Wakati
kukiwa na mswali chiungu nzima kuhusu maiti zilizo okotwa katika mto
Rweru kwenye eneo la mpaka wa burundi na Rwanda, kundi la watu
waliokuwa kwenye mitumbwi yenye kutumia injini, walivuka maji na
kujaribu kuiba miili ya watu waliozikwa upande wa Burundi majuma
matatu yaliopita.
Tukio
hili limekuja kuchochea moto zaidi wakati huu burundi na Rwanda
zimekuwa zikitupiana lawama kila mmooja akimtuhumu mwenzie kuhusika.
Watu
hao waliojaribu kuiba miili hiyo walishindwa kutekeleza azma yao
baada ya mlinzi wa mitiumbai upande wa burundi kuona mwanga wa Tochi
na haitimae kuanza kupiga kelele na hatimae watu hao wakakimbia huku
wakiacha vipao na mifuko ambayo viongozi wa serikali ya Burundi
wanasema mifuko hiyo ingeliwasaidia kuweka miili ya watu hao iwapo
wangelifaulu operesheni hiyo chafu.
Kutokana
na tukio hilo Rwanda imeanza kukodoleaa macho licha ya hapo awali
kukanusha kwamba watu hao hawakutoka nchini Rwanda, wakati huu
shinikizo limeongezeka kuzitaka pande mbili yaani Birindi na Rwanda
kuanzisha uchunguzi wa haraka kubaini watu hao ni kutoka Rwanda au
Burundi.