Pages

mardi 11 mars 2014

OSCAR PISTORIUS ASHINDWA KUJIZUIA NA KUANZA KUTAPIKA WAKATI USHAHIDI UKIWASILISHWA MAHAKAMANI


Kesi ya mauji inayomkabili mwanariadha mwenye ulemavu wa miguu raia wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, imeingia wiki ya pili ambapo upande wa mashtaka umeendelea kuwasilisha ushahidi zaidi kuonesha mwanariadha huyo kumuua mchumba wake kwa makusudi.

Hapo jana mwendesha mashtaka alimwita kizimbani daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Reeva Steenkamp ambapo alielezea majeraha aliyokuwanayo mchumba wa Pistorius baada ya kushambuliwa kwa risasi hali iliyomfanya hata Oscar Pistorius kushindwa kujizuia na kuanza kutapika wakati ushahidi huo ukiwasilishwa.

Pistorius anatuhumiwa kupanga njama za kumuua mchumba wake tarehe 14 ya mwezi February usiku wa kuamkia siku ya wapendanao, ambapo jana pia ushahidi mpya ulitolewa kuonesha kuwa wapenzi hao walikuwa wameamka wote wakati wa tukio tofauti na maelezo ya Pistorius aliyoyatoa awali.

MGAWANYIKO WANUKIA KATIKA CHAMA CHA UPINZANI NCHINI ZIMBABWE.

Katibu mkuu wa Chama cha upinzani nchini Zimbabwe Tendai Binti

Katibu mkuu wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe MDC, Tendai Biti ameendelea kuvutana na mwenyekiti wake, Morgan Tsvangirai, safari hii akitaka kiongozi huyo kutoruhusiwa kuwemo wakati wa kikao cha kamati kuu ya chama kujadili suala la Elton Mangoma.

Mvutano huo ulianza kushuhudiwa toka juma lililopita punde tu baada ya tangazo la kamati ya utendaji kutangaza kumsimamisha kwa muda naibu mweka hazina Elton mangoma kufuatia matamshi yake ya kumtaka kiongozi wa chama hicho kuachia ngazi.

Lakini katika kile kinachoonekana kuwa bado kuna mgawanyiko ndani ya chama hichom hata katibu mkuu wake Tendai Biti anaonekana kutofautiana na mwenyekiti wake kuhusu kuruhusiwa kushiriki wakati wa mkutano wa kamati kuu ya chama.

Wachambuzi wa mambo wameonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa tofauti ndani ya chama hicho na kwamba kunatoa mwanya kwa chama tawala cha ZANU-PF kuendelea kujipatia umaarufu.

lundi 10 mars 2014

NINI KILICHOTOKEA SIKU YA JUMAMOSI MARCH 8 KATIKA OFISI ZA CHAMA CHA UPINZANI CHA MSD NCHINI BURUNDI?



 Polisi nchini Burundi iliendesha shambulizi mwishoni mwa juma lililopita katika makazi ya chama cha upinzani chga MSD kwa lengo la kuwakamata wafuasi wa chama hicho pamoja na mwenyekiti wake Alexis Sinduhije waliokuwa wamewateka polisi wawili.
Watu zaidi ya ishirini walijeruhiwa katika tukio hilo wakiwemo vijana wa chama hicho cha MSD pamoja na polisi watatu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Burundi, tukio hilo lilianza mapema asubuhi siku ya Jumamosi wakati vijana wa chama hicho waliokuwa wamevalia vitamba vya chama walipoluwa wakifanya mazoezi wakielekea mjini kati. Ghafla wakakumbana na polisi ambo waliwasambaratisha, na kuwakamata miongoni mwao ambao walipelekwa moja kwa moja katika jela kuu la Mpimba, huku wengine wakitimkia katika ofisi za chama cha MSD kusini mwa jiji kuu Bujumbura huku polisi ikuwafuata kwa kutumia bomu za kutowa machozi nao wakijibu kwa kurusha mawe.

Katika vurugu hizo polisi wawili walitekwa na vijana hao na kufungwa katika moja ya vyumba vya ofisi. Mwenyekiti wa chama cha MSD Alexis Sinduhije alitetea hatuwa hiyo na kudai kuwa vijana wamejihami baada ya polisi kuwashambulia kwa lengo la kuwauawa, na kuongeza kuwa kamata kamata ya watu kiholela lazima isitishwe, huku akikumbusha kuwa rais Nkurunziza hayupo juu sheria, na kwamba hawatokubali tena, watasimama hadi mwisho na ataendelea kusimama kidete akiwa huru au amekufa.

Shambulio

baada ya kuwateka nyara polisi hao, hali ilibadilika na kuanza kuwa mbaya. Alexis Sinduhije alilazimisha kuachiwa huru kwa wafungewa wa kisiasa kama vile El haj Hussein Rajabu , Frederic Bamvuginyuvira pamoja na wale wote ambao tayari wamemaliza robo ya kifungo kabla ya kuwaacha huru polisi hao.

