mercredi 18 février 2015
JESHI LA NIGERIA LAJIGAMBA KUWAUA BOKO HARAM WAKATI KUNDI HILO LIKITISHIA KUZUIA UCHAGUZI
Jeshi
la Nigeria linasema limewaua wanamgambo zaidi ya 300 wa Boko Haram
katika mji wa Monguno katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa
nchi hiyo.
Msemaji
wa jeshi Chris
Olukolade amesema licha ya kuwaua wanagambo hao imefanikiwa pia
kuwakamata baadhi yao.
Wakati
jeshi likisema hayo, kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekau
kupitia ujumbe wake mpya uliotolewa katika mkanda wa Video amesema
atahakikisha kuwa kundi lake linasambaratisha uchaguzi wa urais
uliopangwa kufanyika tarehe 28 mwezi ujao.
Tume
ya Uchaguzi nchini humo iliahirisha Uchaguzi huo baada ya jeshi
kusema kuwa halikuwa na uwezo wa kutoa ulinzi kwa wananchi wakati huo
na kuomba wiki sita kukabiliana na kundi hilo.
mardi 17 février 2015
MONUSCO YARIDHISHWA NA HATUWA YA SERIKALI YA DRCONGO KUONGOZA OPERSHENI YA KUWASAKA FDLR
Ujumbe
wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO
unapongeza dhamira ya serikali ya DRC kuchukua pekee jukumu la
kuwasaka waasi wa kihutu wa rwanda wa FDLR walioko Mashariki mwa nchi
hiyo kama alivyoamua rais Joseph Kabila.
Kaimu msemaji wa Ujumbe huo Umoja Charles Bambara amesema kuwa pamoja na kupongeza hatua hiyo, MONUSCO itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kutimiza agizo waliokabidhiwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kulingana
na Msemaji huyo, MONUSCO itaendelea kusaidia jeshi la Congo FARDC
katika shughuli nyingine za kijeshi dhidi ya vikundi vingine vyenye
kumiliki silaha mashariki mwa DRC ikiwa ni pamoja na Kivu ya
Kusini, Kivu kaskazini , Butembo, Katanga na mahali pengine.
Kauli hiyo haitofautiani na ile ya Msemaji wa Serikali ya Congo Waziri Lambert Mende ambaye hapo jana katika mkutano na waandishi wa habari amebainisha kuwa MONUSCO kutimiza wajibu wake bila ya kutegemea Jeshi la DRC dhidi ya makundi yote yenye kumiliki silaha kwa vile ni sehemu ya majukumu ya Ujumbe huo.
Kwa
upande wake, MONUSCO pia imeahidi kuendelea kutimiza wajibu wake
kama ilivyo azma ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika
shughuli nyingine za kijeshi kwa kushirikaiana na jeshi la DRC
amesema Charles Bambara.
lundi 16 février 2015
JESHI LA SERIKALI NA WAASI WATUHUMIWA KUTUMIA WATOTO WADOGO JESHINI
Mashirika
ya kutetea haki za binadamu nchini Sudan Kusini yanazituhumu mbande
mbili zinazokinzana nchini humo kusajili watoto wadogo walio na umri
wa chini ya miaka kuni na mitatu kushiriki kwenye vita ya wenyewe kwa
wenyewe, ripoti ambayo serikali ya Juba imekanusha vikali.
Ripoti
ya mashirika hayo, imedai kuwa Serikali inashiriki kikamilifu katika
kusajili vijana wadogo kujiunga na jeshi lake kwa hiari ama kwa
kuwalazimisha wakati waasi wao pia wanatumia watoto kama wanajeshi
katima vita vilivyodumu kwa zaidi ya miezi 14 hivi sasa.
Waziri
wa habari wa Sudan Kusini, Michael Makuei ametupilia mbali madai ya
ripoti hii akisisitiza kuwa jeshi lake bado lina nguvu ya kutosha
kupigana bila kutumia watoto.
SERIKALI YA DRCONGO YAKATAA KUSHIRIKIANA NA MONUSCO KATIKA OPERESHENI DHIDI YA FDLR
Serikali
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC imesema kuwa imekataa ombi
la tume ya Umoja wa mataifa nchini humo kushirikiana na jeshi lake
katika operesheni ya kuwasambaratisha wapiganaji wa kundi la FDLR, na
kutoa onyo dhidi ya taasisi za kimataifa kuingilia masuala yake ya
ndani.
Juma
lililopita, tume ya Umoja wa Mataifa ilitangaza kujiondoa katika
operesheni ya pamoja na jeshi la Serikali ya DRC, kushiriki
operesheni maalumu ya kuwasaka waasi wa Rwanda wa FDLR kwa kile umoja
wa mataifa unataka kwanza majenerali wawili wa juu wa jeshi la DRC
wafutwe kazi kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya ukiukwaji wa haki
za binadamu.
