Pages

lundi 2 février 2015

PETER GRESTE AMEAPA KUENDELEA KUWAPIGANIA WENZAKE SAA CHACHE BAADA YA KUACHIWA HURU


Saa chache baada ya kuachiwa huru na mamlaka nchini Misri, mwandishi wa habari wa kituo cha kimataifa cha Aljazeera raia wa Australia, Peter Greste ameapa kuendelea kuwapigania waandishi wenzake ambao bado wanashikiliwa gerezani kwa tuhuma za uhaini.
Familia yake inasema kuwa, Peter ameahidi kuhakikisha kuwa anaendelea kusimama na wenzake waliosalia gerezani akisisitiza kuwa hawana hatia kama yeye ambavyo amekuwa akieleza kwa vyombo vya usalama nchini Misri.

Waandishi wengine wa kituo hicho wanaoshikiliwa ni pamoja na Mohamed Fahmy mwenye uraia pia wa Canada pamoja na Baher Mohamed raia wa Misri ambao walikamatwa kwa pamoja mwaka 2013 wakituhumiwa kushirikiana na chama cha Muslim Brotherhood.

BOKO HARAM WAENDELEA KUWA TISHIO NCHINI NIGERIA SIKU KADHAA KABLA YA UCHAGUZI MKUU


Siku chache zikiwa zimesalia kabla ya wananchi wa Nigeria kufanya uchaguzi mkuu wa rais, hii leo nchi hiyo imeendelea kushuhudia mashambulizi mapya ya kundi la Boko Haram katika mji wa Maiduguri wakati huu vikosi vya Chad na Cameroon vikiungana na majeshi ya Nigeria kuwakabili wapiganaji hao.

Mwishoni mwa juma miji ya Borno na Maiduguri imeshuhudia mapigano makali kati ya wapiganaji wa Boko Haram na wanajeshi wa Serikali, ambapo majeshi ya serikali kwa kusaidiwa na raia walifanikiwa kudhibiti miji hiyo na kuwazuia wapiganaji hao kuichukua tena.

Wakati majeshi ya Chad na Cameroon yamefanya mashambulizi ya anga kwenye miji ya Gamboru na mashariki mwa mji wa Borno ambako wapiganaji hao wameelezwa kujipanga upya.

Kushuhudiwa kwa mapigano zaidi kati ya vikosi vya Serikali na wapiganaji hawa wa kiislamu, kumeendelea kutishia usalama wa nchi jirani pamoja na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika February 14 mwaka huu.

SALVAKIIR NA RIEK MASHAR WAKUBALIANA KWA MARA YA SABA KUSITISHA VITA


Baada ya miezi 13 ya mapigano na mara saba ya kutiliana saini mikataba ya kusitisha mapigano bila mafanikio, wanadiplomasia wa kimataifa wanaona kuwa kwasasa mkataba wowote wa amani utakaokubaliwa na viongozi wanaohasimiana nchini Sudan Kusini utakuwa bora katika kusaidia kutuliza mzozo wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa makubaliano ya hivi karibuni yaliyopendekezwa na viongozi wa nchi za IGAD mwishoni mwa juma mjini Addis Ababa, yatashuhudia rais Salva Kiir akisalia kuwa rais huku Dr Riek Machar akirejeshwa kwenye nafasi yake ya makamu wa rais nafasi aliyoishikilia mpaka mwezi July 2013 ambapo alikimbia.

Riek Machar na rais Salva Kiir Jumapili hii walikubaliana kutiliana saini mkataba wa kusitisha mapigano lakini wakashindwa kukubaliana namna ya kugawana madaraka kujaribu kumaliza mzozo wa kisiasa unaofukuta nchini humo.

Makubaliano haya yanajiri ikiwa yamepita majuma kadhaa toka watiliane saini makubaliano ya kuunganisha tena chama tawala cha SPLM, makubaliano yaliyosimamiwa na Chama tawala nchini Tanzania CCM

BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LATAKA KUACHIWA HURU KWA RUBANI WA JORDANIA


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetaka kuachiwa huru mara moja kwa mateka anayeshikiliwa na wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Islamic State, wakati huu utawala wa Jordan ukiapa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha raia wake anaachiwa na kundi hilo.

Juma hili baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mauaji ya raia mwingine wa Japan Kenji Goto na kukiita kitendo hicho cha kinyama huku kundi hilo likiapa kumuua ribani raia wa Jordan wanaemshikilia mateka.

Haya yanajiri ambapo mwishoni mwa juma serikali ya Jordan kupitia msemaji wake, Mohammad al Moman amesema Serikali yao iko tayari kubadilishana wafungwa na kundi hilo lakini kwanza wanataka hakikisho kuwa raia wao yuko hai.

lundi 12 janvier 2015

KISANDUKI CHEUZI CHA NDEGE YA AIRASIA CHAGUNDULIKA

Hatimae wapigambizi nchini Indonesia wamefaulu kukipata kisanduku cha ndege ya Malesia AirAsia ilioanguka katika bahari ya Java Desemba 28 iliopita ikiwa na habiria 162 ikiw an hatuwa muhimu katika juhudi za kutafuta mabaki ya ndege hiyo.

baada ya takriban majuma mawili ya shughuli za uokozi Mkurgenzi wa idara ya uokozi Bambang Soelistyo, hatimae kisanduku kinacho rikodi sauti cha ndege iliokuwa ikiunganisha Indonesia na Surabaya nchini Singapour kimepatikana na sasa wanajaribu kutafuta kifaa maalum kinachorikidi sauti ili kufaham zaidi kuhusu mawasiliano ya mwisho ya rubani wa ndege hiyo.

