Pages

vendredi 23 juin 2017

SERIKALI YA BURUNDI YAKIUKA MASHARTI YA UMOJA WA ULAYA

Serikali ya Burundi inaelezwa kukiuka masharti ya kuchukuwa asilimia 20 ya mshahara wa wanajeshi wanaolinda amani nchini Somalia Amisom, kama ilivyokuwa imeafikiana na Umoja wa Ulaya. Mengi zaidi na Ali Bilali

Baada ya mvutano na hatimae kupatikana muafaka, Umoja wa Ulaya ulikubali kutoa malipo ya mshahara wa wanajeshi wa Burundi walipo katika kikosi cha Umoja wa Afrika wanaolinda amani nchini Somalia Amisom, baada ya kukubaliana masharti mawili na serikali ya Burundi.

Sharti la kwanza ilikuwa ni pesa hizo kutopitia kwenye Benki kuu ya taifa, badala yake ziwekwe kwenye akaunti ya benki binafsi, wakati sharti lingine ni serikali ya burundi kutokata asilimia 20 ya mshahara huo wa wanajeshi kama ilivyokuwa imezoeleka.

Umoja wa Ulaya umeanza kutoa pesa hizo tangu kipindi kadhaa, ambazo zinapitia kwenye benki binafasi kama ilivyoasfikiwa katika makubaliano na serikali ya Burundi, lakini wanajeshi wanaofaidi na hatuwa hiyo hata hivyo wamesema hakuna kilichobadilika.

Hata hivyo wazara ya ulinzi nchini Burundi ilikuwa imefahamisha awali kwamba wanajeshi wote walipo nchini Somalia, watapokea mishahara yao kupitia akaunti za ushirikiano wa kijeshi ama cooperative militaire ambazo jeshi linadhibiti kwa asilimia mia moja.

Duru za kidiplomasia zinaeleza kwamba Umoja wa Ulaya umekeisha lipa malimbikizo ya mwaka mzima ya wanajeshi hao ambao wao wanasema wamekewisha pokea malimbikizo ya mshahara wa miezi mitano pekee na bado wanakatwa asilimia 20

msemaji wa jeshi la Burundi Gaspard baratuza amesema wanajeshi wenyewe ndio waliokubali kuchangia wenyewe ili kusaidia kuendelea kwa harakati za kulinda amani nchini Somalia, jambo ambalo limepingwa vikali na wanajeshi

Umoja wa Ulaya haijazungumza lolote kuhusu swala hili nyeti na lenye utata.





RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME ALAANI SHAMBULIO LA RUSIZI

Rais wa Rwanda Paul Kagame, amebaini maskitiko yake kufuatia tukio la hivi karibuni katika eneo la Rusizi sekta ya Bugarama, ambako watu wenye silaha walishambulia na kusababisha mauaji ya mtu mmoja na kuwajeruhi wengine nane.

Taarifa zinaeleza kwamba washambuliaji waliingia katika baa moja katika kijiji cha Ryankana na kuanza kupigia risase wakifuatisha na guruneti, tukio ambalo msemaji wa polisi nchini Rwanda Rene Nkendabanga juma hili alieleza kwamba linafanana na tukio liliotkea miezi kadhaa iliopita ambapo watu kutoka Burundi waliashambulia na kusababisha mauaji kabla ya kutokomea.


Rais Kagame amesema matukio hayo hayawezi kuendelea, lazima yapatiwe suluhu la haraka.

vendredi 16 juin 2017

WANANCHI WA UINGEREZA WATAKA MAJIBU YA KINA KUHUSU CHANZO CHA MOTO ULIOGHARIMU MAISHA YA WATU 17

Wananchi wa Uingereza wameendelea kuonesha hasira zaid dhidi ya Serikali wakitaka majibu ya kina kuhusu chanzo kilichosababisha moto mkubwa kwenye jengo moja mwanzoni mwa juma hili ambapo watu 17 walipoteza maisha huku miili mingine ikishindikana kutambuliwa kutokana na kuungua vibaya.

Meya wa jiji la London Sadiq Khan alijikuta matatani baada ya kundi la wananchi kumvamia na kuhoji hatua gani zitachukuliwa dhidi ya wamiliki wa jengo hilo na wengine wakitaka majibu ya chanzo cha moto huo.

Waziri mkuu Theresa May tayari ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu chanzo cha moto huo pamoja na wamiliki wake kuhojiwa akiahidi hakuna atakayeachwa kwenye uchunguzi huo.

Juma hili jengo la Ghorofa 24 kwenye eneo la Grenfell liliwaka moto na kuziacha mamia ya familia zikiwa hazina mahali pa kuishi na wengine kupoteza ndugu zao.


