Mfalme
Goodwill Zwelithini wa jamii ya waZulu nchini Afrika kusini
aliyetuhumiwa kuwa chanzo cha vurugu dhidi ya wageni amekanusha
kuhusika kwake na matukio hayo.
Katika
mkutano wa hadhara Zwelithini amekanusha kuhusika katika vurugu hizo
na kudai kuwa ametafsiriwa vibaya baada ya kauli yake ya kuomba
wageni kufungasha virago na kuondoka nchini humo.
Mkutano wa dharura wa viongozi wa kijadi nchini humo akiwepo mfalme huyo pamoja na mkutano baina yake na mawaziri wa Mambo ya Ndani na wa Usalama yaonekana kuwa chachu ya kukomesha mashambulizi hayo ambapo Mfalme Zwelithini amesema kuwa mashambulizi dhidi ya wageni ni aibu kubwa kwa taifa.
Serikali
ya Marekani imelaani jana machafuko ya ubaguzi dhidi ya wageni
yanayoshuhudiwa nchini Afrika Kusini na kuwatolea wito viongozi wa
nchi hiyo kuchukuwa hatuwa madhubuti kukomesha mashambulizi dhidi ya
wageni.
Machafuko
hayo yaliwalenga raia wa kigeni waishio nchini Afrika Kusini na
kusababisha vifo vya watu 7 na maelfu wengine kukimbia katika miji ya
Durban na Johanesbourg.
Msemaji
wa wizara ya mambo ya nje Marie Harf amesema Marekani kama vile
mataifa mengine pamoja na mashirika ua kiraia wanalaani vikali mauaji
dhidi ya wageni yanayo shuhudia nchini Afrika Kusini.
Hayo
yanajiri wakati huu mataifa kadhaa barani Afrika yakiendelea
kujiandaa kuwarejesha nyumbani raia wake waishio nchini Afrika
Kusini. Miongoni mwa mataifa hayo ni pamoja na, Malawi, Msumbiji,
Zambia, Zimbabwe na Tanzania.