura zikiendelea kuhesabiwa baada ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu hapo jana.

Matokeo ya hivi punde yanaonesha kuwa chama cha ANC kinaongoza kwa asilimia sitini , huku kile cha Democratic Aliance kikiwa na asilimia 22 wakati chama cha aliyekuwa kiongozi wa vijana katika chama cha ANC Julius Malema cha Economic Freedom Fighters, kikiwa cha tatu.

Ilikuwa imetabiriwa kuwa licha ya viongozi wa chama cha ANC kukumbukwa na kashhfa za ufisadi kitapata ushindi na kile cha Democratic Alliance kitaongeza viti vyake bungeni.

Baada ya wabunge 400 kuchaguliwa watakuwa na jukumu la kumchagua rais wa nchi hiyo.

HALI BADO SI SHWARI NCHINI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI


Wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya kati wakiyatoroka makwao
Watu 13 wamepoteza maisha wakiwemo raia wawili wa kawaida katika mapigano ya makundi ya waasi wa kundi la Seleka linaloundwa na waumini wa kiislam pamoja na waasi wa kundi la Anti Balaka wa Kikristo katika mji wa Kaga Bandoro kwenye umbali wa kilometa 300 kaskazini mwa Bangui duru za jeshi la Umoja wa Afrika nchini humo zimethibitisha.

Duru hizo zimesema mapigano makali yameripotiwa wakati kundi la Anti Balaka lilipo washambulia wapiganaji wa Seleka na ndipo kusababisha mapigano makali yaliopelekea wananchi kukimbilia katika kanisa la Kikatoliki ambalo sasa limewapokea wakimbizi elfu kumi na tatu.

Mashahidi waliokimbilia katika kanisa hilo wanasema kundi la waasi zamani la seleka linataka wa Anti Balaka waliokimbilia kanisani hapo wajisalimisha la sivyo watashambulia kanisa hilo na kuwauwa watu waote waliopo hapo.

UFARANSA KUTUMA WANAJESHI ELFU TATU KATIKA UKANDA WA SAHEL

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian

Ufaransa imetangaza kuwa itawatuma wanajeshi wake 300 kupambana na wapiganaji wa makundi ya kiislam katika eneo kubwa la ukanda wa Sahel. Wakati huu askari mmoja wa Ufaransa akiarifiwa kupoteza maisha kaskazini mwa Mali.

akifahamisha taarifa hii, waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian amesema jukumu lao ni kuwafuata wanamgambo wa makundi ya kiislam walikojificha katika maeneo ya kaskazini mwa Mali, Niger na Tchad na sasa wanapanga kikosi cha wanajeshi mia tatu wataopelekwa katika maeneo hayo.

Hata hivyo waziri Ledrian amesema Ufaransa ilikuwa inalekea katika mchakato wa kuhitimisha vita huko kaskazini mwa Mali, lakini askari elfu moja watabaki katika eneo la Gao kaskazini mashariki mwa nchi hiyo

Hayo yanajiri wakati huu askari mmoja wa Ufaransa akiripotiwa kupoteza maisha katika baada ya kukanyaga bomu la kutegwa ardhini lililotegwa na wapiganaji wa makundi ya kiislam.

Viongozi wa Ufransa kuanzia kwa rais francois Hollande wamezipeleka salam za rambi rambi kwa familia ya mwanajeshi huyo na kusema kwamba amekufa kishijaa wakati akipigania usalama wa dunia.

Ufanrasa ilianzisha operesheni Serval Januari mwaka 2013 kuwasaidia wanajesi wa Mali kupambana na makundi ya kiislam yaliokuwa yameteka miji ya kaskazini na kuayasambaratisha.


VIONGOZI MBALIMBALI DUNIANI WAUNGANA NA TAIFA LA NIGERIA KUWATAFUTA WASICHANA WALIOTEKWA NA BOKO HARAM



Kiongozi wa kanisa katoliki Duniani Papa Francis ni miongoni mwa viongozi duniani waliungana na Nigeria katika kazi hii ya kutekwa kwa wasichana zaidi ya mia mbili 
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema kutekwa nyara kwa wasichana zaidi ya mia mbili na kundi la kigaidi la Boko Haram majuma mawili yaliyopita, itakuwa mwisho wa kundi hilo nchini humo.

Rais Jonathan ameongeza kuwa jitihada zinazofanywa na Jumuiya ya Kimataifa kuwaokoa wasichana hao walio mikononi mwa Boko Haram zitazaa matunda na wanagmabo hao hawatakuwa pa kukimbilia.

Mataifa ya Marekani, Uingereza, Ufaransa na China yanetuma watalaam wake nchini humo kusaidia kuwaokoa wasichana hao wa shule ambao kundi hilo linasema litawauza.

