Pages

mercredi 18 novembre 2015

KENYA YATANGAZA MIKAKATI MIPYA YA UBANAJI MATUMIZI

Baada ya majuma kadhaa ya tuhuma mbalimbali za rushwa na matumizi mabaya ya fedha, Serikali ya Kenya imetangaza mikakati mipya ya ubanaji matumizi, ambapo imepiga marufuku safari na mafunzo yasiyo ya lazima kwa wafanyakazi wa umma.

Waziri wa fedha Henry Rotich amesema kuwa tayari ameshatoa waraka kwa maofisa wa wizara na vitengo mbalimbali vya uma, akipiga marufuku safari za nje na matumizi mengine yasiyo ya lazima.

Waziri Rotich amesema safari za mafunzo za ndani na zile za kaunti zimepigwa marufuku.


Hatua hii itasaidia Serikali ya Kenya kupunguza matumizi makubwa yanayolalamikiwa na upinzani pamoja na wananchi? Mwenzangu Victor Abuso amezungumza na James Shikwati mchambuzi wa masuala ya Uchumi akiwa jijini Mwanza nchini Tanzania.

vendredi 12 juin 2015

MUANDISHI WA HABARI WA RWANDA ATIWA NGUVUNI NCHINI BURUNDI KWA TUHUMA ZA UJASUSI


Hakimu mkuu wa jamhuri katika Mkoa wa Muyinga kaskazini mwa burundi metangaza kumtia nguvuni muandishi wa habari wa Rwanda kwa kosa la upepelezi baada ya kukutwa anafanya kazi mkaoni hapo bila kibali halali.

Hivi karibuni viongozi wa serikali ya Burundi wamepaza sauti kuhusu waandishi wa habari wa kigeni tangu kuanza kwa maandamano mwezi April kupinga umauzi wa rais Nkurunziza kuwani amuhula wa 3.

Etienne Besabesa Mivumbu ambae kulingana na kituo cha habari nchini Rwansa RNA alikuwa anafanya kazi katika kituo binafsi cha Izuba pamoja na mtandao wa Igihe.com.

Hakimu mkuu wa jamuhuri katika Mkoa huo ameeleza kwamba muandishi huyo wa habari alikamatwa akiwa na vifaa vya kunasa sauti pamoja na camera akiwa kwenye besketi akitokea nchini Rwanda katika tarafa ya Giteranyi, hivyo anatuhumiwa kufanyakazi ya kuchukuw ahabari bila kibali.

mercredi 10 juin 2015

IKULU YA RAIS BURUNDI YATHIBITISHA UCHAGUZI KUFANYIKA JULAY 15

Siku moja baada ya tume ya taifa ya uchaguzi nchini Burundi kupendekeza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge na ule wa urais, ikulu ya Bujumbura hii leo imethibitisha rasmi kuwa uchaguzi wa wabunge utafanyika June 29 na ule wa urais utafanyika July 15 kama ilivyopendekezwa na tume.

Kusogezwa mbele kwa uchaguzi huu kumeenda sambamba na maazimio ya wakuu wa nchi za Afrika Mashariki na kati ambao walitaka uchaguzi usogezwe mbele ili kupisha kufanyika kwa mazungumzo kati ya upinzani na Serikali ili kusaka muafaka kuhusu muhula watatu wa rais Pierre Nkurunziza.

Tangazo hili la ikulu linatolewa ikiwa ni siku moja tu imepita toka msemaji wa rais Nkurunziza atangaze kuwa suala la kuwania muhula wa tatu kwa rais Nkurunziza ni suala ambalo halina mjadala.



Tangazo hili la Serikali pia limetupilia mbali uwezekano mwingine wa kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu nchini humo kinyume na tarehe zilizotangazwa.

mardi 9 juin 2015

SERIKALI YA BURUNDI YASEMA HAKUNA MJADALA KUHUSU MUHULA WA 3 WA RAIS NKURUNZIZA

Licha ya upinzani na maandamano yanayoendelea kushuhudiwa nchini Burundi, Serikali ya Bujumbura inasema kuwa suala la rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu, ni suala ambalo halina mjadala, na kwamba kiongozi huyo hana nia ya kubadili uamuzi wake.

Akizungumza kwenye kituo kimoja cha redio, msemaji wa Serikali Philippe Nzobonariba, amesisitiza kuwa uamuzi wa rais Nkurunziza kuwania uongozi kwa muhula wa tatu, ni uamuzi ambao hauna mjadala, kauli inayozima kabisa madai ya upinzani ambao unataka rais Nkurunziza kutowania tena urais.