Kiongozi wa jeshi jenerali Moeldoko amesema kuna matumaini ya kupata kisanduku kingine na kifaa kinacho rikodi sauti hakiko mbali sana na eneo hilo. Jenerali huyo amesema matumaini haya yanakuja baada ya kuwepo kwa viashiria katika eneo hilo.

Mtaalamu mmoja wa kamati ya kitaifa ya usalama wa usafiri kimataifa Mardjono Siswosuwarno amesisitzz kwamba kisanduki hicho cheusi kilichopatikana kitasafirishwa hadi jijini Jakarta kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Ndege hiyo ya kampuni ya Malesia ilianguka desemba 28 muda mfupi baada ya kupaa angani eneo la Surabaya wakati ikielekea nchini Singapour.

Viongozi wa indonesia wanasema rubani wa ndege hiyo iliokuwa na habiri zaidi ya mia moja aliomba ruhusa ya kupaa juu zaidi kuepuka mawingi yaliokuwa tishio, lakini hakuweza kupjibiwa kutokana na mawasiliano kuwa mengi katika sekta hiyo, ambapo mawasiliano kati ya ndeger hiyo na idara ya uchunguzi yalitoweka muda mfupi baadae.

VIONGOZI WA ULAYA WASHINDWA KUAFIKIANA KUHUSU SWALA LA USALAMA

Mashambulizi ya kigaidi yaliotokea jijini paris nchini Ufaransa juma lililopita yamezua hisia tofauti kwa viongozi wa ulaya juu ya swala la kushirikiana katika kuzidisha ulinzi wa kuzuia kutokea kwa mashambulizi zaidi ya kigaidi katika bara la Ulaya.

Hata hivyo kumekuwa na hali ya kutoelwana kuhusu swala hili la kubadilisha taarifa katika ya mataifa ya bara la ulaya ambapo bunge la umoja wa ulaya linahofia kuwanyima haki ya kutembea wananchi kutoka katika maeneo hayo.

Miongoni mwa hatuwa hizo ni kurekebisha sheria za kusafiri katika eneo la Shengen, kufanya upekuzi zaidi kwa baadhi ya abiria, kuorodhesha katikas kitabu maalum wasafiri, kupeana taarifa za kijasusi kati ya mataifa ya Ulaya, kudhibiti matumizi ya mitandao ya Internet na kuzuia kuzagaa kwa silaha.


Hii si mara ya kwanza viongozi wa ulaya wanazungumzia kuhusu swala hili, lakini mara zote wameshindwa kukubaliana.

HALI YA TAHARUKI YATANDA JIJINI KINSHASA

Hali ya taharuki imeendelea kutanda jijini Kinshasa karibu na biunge la taifa nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako polisi ya usalama imeendelea kuewatawanya wafuasi wa upinzani wanaopinga mpango wa mageuzi ya sheria ya uchaguzi ambayo ilipangwa kujadiliwa bungeni hii leo.

upinzani nchini drcongo unaona kwamba mageuzi ya sheria hiyo ya uchaguzi yatachelewesha kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa rais utaompa nafasi rais wa sasa wa nchi hiyo Joseph Kabila madarakani tangu mwaka 2001 kuendelea kusalia uongozini baada ya kutamatika kwa muhula wake wa tatu na wa mwisho mwaka 2016.

polisi wa usalama wa raia wamezuia maeneo yote yanayoelekea kwenye majengo ya bunge la taifa nchini humo Palais du peuple ambako wabunge walipanga kujadili muswada wa sheria uhusuo mabadiliko ya sheria ya uchaguzi uliowasilishwa bungeni na serikali kwa ajili ya kujadiliwa katika kikao cha bunge mchana huu.

Katika taarifa ya awali wabunge wa upinzani waliafifu kwamba watasusia cikoa hivyo vya kufanya mageuzi katiba ya nchi hiyo katika kile walichokiita kuhofia kuwa wahaini.

Mapema leo asubuhi polisi wamewasambaratisha wafuasi wa upinzani takriban 300 hivi waliokuwa wamekusanyika karibu na ofisi za bunge kwa kutumia bomu za kutowa machozi, kabla ya kukimbilia kwenye ofisi za vyama vya upinzani hususan chama cha UNC cha Vital Kamerhe ambako kumeshuhudiwa mvutano wa polisi na vijana waliochoma moto magurudumu.

Israel Mutombo Msemaji wa kiongozi wa polisi nchini humo jenerali Celsstin Kanyama amesema wamekuhamasisha idadi kubwa ya polisi nchini na kwamba hawana habari yoyote kutoka serikali inayoruhusu kufanyika kwa maandamano.



KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...