RAIS WA MAREKANI AWAJIBU KWA HASIRA WALE WOTE WANAOMSAKAMA

Rais wa Marekani amewajibu kwa hasira wakosoaji wake baada ya kuchapishwa kwa ripoti kwenye gazeti la Washington Post ikieleza kuwa anachunguzwa na tume maalumu kuhusu kutaka kupindisha sheria katika kile alichokiita “utafutaji wa mchawi” unaoongozwa na watu wabaya dhidi yake.

Trump alikuwa akijibu tuhuma dhidi yake ambapo anadaiwa kuwa tayari uchunguzi rasmi umeanzishwa dhidi yake huku mwenyewe akikosoa namna ambavyo wakosoaji wake wamedhamiria kumlenga kwa tuhuma ambazo hazina msingi.

Licha ya kuwa rais Trump hakuzungumzia moja kwa moja tuhuma zinazomkabili, lakini akaeleza kuwa kinachoendelea hakijawahi kushuhudiwa kwenye historia ya Marekani kwa rais kushambuliwa kwa wakati mmoja.

Rais Trump amesema walitengeneza habari kuhusu kushirikiana na Urusi kwenye uchaguzi uliopita lakini hawakupata ushahidi na sasa wameamua kuchunguza kuhusu uwezekano wa kutaka kupindisha sheria.


Hata hivyo kamati inayochunguza sakata hili haijaweka wazi ikiwa kweli inamchunguza rais Trump.

WAFANYAKAZI WAWILI WA CICR WAACHIWA HURU MASHARIKI MWA DRCONGO

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu imesema kuwa wafanyakazi wake wawili waliotekwa nyara na kundi la watu wenye silaha mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo juma lililopita, wameachiwa huru.

Wafanyakazi hao walitekwa nyara Juni 7 katika eneo la kati ya mji wa Kirumba na Beni kaskazini mwa jimbo la Kivu Kaskazini wakati walipokuwa kwenye operesheni za kibinadamu, hatua iliyoilazimu kamati hiyo kusitisha huduma zake kwenye eneo hilo ikitaka kwanza wafanyakazi wake waachiwe.

Msemaji wa kamati hiyo Christine Cipolla amethibitisha kuachiwa kwa wafanyakazi wao na kuongeza kuwa wamepata ahueni lakini wanasikitishwa na kuendelea kuongezeka kwa vitendo vya utekaji nyara kwenye eneo la mashariki.

Kamati hiyo imesema kuwa makataa yake ya kuhudumia eneo la mashariki bado itaendelea ambapo ilikuwa ikihudumia zaidi ya familia elfu 5.


Eneo la Kivu Kaskazini kwa muda mrefu limekuwa kitovu na makazi ya wapiganaji wa Kihutu wa FDLR wa nchini Rwanda toka mwaka 1994 na limekuwa likiendesha vitendo vya utekaji nyara na kutatiza usalama mashariki mwa nchi hiyo.

HAKI ZA BINADAMU NCHINI BURUNDI HALI TETE, YASEMA RIPOTI YA TUME YA HAKI ZA BINADAMU YA UMOJA WA MATAIFA

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanasema kuwa vyombo vya usalama nchini Burundi na wapiganaji wanaoshirikiana na Serikali wameendelea kutekeleza vitendo vya mateso na kuua wapinzani, tuhuma ambazo zinakanushwa vikali na Serikali.

Wachunguzi hao kutoka tume ya umoja wa Mataifa iliyopewa jukumu la kuchunguza matukio ya ukiukwaji wa haki za Binadamu nchini Burundi walinyimwa kibali cha kuingia nchini humo ambapo wamesema kuna vitendo vingi vya ukiukaji wa haki za binadamo vinavyofanywa na Serikali na washirika wake.

Tume hiyo imesema kuwa baada ya kuwahoji zaidi ya raia 400 waliokimbia nchi yao, wamethibitisha pasipo na shaka hofu waliyokuwa nayo toka awali kuhusu vitendo vya unyanyasaji vinavyotekelezwa na Serikali ya Burundi.

Serikali ya Burundi kwa upande wake tayari imesema haikubaliana na matokeo ya uchunguzi wa kamati hii na kwamba imelenga kwa makusudi kutaka kuwapeleka maofisa kadhaa wa Serikali kwenye mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC.

Tume hii iliundwa mwaka 2016 ilipewa jukumu la kuchunguza na kuamua ikiwa kuna watu wanapaswa kuwajibishwa kutokana na tuhuma za ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu dhidi ya binadamu.



