Pages

jeudi 1 mars 2018

MBUNGE WA CGAMA CHA KANU NCHINI KENYA APENDEKEZA MABADILIKO YA MFUMO WA UTAWALA

Mbunge wa chama cha KANU nchini Kenya Kassait Kamket, amependekeza mswada bungeni unaolenga kubadilisha mfumo wa uongozi nchini humo kwa kuibadilisha Katiba.

Mswada huu iwapo utakubaliwa na wabunge, ina maana kuwa Katiba mpya ya Kenya iliyopatikana mwaka 2010, itafanyiwa mabadiliko makubwa.

Mbunge huyo anapendekeza kuundwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu atakayekuwa na madaraka makubwa lakini pia kuwepo kwa rais ambaye atakuwa ishara ya umoja wa kitaifa.

Iwapo marekebisho hayo yatafanyika, bunge la pamoja, lile la kitaifa na Senate litamchagua rais ambaye atakuwa na jukumu la kumteua Waziri Mkuu kutoka kwenye chama chenye wabunge wengi bungeni.

Waziri Mkuu atahudumu kwa muda wa miaka mitano kabla ya Uchaguzi mwingine kufanyika, huku rais ambaye ni lazima awe na zaidi ya miaka 50, akihudumu kwa muhula mmoja wa miaka saba.


MAELFU WAJITOKEZA KUAGA MUILI WA NYOTA WA FILAMU NCHINI INDIA SRIDEV KAPOOR

Maelfu ya mashabiki wamejitokeza huko Mumbai kwa ajili ya mazishi ya Sridevi Kapoor, muigizaji nyota wa filamu za Bollywood ambaye alipata ajali ya kuzama bafuni katika hoteli moja huko Dubai mwishoni mwa juma lililopita ambako alikuwa amekwenda kuhudhuria sherehe ya harusi ya mwipwa wake.

Makundi ya watu wamejitokeza jana Jumatano asubuhi ili kutoa kuheshimu zao za mwisho kwa muigizaji huyo nyota wa filamu mwenye umri wa miaka 54 kabla ya kufanyika kwa mazishi yake

Mwili wake uliwekwa kwenye kikapu cha kioo kilichofunikwa na bendera ya India wakati akipelekwa katika safari yake ya mwisho kwenda kwenye chumba cha kuchomwa moto huku mumewe Boney Kapoor akisimama karibu.

Siku ya Jumapili asubuhi, familia ya muigizaji huyo ilithibitisha kifo chake ambapo polisi nchini India ilizuia muili kwa ajili ya uchunguzi, na mwisho wa siku ikabainika kuwa aliza kwa ajali ndaniya bafu.

vendredi 23 février 2018

RAIS WA MAHAKAMA YA RUFAA MJINI GITEGA NCHINI BURUNDI NA JAJI WA MAHAKAMA HIYO WATIWA MBARONI

Thomas Ntimpirangeze
Thomas Ntimpirangeza, rais wa Mahakama ya rufaa mjini Gitega na Prime Habiyambere, jaji katika mahakama hiyo, wametiwa nguvuni hivi majuzi kufuatia waranti ya kukamatwa kwao kutoka kwa hakimu mkuu wa jamuhuri.


Wawili hao walikamatwa kwa nyakati tofauti, ambapo mmoja alikamatwa ofisini kwake huko Gitega, huku mwingine akikamatwa akiwa ziarani jijini Bujumbura. Wote wawili kwa sasa wamewekwa korokoroni katika jela kuu la Mpimba.


Taarifa za awali zilieleza kwamba wawili hao walikamatwa baada ya kumuacha huru mshukiwa wa wizi wa dheruji ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu, ambapo ilikuwa ni msaada kutoka Ikulu ya Rais.


Huku habari nyingine zikieleza kwamba rais Mahakama ya rufaa alikamatwa baada ya kurusha kwenye mitandasno ya kijamii kampeni ya kura ya hapana katika uchaguzi wa kura ya maoni ujao nchini Burundi.


Hata hivyo hakimu mkuu wa Jamuhuri Sylvestre Nyandwi anasema wawili hao wamekamatwa kwa makosa ya Rushwa huku akikanusha taarifa kwamba wawili gao wamekamatwa kutokana na kuendesha kampeni ya hapana.

HASIRA YATAWALA YATAWALA MJINI DAPCHI SIKU 4 BAADA YA KUTOKEWEKA KWA WASICHANA 111

Waziri wa habari nchini Nigeria Lai Mohamed
Siku nne baada ya kutokea kwa shambulio katika shule moja mjini Dapchi nchini Nigeria, kumekuwa na mkanganyiko mkubwa katika mji huo uliopo kaskazini mashariki mwa Nigeria ambako vikosi vya usalama vimekabiliana na wananchi wenye hasira ambao hadi sasa hawajuwi wapi walipo binti zao.

Polisi imethibitisha kuwa wasichana 111 wa shule la wasichana mjini Dapchi wametoweka tangu kutokea kwa shambulio la kundi la kijihadi la Boko Haram

hofu imeendelea kutanda katika eneo hilo ikihofiwa kutokea kwa Chibok mpya, jimbo lililopo jirani na mji wa Borno ambako kundi la Boko Haram liliwateka wasichana 276 April mwaka 2014, tukio lililolaaniwa ulimwengu mzima.