Rais Jonathan amewashukuru wageni waliohudhuria mkutano wa Kimataifa wa kiuchumi unaomalizika kesho jijini Abuja, kwa kile alichokisema ikiwa hawangehudhuria kwa sababu ya uongo, wanagmabo hao wangejiona washindi.

mardi 6 mai 2014

IDADI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA HUKO KENYA BAADA YA KUNYWA POMBE HARAMU YAFIKIA SITINI



Idadi ya watu walipoteza maisha baada ya kunywa pombe haramu nchini Kenya katika kijiji cha Kawamwaki karibu na mji wa Limuru baada ya kunywa pombe haramu ya kienyeji iliyotiwa sumu.

Naibu Kamishena wa Kaunti ya Limuru Kang’ethe Thuku amethibitsiba kutokea kwa mauaji hayon na kusema kuwa huenda pombe hiyo ilitiwa kemikali aina ya Methanol.

Mbali na Limuru, watu wengine 18 wanahofiwa kupoteza maisha pia baada ya kunywa hiyo na wengine zaidi ya arobaini wamelazwa Hospitalini.

Si mara ya kwanza watu kupoteza maisha nchini humo kwa kunywa pombe haramu na hata wengine wamekuwa wakibaki vipofu kwa kubugia pombe hiyo.

RAIS WA UFARANSA FRANCOIS HOLLANDE AZIDI KUPOTEZA UMAHARUFU MIAKA MIWILI TANGU KUKALIA KITI CHA URAIS


Ni mwaka wa pili tangu rais wa Ufaransa Francois Hollande alipochaguliwa kuwa kiongozi wa nchi hiyo. Na tangu kukalia kiti cha Urais Francois Hollande amepoteza umaharufu mkubwa kufuatia kutotekeleza ahadi alizozitowa wakati akiomba kura kwa wananchi.

Rais Hollande amewaambia Wafaransa kuwa licha ya uongozi wake wa miaka miwili kukumbukwa na misukusuko ya hapa na pale, anafanya kila kilicho ndano ya uwezo wake kulete mabadiliko yatakayoimarisha maisha ya wananchi wa taifa hilo.

Kura za maoni zinaonesha kuwa umaarufu wa kiongozi huo wa chama cha Kisosolisti umepungua mno ikilinhganiswa na rais wa zamani Nicolas Sarkozy aliyekuwa maarufu wakati kama huu wakati wa uongozi wake.

Rais Hollande ameahidi kuimarisha uchumi wa taifa hilo na kuunda nafasi zaidi za kazi wakati wa uongozi wake.

lundi 5 mai 2014

KESI YA PISTORIUS YARUDI TENA KURINDIMA

Kesi ya Bingwa wa mbio za dunia za walemuavu Oscar Pistorius dhidi ya mchumba wake Reeve Steenkamps imerudi tena kurindima leo, ambapo mashahidi wawili waliokuwepo baada ya tukio hilo lililotokea Februri mwaka 2013, wamesema Pistorius alivunjika nguvu baada ya kugunduwa kuwa amemuuwa mpenzi wake. 

Johan Stander mmoja kati ya watu waliopigiwa sim na Pistorius, ameiambia mahakama kwamba alipokea sim ya Pistorius majira ya saa tisa alfajiri akimnasihi kuja kumsaidia kwani amempiga risase Reeve akihisi kuwa ni jambazi.

Baada ya kuwasili katika eneo la tukio akiwa na binti yake Carice Viljoen, Johan Stander amesema walimkuta Pistorius akishuka ngazi huku akiwa na mpenzi wake mikononi akiomba msaada wa kumpeleka mpenzi wake Hospitalini huku machozi yakibubujika, akilia na kuonekana mwenye huzuni kubwa.

Naye binti wa Johan Stander alishindwa kuendelea kutowa ushahidi na kujikuta akimwaga machozi na kueleza kwamba alihisi huenda Pistorius atajipa sumu wakati alipokwenda kutafuta kitambulisho cha Reeve ilikutambuwa wakati wa huduma ya kwanza.

Kinyuma na ushaihidi mwingine, ambao unasema sauti ya mwanamke ambaye huenda alikuwa Reeve akilalamika mbele ya muuaji, Carice Viljoen amesema alisikia sauti ya ambayo anauhakika kwamba ni ya mwanaume.

Oscar Pistorius mwenye umri wa miaka 27 anaweza kufungwa kifungo cha miaka 25 iwapo atakutwa na hatia ya kumuuwa mpenzi wake Reeve Steenkamp mwanamitindo.

BOKO HARAM WAKIRI KUHUSIKA NA UTEKAJI WA WASICHANA 220 MAJUMA MAWILI YALIOPITA

wakati rais wa Nigeria Goodluck Jonhattan akitowa wito kwa serikali ya Marekani na mataifa mengine kumsaidia kutatua hali ya usalama nchini Mwake, kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakr Shekau ametowa mkanda wa Video ambao anajigamba kuwa kundi lake ndilo lililohusika na utekaji nyara wa wasichana 220 katika wiki mbili zilizopita.