Wakati huo polisi walikuwa wamekusanyika mbali kidogo na eneo hilo wakiwa na silaha. Ndani ya ofisi za chama, vijana wafuasi wa chama walikuwa wanaimba nyimbo za kukitukuza chama chao.
Saa kumi jioni, wanaharakati wa mashirika ya kiraia hususan mkuu wa chama kinacho tete haki za wafungwa APRODH Pierre Claver Mponimba alijaribu kuendesha usuluhishi kati ya Alexis Sinduhije na ma afisa wa Polisi bila mafaanikio. Alimtaka Sinduhije kuwaacha huru polisi hao ili kuepusha mashambulizi. Saa moja baadae wafuasi wa chama hicho walikubali kukabidhi silaha mbili walizokuwa nazo kutoka kwa polisi hao waliowashikilia mateka aina ya AK40 na kusalia na radio zao za mawasiliano.

Saa kumi na moja na nusu, polisi iliamuwa kuendesha shambulio kwa kutumia bomu za kawaida pamoja na za kutowa machozi, huku milio ya risase ikisikika kwa wingi na kudai kuwa vijana wa chama cha MSD ndio waliaonza kurusha risase. Baada ya muda wa zaa nzima za makabiliano, polisi walifaulu kuiteka ofisi hiyo, huku mwenyekiti wa chama Alexis Sinduhije na wafuasi wake wa karibu wakafaanikiwa kutoroka. Vijana kadhaa wa chama cha MSD walitiwa nguvuni, mateka hao polisi waliachiwa huku ofisi za chama hicho zikilindwa na polisi.

Picha kwa Idhni ya Gazeti la Iwacu


MKUU WA SERA ZA NJE KWENYE UMOJA WA ULAYA CATHERINE ASHTON AKIRI KUWA SAFARI BADO NDEFU KUFIKIA MAKUBALIANO YA NYUKLIA YA IRAN


Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya EU, Catherine Ashton, amekiri kuwa ziara yake nchini Iran haitoi hakikisho kuhusu kufikiwa makubaliano ya matumizi ya nyukilia ya taifa hilo.

Kwenye mkutano wake na wanahabari mjini Tehran punde baada ya kikao chake na waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, Mohammad Javad Zarif, Ashton amesema kuwa bado kunasafari ndefu ya kufikiwa suluhu kati ya nchi hiyo na mataifa ya magharibi.

Ziara ya Ashton mjini Tehran imekuja ikiwa imepita miezi kadhaa toka utawala wa Iran chini ya rais mpya, Hassan Rouhani utangaze nia yake ya kuwa na mazungumzo ya wazi kuhusu mpango wake wa nyuklia na mataifa ya magharibi na hatimaye kutia saini mkataba wa kuanza kutekeleza maazimio ya Umoja wa mataifa.

JESHI LA AMISOM LAITEKA MIJI KADHAA NCHINI SOMALIA




Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na vikosi vya Serikali ya Somalia wamefanikiwa kuikamata miji muhimu ya kusini mwa nchi hiyo iliyokuwa inakaliwa na wanamgambo wa Al-Shabab wenye uhisiano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda.

Miji ambayo imetwaaliwa toka kwenye mikono ya Al-Shabab ni ile iliyoko kwenye mpaka wa nchi hiyo na Ethiopia, ambayo ni mji wa Wajid na Hudur ambako waasi wa Al-Shabab walikuwa wamepiga kambi.

Wanajeshi wa AMISOM wamesema kuwa, wameanzisha operesheni maalumu toka juma lililopita kuwasaka wanamgambo hao kwenye miji ya kusini mwa nchi hiyo, operesheni inayotekelezwa ikiwa zimepita siku kadhaa toka wapiganaji wa Al-Shabab wafanye mashambulizi ya kujitoa muhanga mjini Mogadishu.

HOFU YA KUGAWANYIKA KWA CHAMA KIKUU CHA UPINZANI CHA MDC NCHINI ZIMBABWE YAZIDI KUTANDA


Hofu ya kushuhudiwa mgawanyiko zaidi ndani ya chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for democratic Change MDC, imeendelea kutanda wakati huu ambapo uongozi wa chama hicho ukiwataka viongozi waliochoka kuwemo ndani ya chama hicho kujiondoa wenyewe.

Msimamo wa chama hicho umetolewa mwishoni mwa juma na rais wake, Morgan Tsvangirai ambaye ameendelea kusisitiza kuwa hatoondoka madarakni kwa shinikizo la viongozi wachache wenye kutaka kumpindua.

Kauli ya Tsvangirai ameitoa ikiwa zimepita siku mbili tu, toka chama hicho kitangaze kumsimamisha kwa muda naibu mweka hazina wa chama hicho, Elton Mangoma kufuatia matamshi yake ya hivi karibu kumtaka kiongozi huyo kujiuzulu.

Mangoma sasa anasubiri uamuzi wa kamati ya nidhamu ya chama hicho ambayo itaketi hivi karibuni kuamua hatma yake.

VYAMA ZAIDI YA 30 VYAUNGANA NCHINI DRCONGO KWA AJILI YA UCHAGUZI WA 2016

Augustin Kikukama

 Vyama zaidi ya thelathini nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo vimeungana kwa lengo la kugombea kwenye uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika nchini humo mnamo mwaka wa 2016.

Akiwa na matumaini ya kupata ushindi kwenye uchaguzi Kuiongozi wa chama M17 Augustin Kikukama anasema kuwa wao wamejidhatiti kuhakikisha wanaiokoa nchi hiyo.

 Kwa Upande wake Waziri wa Habari akiwa pia msemaji wa serikali ya Kinshasa Lambert Mende, amesema hakuna haja ya kulalama kwani Raisi ameshathibitisha kwamba hawezi kwenda kinyume na katiba ya taifa hilo.

Lambert Mende


KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...