Philippe Nzobonariba, ameongeza kuwa mapendekezo yaliyotolewa na tume ya taifa ya uchaguzi kutaka kusogeza mbele baadhi ya chaguzi nchini humo, ni uamuzi wa mwisho na kwamba hata uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika July 15 huenda ukasogezwa mbele.


UPINZANI NCHINI BURUNDI WADAI KUUNDA TUME NYINGINE YA UCHAGUZI

Upinzani nchini Burundi umetupilia mbali pendekezo la kalenda ya uchaguzi iliowasilishwa na tume ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa bunge na ule wa rais na kutowa mashati kadhaa katika maandalizi ya uchaguzi huo.

Mmoja kati ya viongozi wa upinzani bwana Charles Nditije ameomba uundwa wa tume nyingine ya uchaguzi ambapo wajumbe wawili kati ya watano walijiuluzu na kuitoroka nchi.

Miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kuwapokonya silaha vijana wa chama tawala wa Imbonerakure na kumtaka rais kuachana na nia yake ya kuendelea kuwania muhula wa tatu ambao ndio chanzo cha vurugu zinazoendelea nchini humo.

Charles Nditije amesema hawawezi kuandaa uchaguzi wakati huu kabla hawaja kaa chini na kujadili kuhusu uundwaji wa tume nyingine ya uchaguzi, kama hawajadili kuhusu mazingira ya siasa na usalama wakati nchi ikielekea kwenye uchaguzi, kama hawajadili kuhusu kuwapokonya silaha wakereketwa wa chama tawala na kama Nkurunziza hatupilii mbali nia yake ya kuwani amuhula wa 3.

nditije aliyasema hayo muda mfupi baada ya tume ya uchaguzi kupendekeza kufanyika kwa uchaguzi wa Bunge juni 26, uchaguzi ambao hawali ulikuwa umepangwa kufanyika Mei 26 kabla ya kuahirishwa hadi Juni 5 na ule wa rais kufanyika Julay 15.

hapo jana waziri wa mambo ya ndani aliomba upinzani kuwasilisha majina ya watu wawili wataochukuw anafasi ya wajumbe 2 waliojiuzulu kwenye tume ya uchaguzi, lakini upinzani wao unadai iundwe tume nyingine na sio hii iliopo..


Upinzani nchini Burundi umetupilia mbali pendekezo la kalenda ya uchaguzi iliowasilishwa na tume ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa bunge na ule wa rais na kutowa mashati kadhaa katika maandalizi ya uchaguzi huo.

Mmoja kati ya viongozi wa upinzani bwana Charles Nditije ameomba uundwa wa tume nyingine ya uchaguzi ambapo wajumbe wawili kati ya watano walijiuluzu na kuitoroka nchi.

Miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kuwapokonya silaha vijana wa chama tawala wa Imbonerakure na kumtaka rais kuachana na nia yake ya kuendelea kuwania muhula wa tatu ambao ndio chanzo cha vurugu zinazoendelea nchini humo.

Charles Nditije amesema hawawezi kuandaa uchaguzi wakati huu kabla hawaja kaa chini na kujadili kuhusu uundwaji wa tume nyingine ya uchaguzi, kama hawajadili kuhusu mazingira ya siasa na usalama wakati nchi ikielekea kwenye uchaguzi, kama hawajadili kuhusu kuwapokonya silaha wakereketwa wa chama tawala na kama Nkurunziza hatupilii mbali nia yake ya kuwani amuhula wa 3.

Nditije aliyasema hayo muda mfupi baada ya tume ya uchaguzi kupendekeza kufanyika kwa uchaguzi wa Bunge juni 26, uchaguzi ambao hawali ulikuwa umepangwa kufanyika Mei 26 kabla ya kuahirishwa hadi Juni 5 na ule wa rais kufanyika Julay 15.

Hapo jana waziri wa mambo ya ndani aliomba upinzani kuwasilisha majina ya watu wawili wataochukuw anafasi ya wajumbe 2 waliojiuzulu kwenye tume ya uchaguzi, lakini upinzani wao unadai iundwe tume nyingine na sio hii iliopo..


lundi 4 mai 2015

WATU WAWILI WAUAWA KATIKA MASHINDANO YA KUCHORA VIBONZO VYA MTUME MUHAMAD JIJINI TEXAS


Watu wawili wanaodaiwa kuwa huenda walikuwa wamebeba mabomu wameuawa kwa kupigwa risasi, na polisi mmoja kujeruhiwa nje ya ukumbi ambao kulikuwa kunafanyika mashindano ya kuchora kikaragosi cha Mtume Muhammed mjini Texas, Marekani.

Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo kutoka taasisi ya Marekani ya kulinda uhuru wa kutoa maoni, wamesema kuwa watu hao waliuawa baada ya kurusha risasi kuelekea sehemu ambayo shindano hilo lilikuwa linafanyika na ndipo polisi walipolazimika kutumia nguvu kuwakabili.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hili, wanasema kuwa wakati shindano hilo likiendelea, watu wawili waliokuwa na silaha na vifaa vinavyodaiwa kuwa ni mabomu walianza kusogea kwenye eneo la tukio na kabla ya kufika waliwafyatulia risasi polisi walipkuwa jirani na kuwalenga baadhi ya watu waliohudhuria kabla ya kuuawa na kikosi maalumu cha Polisi wanajeshi.

Polisi mjini Texas wanasema wanaendelea kufanya uchunguzi kubaini sababu iliyowafanya watuhumiwa hao kuwafyatulia risasi waandaaji wa shindano hilo, ingawa baadhi ya watu wamewakosoa watu walioandaa shindano hilo wakijua fika kuwa lazima lingewakera baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu.

Waumini wa dini ya kiislamu wamelaani shambulio hili lakini wakawakosoa waandaaji wa shindano hilo ambalo mshindi alizawadia dola za Marekani elfu 10 kwa kuchora kibonzo wa kinachomuonesha Mtume Muhammad.

Tukio hili linajiri ikiwa ni miezo michache tu imepita toka kushambuliwa kwa ofisi za gazeti la Charlie Hebdo nchini Ufaransa ambalo lilichapisha kibonzo cha mtume Muhammed, ambapo watu wenye silha waliwashambulia wafanyakazi wake na kuua watu 16.

MAANDAMANO YASHUHUDIWA TENA JIJINI BUJUMBURA KULAANI MUHULA WA 3 WA RAIS NKURUNZIZA

Waandamanaji wamerejea barabarani katika baadhi ya mitaa za manispaa ya jiji la Bujumbura mapema leo asubuhi baada ya Makataa ya saa 48 yaliyotolewa na waandamanaji nchini Burundi kumpa nafasi Rais Nkurunziza kufikiria upya uamuzi wake wa kugombea muhula wa tatu kinyume na katiba na azimio la Arusha kufikia mwisho.

Taarifa kutoka Bujumbura zaeleza kuwa waandamanaji katika mitaa ya Buterere, Musaga, Nyakabiga, Bwiza wamechoma ma tyri barabarani huku katika tarafa ya buterere risase zikisikika kwa wingi, na huko Kinama vipeperushi vimesambazwa vinavyo wartia hofu waandamanaji kwamba ataeandamana basi watakiona cha moto

Tangu kuanza kwa maandamano hayo April 26 mwaka huu, watu 10 wameuawa wakati wa maandamano na ambapo shughuli za mazishi kwa baadhi ya wahanga hao zikifanyika hapo jana ambapo rais wa zamani wa Burundi Domitien Ndayizeye alisisitiza kuheshimiwa kwa katiba ya nchi.


Wakati hayo yakijiri, Mkuu wa jeshi nchini humo, Jenerali Prime Niyongabo akisoma tangazo maalum la jeshi, amerejelea kauli ya waziri wa Ulinzi Nchini Humo Brigadia Jenerali Pontien Gaciyubwenge siku ya jumamosi, ambapo amelisifu jeshi nchini humo kwa weledi wake katika kipindi chote cha maandamano hayo na kulionya kutokuwa na upande wowote.

Wataalamu wanaona kwamba taarifa ya jeshi ya kutaka viongozi kuheshimu katiba na mkataba wa Arusha ni ujumbe wa moja kwa moja kwa rais Nkurunziza ambae kulingana na Upinzani na wanaharakati wa mashirika ya kirai, anataka kuvunja makubaliano ya Arusha.

Kumekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na hali inayoendelea nchini Burundi wakati huu polisi ikiendelea kuwatisha raia kutoandamana, jambo ambalo linalowafanya raia kuwoana polisi kama adui.


Jumuiya ya Kimataifa imeonya Burundi kuhusu hali inayoendelea kushuhudiwa nchini humo na kwamba iwapo hatua hazitachukuliwa mapema huenda taifa hilo likaingi kwenye machafuko.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...