Waziri
wa habari na msemaji wa serikali ya DRC, Lambert Mende, amesema
serikali yake inakataa rasmi ombi la Umoja wa mataifa na kwamba
wanajeshi hao hawatafutwa kazi kwa shinikizo na kuzionya taasisi za
Umoja huo kutoingilia masuala yake ya ndani.
SAKATA LA KUWANIA MUHULA WA 3 KWA RAIS NKURUNZIZA LAIBUKA TENA
Chama
tawala nchini Burundi kimesisitiza kuwa Rais Pierre Nkrunzinza
atawania muhula wa tatu wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi June
mwaka huu, iwapo jina lake litapitishwa na chama kuwania nafasi hiyo.
Msimamo
huu wa chama tawala cha CNDD-FDD unatolewa wakati huu ambapo muungano
wa mashirika ya kiraia nchini Burundi yakitoa wito kwa rais
Nkurunzina kutowania muhula mwingine wa urais kuepusha kile
walichokiita machafuko nchini humo.
Msemaji
wa Rais, Willy Nyamitwe amesema kuwa rais Nkurunzinza atawania
kiti cha urais katika uchaguzi ujao iwapo kamati kuu ya chama
itamteua kufanya hivyo kulingana na katiba huku akiwaonya watu
wanaotaka kuchochea vurugu nchini humo.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa vyombo vya usalama pamoja na vyombo vya sheria vitawachukulia hatua wale wote ambao watabainika kupanga njama za kuchochea machafuko nchini humo kabla na hata wakati wa uchaguzi mkuu.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa vyombo vya usalama pamoja na vyombo vya sheria vitawachukulia hatua wale wote ambao watabainika kupanga njama za kuchochea machafuko nchini humo kabla na hata wakati wa uchaguzi mkuu.
Mashirika
ya kutetea haki za binadamu pamoja na mashirika ya kiraia zaidi ya
300 juma lililopita walianzisha kampeni maalumu ya kupinga hatua
yoyote ile ya kumuwezesha rais Nkurunzinza kuwania urais kwa muhula
wa tatu, jamabo ambalo wanasema iwapo litafanyika litakwenda kinyume
na katiba ya nchi.
jeudi 12 février 2015
MVUTANO KATI YA UN NA SERIKALI YA KINSHASA KUHUSU MA JENERALI 2 WAENDELEA
Msemaji
wa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo Monusco, Charles Bambara amesema Umoja wa Mataifa unafanya
mapunziko katika utoaji msaada kwenye maandalizi ya mashambulizi
dhidi ya kundi la waasi wa kihutu wa Rwanda waliopiga kambi mashariki
mwa DRCongo.
Hivi
majuzi akiwa jijini New York kiongozi mmoja wa umoja wa mataifa ambae
hakupenda jina lake litajwe alisema kwamba Umoja wa Mataifa
umesitisha kwa kuda utoaji msaada wake katika operesheni hiyo baada
ya kutokea mvutano baina ya monusco na serikali ya Kinshasa kuhusu
uteuzi wa ma jenerali wawili wa jeshi la FARDC na ambao wanatuhumiwa
na Umoja wa Matifa kuhusika katika makosa ya ukiukwaji wa haki za
binadamu.
umoja
wa Mataifa umesema kulingana na kanuni zake haziwaruhusu kushirikiana
na majenerali hao, huku kukiwa na taarifa kwamba Umoja wa Mataifa
umeipa makataa serikali ya DRCongo hadi Februari 13 kuhakikisha
maafisa hao wa kijeshi wamebadilishwa, la sivyo Monusco haitoshiriki
katika opersheni hiyo.
Tayari
serikali ya DRCongo imetupilia mbali makataa hayo kwa sababu maafisa
hao jenerali Bruno Mandevu na Sikabwe Fall hawana kesi yoyote ya
kujibu katika mahakama ya kijeshi.
Inscription à :
Articles (Atom)
KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?
Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...
-
Waziri wa sheria nchini Afrika Kusini Jeff Radebe Serikali ya Afrika Kusini imezungumzia kwa mara ya kwanza kuhusu mgogoro wa kidiplo...
-
Watu zaidi ya 20 wamejeruhiwa wawili wakiwa katikahali mbaya wakiwa ndani ya ndege bada ya ndege hiyo kupata hitilafu ambapo ilikuwa ik...
-
Wahanga wa mauaji ya ajali ya moto uliotokana na kuteketea kwa lori la mafuta katika kijiji cha Sange Mkoa wa Kivu ya Kusini kwenye um...