SERIKALI YA TANZANIA YALIFUNGIA GAZETI LA MAWIO KWA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI BAADA YA KUKIUKA SHERIA

Serikali ya Tanzania kupitia waziri wake wa habari Dr Harrison Mwakyembe imetangaza kulifungia gazeti la MAWIO kwa muda wa miaka miwili baada ya gazeti hilo kuchapisha habari iliyowahusisha marais wastaafu na ripoti ya madini iliyokabidhiwa kwa rais Magufuli Jumatatu ya wiki hii.

Juma hili rais Magufuli alivionya vyombo vya habari kuhusu kuwahusisha viongozi hao na taarifa za uchunguzi wa sakata la madini alizokabidhiwa ikulu.

Serikali inasema viongozi hao hawakutajwa popote kwenye ripoti ya uchunguzi na hivyo kuwahusisha na ripoti hizo ni kutaka kuwachafua viongozi hao.

Akitoa tangazo hilo mkurugenzi wa idara wa Idara ya Habari Maelezo, Dr Hassan Abbasi amesema hatua zilizochukuliwa zimezingatia sheria mpya ya huduma za habari.

Gazeti la MAWIO liliandika habari iliyoambatana na picha za marais wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete habari yenyewe ikiwahusisha viongozi hao na ripoti ya uchunguzi wa madini iliyowasilishwa kwa rais Magufuli.

jeudi 15 juin 2017

MTU MMOJA AUAWA WENGINE TISA WAJERUHIWA KWA GURUNETI JIJINI BUJUMBURA

Mtu mmoja ameuawa jana jioni jijini Bujumbura katika kata ya Musaga, baada wahalifu kuvurumisha guruneti iliowajeruhi pia watu kadhaa.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi nchini humo Pierre Nkurikiye, guruneti hiyo ilrushwa karibu na kituo cha mafuta majira ya saa kumi na mbili saa za Bujumbura na kusababisha kifo cha dereva mmoja wa gari huku watu wengine tisa wakijeruhiwa.


Inahofiwa idadi ya waliopoteza maisha kuongezeka kufuatia baadhiya majeruhi ambao walijeruhiwa vibaya.

WATU 6 WAPOTEZA MAISHBA KATIKA SHAMBULIO LA KUJITOA MUHANGA MJINI MOGADISHU

Watu sita wameripotiwa kufa na wengine mamia wamejeruhiwa baada ya mtu aliyejitoa muhanga kwa kutumia gari kulenga mgahawa mmoja maarufu ulioko mjini Mogadishu, Somalia wakati watu wakiwa wanakula futari.

Polisi mjini Mogadishu imethibitisha kutoke kwa tukio hilo ambalo imesema kuwa mtu aliyejitoa muhanga aliendesha gari lililokuwa na vilipuzi ndani ya jengo ambalo mgahawa wa Posh Treat ulikuwa umesheheni waumini wa dini ya kiislamu.

Afisa wa polisi Abukar Mohamed amethibitisha kuuawa kwa watu sita na wengine kadhaa kujeruhiwa na kuongeza kuwa operesheni ya kukagua jengo hilo imeendelea usiku kucha huku eneo lote la mgahawa huo likiwa limefungwa.

Kundi la Al-Shabab ambalo lina uhusiano na mtandao wa kigaidi wa AL-Qaeda kundi ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara mjini Mogadishu kuvilenga vikosi vya Serikali na vile vya kigeni, limekiri kuhusika kwenye shambulio hili.

Mara nyingi wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadan kundi la Al-Shaba limekuwa likizidisha mashambulizi yake nchini Somalia.


ICC YATAKA SEIF AL ISLAM AKAMATWE BAADA YA KUACHIWA JUMA LILILOPITA

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC ametoa wito wa kukamatwa na kujisalimisha kwa mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya marehemu kanali Muammar Gaddafi, Seif al-Islam aliyeachiwa juma lililopita kutoka kwenye gereza la Zintan alikokuwa anashikiliwa.

Mwendesha mashtaka Fatou Bensouda amesema kuwa hati ya kukamatwa kwa Seif al-Islam iliyotolewa na mahakama hiyo mwaka 2011 bado ni halali na viongozi wa Libya wanawajibika kumkamata licha ya msamaha wowote aliopewa nchini humo.

Seif al-Islam aliripotiwa kuachiwa huru Ijumaa ya wiki iliyopita na waasi wa eneo la Zintan, kundi ambalo lilikuwa likimshikilia kwa zaidi ya miaka mitano ambapo lilitangaza kumuachia huru kwa msamaha katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadan.