Ujumbe wa serikali ukiongozwa na waziri wa habari Lai Mohamed ulielekea katika eneo hilo na hivyo kuzua hasira miongoni mwa wananchi ambao wanasema hawajuwi nani wa kuwapa msaada.

Hivi majuzi watu wenye silaha walivamia mji huo na kusababisha mtafaruku mkubwa.

Waziri wa ulinzi nchini Nigeria Jenerali Mansour Dan Ali amesema wasichana wengi walikimbia kutokana na uoga na baadhi wameanza kurejea shuleni.

vendredi 23 juin 2017

SERIKALI YA BURUNDI YAKIUKA MASHARTI YA UMOJA WA ULAYA

Serikali ya Burundi inaelezwa kukiuka masharti ya kuchukuwa asilimia 20 ya mshahara wa wanajeshi wanaolinda amani nchini Somalia Amisom, kama ilivyokuwa imeafikiana na Umoja wa Ulaya. Mengi zaidi na Ali Bilali

Baada ya mvutano na hatimae kupatikana muafaka, Umoja wa Ulaya ulikubali kutoa malipo ya mshahara wa wanajeshi wa Burundi walipo katika kikosi cha Umoja wa Afrika wanaolinda amani nchini Somalia Amisom, baada ya kukubaliana masharti mawili na serikali ya Burundi.

Sharti la kwanza ilikuwa ni pesa hizo kutopitia kwenye Benki kuu ya taifa, badala yake ziwekwe kwenye akaunti ya benki binafsi, wakati sharti lingine ni serikali ya burundi kutokata asilimia 20 ya mshahara huo wa wanajeshi kama ilivyokuwa imezoeleka.

Umoja wa Ulaya umeanza kutoa pesa hizo tangu kipindi kadhaa, ambazo zinapitia kwenye benki binafasi kama ilivyoasfikiwa katika makubaliano na serikali ya Burundi, lakini wanajeshi wanaofaidi na hatuwa hiyo hata hivyo wamesema hakuna kilichobadilika.

Hata hivyo wazara ya ulinzi nchini Burundi ilikuwa imefahamisha awali kwamba wanajeshi wote walipo nchini Somalia, watapokea mishahara yao kupitia akaunti za ushirikiano wa kijeshi ama cooperative militaire ambazo jeshi linadhibiti kwa asilimia mia moja.

Duru za kidiplomasia zinaeleza kwamba Umoja wa Ulaya umekeisha lipa malimbikizo ya mwaka mzima ya wanajeshi hao ambao wao wanasema wamekewisha pokea malimbikizo ya mshahara wa miezi mitano pekee na bado wanakatwa asilimia 20

msemaji wa jeshi la Burundi Gaspard baratuza amesema wanajeshi wenyewe ndio waliokubali kuchangia wenyewe ili kusaidia kuendelea kwa harakati za kulinda amani nchini Somalia, jambo ambalo limepingwa vikali na wanajeshi

Umoja wa Ulaya haijazungumza lolote kuhusu swala hili nyeti na lenye utata.





RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME ALAANI SHAMBULIO LA RUSIZI

Rais wa Rwanda Paul Kagame, amebaini maskitiko yake kufuatia tukio la hivi karibuni katika eneo la Rusizi sekta ya Bugarama, ambako watu wenye silaha walishambulia na kusababisha mauaji ya mtu mmoja na kuwajeruhi wengine nane.

Taarifa zinaeleza kwamba washambuliaji waliingia katika baa moja katika kijiji cha Ryankana na kuanza kupigia risase wakifuatisha na guruneti, tukio ambalo msemaji wa polisi nchini Rwanda Rene Nkendabanga juma hili alieleza kwamba linafanana na tukio liliotkea miezi kadhaa iliopita ambapo watu kutoka Burundi waliashambulia na kusababisha mauaji kabla ya kutokomea.


Rais Kagame amesema matukio hayo hayawezi kuendelea, lazima yapatiwe suluhu la haraka.

vendredi 16 juin 2017

WANANCHI WA UINGEREZA WATAKA MAJIBU YA KINA KUHUSU CHANZO CHA MOTO ULIOGHARIMU MAISHA YA WATU 17

Wananchi wa Uingereza wameendelea kuonesha hasira zaid dhidi ya Serikali wakitaka majibu ya kina kuhusu chanzo kilichosababisha moto mkubwa kwenye jengo moja mwanzoni mwa juma hili ambapo watu 17 walipoteza maisha huku miili mingine ikishindikana kutambuliwa kutokana na kuungua vibaya.

Meya wa jiji la London Sadiq Khan alijikuta matatani baada ya kundi la wananchi kumvamia na kuhoji hatua gani zitachukuliwa dhidi ya wamiliki wa jengo hilo na wengine wakitaka majibu ya chanzo cha moto huo.

Waziri mkuu Theresa May tayari ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu chanzo cha moto huo pamoja na wamiliki wake kuhojiwa akiahidi hakuna atakayeachwa kwenye uchunguzi huo.

Juma hili jengo la Ghorofa 24 kwenye eneo la Grenfell liliwaka moto na kuziacha mamia ya familia zikiwa hazina mahali pa kuishi na wengine kupoteza ndugu zao.


KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...