Hayo yanajiri wakati huu hasira ikipanda miongoni mwa wananchi wa Nigeria wakiilaumu serikali ya nchi yako kutofanya lolote katika juhudi za kuwatafuta watoto hao waliotekwa nyara tangu April 14.

Rais Goodluck ameahidi kuzidisha juhudi za kuwatafuta wasichana hao wakati huu kukiandaliwa mkutano wa kimataifa jijini Lagos chini ya Ulinzi mkali baada ya kutokea mashambulio mawili mjini hapo.


MAREKANI YAMTAKA RAIS KABILA KUHESHIMU KATIBA YA NCHI YAKE


Serikali ya Marekani imemshawishi rais wa DRCongo Joseph Kabila Kabange kuondoka madarakani ifikapo mwaka 2016 kama inavyoagiza katiba ya nchi hiyo na imejikubalisha kutowa kitita kinachokadiriwa kufikia dola za Marekani Milioni thalathini zai ziada katika kuunga mkono mchakatoi wa uchaguzi nchini humo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ambaye yu ziarani baranai Afrika kwa lengo la kutatua mizozo iliokita mizizi katika mataifa ya Afrika Hususan nchini Sudani Kusini na eneo la ukanda wa Maziwa makuu amesema nchi yake inaimani kwamba katiba ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo itaheshimiwa.

Wakati huo huo mjumbe wa marekani katika Ukanda wa maziwa makuu Russell Feingold ameweka wazi kwamba hawataki kuona rais Kabila anafanya mabadiliko ya katiba au kuwania tena urais kwa muhula wa tatu.

vendredi 2 mai 2014

ALEXIS SINDUHIJE AKANUSHA TAARIFA ZA KUKAMATWA BALI AZUILIWA KUINGIA MJINI BRUSSELS


Kiongozi wa chama cha upinzani cha MSD nchini Burundi Alexis Sinduhije amezuiliwa tangu jana asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brusels nchini Ubelgiji wakati alikua akitokea jijini Nairobi nchini Kenya.

Viongozi wa Burundi walitoa mwishoni mwa mwezi machi hati ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa upinzani, akituhumiwa kuanzisha vuguvugu dhidi ya utawala wa Pierre Nkurunziza.

Alexis Sinduhije anatuhumiwa na serikali ya Bujumbura kwamba alihusika na machafuko yaliyotokea mwezi machi kati ya wafuasi wake na polisi.

Taarifa zaidi zinaarifu kwamba serikali ya Burundi kupitia ubalozi wake jiji Brussels umewasilisha hati ya kukamatwa kwa mwanasiasa huyo. Jambo ambalo serikali ya Ubelgiji inasema haiwezi kutekeleza amri ya kurejeshwa kwa raia yeyote kwa sababu za kisiasa.

RAIS WA SUDANI KUSINI SALVA KIIR AKUBALI KUKUTANA ANA KWA ANA NA MPIZANI WAKE RIEK MACHAR

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amefanya ziara ya kushtukiza nchini Sudani Kusini ili kulazimisha pande mbili zinazo zozana nchini humo kusitisha mapigano katika nchi hiyo inayo kabiliwa na kitisho cha njaa na kutokea kwa mauaji ya kimbari.

Hizi ni juhudi za hali ya juu za kidiplomasia kujaribu kuzishwawishi pande mbili husika na mzozo huo angalau kusitisha mapigano yalioanza kushuhudiwa Desemba 15 mwaka jana katika taifa hilo changa kuliko yote barani Afrika.

Baada ya kukutana na rais salva Kiir, hatimyae amekubali kukutana ana kwa ana na mpinzani wake Riek Machar kiongozi wa waasi walioiteka miji kadhaa yenye utajiri wa mafuta.


John Kerry amewataka waasi na wanajeshi wa serikali kuheshimu makubaliano ya kusitishwa vita yaliofikiwa Januari mwaka huu na ambayo hayajawahi kuheshimiwa na kuacha kuwashambulia raia wasiokuwa na hatia.

VIONGOZI WA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI WAZINDUWA MFUMO WA PAMOJA WA KIELEKTRONIKI

Viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki wamekutana jijini Nairobi nchini Kenya Ijumaa hii na kuzindua mfumo wa pamoja wa Kieletroniki kurahihisha usafirishaji wa bidhaa na kufanya biashara baina ya Mataifa hayo.

Hii inaamanisha kuwa wafanyibiashara kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Tanzania , Rwanda, Burundi na Sudan Kusini wataweza kuwasilisha nyaraka zao ikiwemo vibali vya kufanya biashara,malipo mbali,bali katika eneo moja kwa njia ya eletroniki.

Akizindua mfumo huo rais wa Rwanda Paul Kagame, amesema mfumo huu utaiharakisha biashara na shirikish la Afrika Mashariki.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta naye amesema mfumo huu ikia utatekelezwa ipasavyo, ndoto ya shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki litatimia.

Tanzania iliwakilishwa katika mkutano huo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, huku Burundi ikiwalishwa na Makamu wa pili wa rais Gervais Rufyikiri.



KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...