Hata hivyo ofisi ya mwendsha mashataka wa ICC iliyoko mjini Tripoli Libya ambako iko Serikali inayotambuliwa kimataifa, imesema kuwa msamaha huo hauwezi kumuhusu Seif al-Islam kwa sababu tu ya aina ya makosa anayotuhumiwa nayo.


Bensouda amesema Seif al-Islam anatakiwa na mahakama hiyo kwa tuhuma za makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na kwamba hivi sasa wanajaribu kujua mahali aliko.

WAKATI MZOZO WA QATAR NA NCHI ZA GHUBA UKIENDELEA MAREKANI YASAINI MKATABA WA KUIUZIA QATAR NDEGE ZA KIVITA

JIM MATTIS waziri wa Ulinzi wa Marekani
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu hapo jana amefanya mazungumzo na mfalme wa Qatar, mazungumzo ambayo yalilenga kuendelea kujaribu kutafuta suluhu kati ya nchi hiyo na mataifa mengine ya Ghuba wakati huu pia umoja wa Mataifa ukieleza kuguswa na hali inayoendelea.

Haya yanajiri wakati huu nchi ya Marekani kupitia kwa waziri wake wa mambo ya Kigeni Rex Tillerson akizikosoa nchi za Ghuba kwa kukitangaza chama cha Muslim Brotherhood kama kundi la kigaidi wakati kipo karibu kwenye nchi zote za Ghuba na baadhi ya wafuasi wake ni viongozi.

Miongoni mwa vikwazo vilivyotangazwa dhidi ya Qatar ni pamoja na nchi hiyo kutakiwa kuacha ufadhili wake kwenye chama cha Muslim Brotherhood.


Katika hatua nyingine waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis na mwenzake wa Qatar Khalid al-Attiyah wametiliana saini makubaliano ya nchi hiyo kuiuzia Qatar ndege za kivita zenye thamani ya dola bilioni 12.s

mardi 6 juin 2017

MSULUHISHI KATIKA MGOGORO WA BURUNDI BENJAMIN MKAPA AKIRI KUWEPO KWA CHANGAMOTO NYINGI KATIKA KUWALETA PAMOJA WANASIASA WA BURUNDI

Wakati mazungumzo ya kusaka amani nchini Burundi yakionekana kukwama, risala inayoonekana kuwa ya siri ya mratibu wa mazungumzo kwa viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki katika mkutano wa Mei 20, inatembea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Ali Bilali anatudokzea yaliomo kwenye hotuba hiyo.

Katika risala hiyo iliovuja, Benjamin Willima Mkapa ambae sio mara nyingi kuzungumzia shughuli zake katika mazungumzo ya Warundi, ametaja matatizo kadhaa anayo kabiliana nayo katika juhudi za kuwaleta pamoja wanasiasa wa Burundi.

Tangu kukabidhiwa jukumu zito la kuwaleta pamoja wanasiasa wa Burundi, mratibu wa mazungumzo Benjamin Mkapa, ameandaa vikao mara tatu mjini Arusha, vikao ambavyo havikuzaa matunda yoyote hadi sasa.

Mwaka mmoja tangu uteuzi huo msuluhishi katika mzozo huo hajafaulu kuzileta pamoja pande zote katika mgogoro wa Burundi, amekuwa akikutana nao kwa nayakati tofauti na ambapo wamekuwa wakimpa maoni ambayo inaonekana imekuwa vigumu kuyaweka pamoja.

Seriali ya Burundi inashikilia msimamo wake kwamba nchi ni tulivu, mazungumzo lazima yafanyike nchini Burundi na imeanza mchakato wa manadiliko ya katiba, jambo ambalo linatupiliwa mbali na upinzani unaodai kuwa usalama ni mdogo huku watu wakitiwa nguvuni kiholela, matukio ya utesaji, unyanyasaji, na watu wanaotoweka katika mazingira tatanishi.

Neno msuguano limerejea mara nyingi katika risala hiyo ambapo serikali imeelezwa kuwajibika katika kusuasua kwa mazungumzo hayo. Mratibu anawataka viongozi wa serikali kuonyesha dhamira ya dhati kwa kufuta waranti ya kukamatwa kwa viongozi wa upinzani na wa mahirika ya kiraia, kuwaacha huru wafungwa na kukubali kuzungumza na makundi yanayo shikilia silaha.

Katika kutamatisha risala hiyo ya siri, Benjamin Mkapa ameeleza ofisi yake imeathirika mara kadhaa na uvujishwaji wa taarifa. Na kukumbusha kwamba baadhi ya nyaraka huwasilishwa kwa sekretarieti ya jumuiya ya Afrika mashariki.



KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...