Pages

lundi 12 mars 2018

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwaunganisha warundi baada ya miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo maelefu ya watu walipoteza maisha huku wengine wakilazimika kutoroka makwao.

Matumaini yalianza kufifia tangu pale chama hicho kilipofanya mageuzi na kumuondoa aliekuwa kinara wa chama hicho Al Haj Hussein Radjabu katika kongamano ambalo lilichukuliwa na wengi kuwa halikuwa halali.


Mageuzi kadhaa yamekuwa yakifanyika ndani ya chama, bila hata hivyo kujali wapi chama hicho kimetoka na nini ilikuwa agenda ya chama, kiasi kwamba kila anaehoji anakuwa aduwi wa chama.

Wafuasi wengi wa chama wametoweka katika mazingira tatanishi kutokana na misimamo yao kutoleweka, huku wengine wakufaulu kutimka.

Pierre Nkurunziza ambae mwanzoni kabisa alifanya mabadiliko na kuunda nafasi ya mkuu wa wazee wa Busara, sasa ameunda nafasi na kiongozi wa juu, hatuwa itayonfanya asalie kuwa kiongozi maisha.

Nini anacholenga hapa? na je atafaulu azma yake?

Je huu ndio ule msemo wake amekuwa akisema kila mara kwamba mchezo wa ndani? Tusibiri tuone.

UPINZANI NCHINI DRCONGO WAJADILI KUHUSU MUSTAKABALI WA UCHAGUZI HUKO A. KUSINI

Makundi ya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamemuunga mkono kiongozi aliye uhamishoni Moise Katumbi, hatua iliyofikiwa katika mazungumzo yaliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Johannesburg, Afrika Kusini.


Mazungumzo haya ya mwishoni mwa juma yaliyowakutanisha wanasiasa wa upinzani kutoka nchini DRC, yalilenga kuunda muungano utakaosimama kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Katumbi aliongoza mamia ya wanasiasa wa upinzani katika mkutano wa siku 3 jijini Johannesburg kutengeneza mkakati watakaoutumia wakati wa uchaguzi mkuu wa Desemba 23 kuchukua nafasi ya rais Joseph Kabila anaemaliza muda wake.

Wanasiasa waliohudhuria mkutano huu wameonesha wazi kumuunga mkono gavana wa zamani wa eneo la Katanga Moise Katumbi kusimama kama mgombea wa muungano wa upinzani kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

Katumbi amesema anaamini muungano wao utakuwa silaha tosha ya kuleta mabadiliko ya kidemokrasia nchini mwao, kauli ambayo imeonekana kuungwa mkono na baadhi ya nchi za Ulaya zinazoshinikiza kufanyika kwa uchaguzi wa mapema.


WATU 16 WAPIGWA NA RADU NCHINI RWANDA

Takriban watu 16 wameuawa kwa kupigwa na radi siku ya Jumamosi kusini mwa Rwanda katika kanisa la wasabato, aifsaa mmoja wa eneo hilo ameeleza hapo jana Jumapili.

Meya wa Wilaya ya Nyaruguru Habitegeko Francois aliiambia shirika la habari la Ufaransa AFP kupitia njia ya simu kwamba watu 14 walikufa mara moja na wawili waliopoteza maisha baadae.


Watu wengine 140 wamejeruhiwa na kupelekwa haraka hospitalini na vituo vya afya, na madaktari wanasema watatu wao walikuwa katika hali mbaya lakini sasa wameanza kupata ahueni na wameruhisiwa kurejea nyumbani.


Kwa mujibu wa taarifa za meya, tukio kasma hilo lilitokea Ijumaa katika eneo moja ambalo radi ilipiga kundi la wanafunzi 18, na kuua mmoja kati yao.



WATU 14 NDIO WALIOUWA KWAMUJIBU TUME YA HAKI ZA BINADAMU NCHINI DRCONGO

Tume inayofanya uchunguzi kuhusu matukio ya Desemba 31 mwaka 2017 na Januari 22 mwaka 2018 wakati wa maandamano nchini DRCongo, imesema jumla watu 14 walipoteza maisha 7 ikiwa ni wakati wa maandamano yaliotishwa na kanisa katoliki kupinga utawala wa rais Joseph Kabila.

Takwimu hizo zimetolewa Jumamosi March 10 na waziri wa haki za binadamu nchini DRCongo Marie Ange Mushobekwa alieambatana na ripota wa tume hiyo Georges Kapiamba ambae anawakilisha mashirika ya kiraia na kukubaliana kuhusu takwimu hiyo.

Takriban Waathirika na mashuhuda 122 walikubali kujibu wito uliotolewa na tume ambapo watu 14 waliuawa, 12 kwa risase na wengine 2 kwa moshi wa bomu za kutoa machozi huku wengine 65 wakijeruhiwa na wengi kwa risase.

Wakati huo huo tume hiyo imesema watu zaidi 40 walikamatwa na kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji katika matukio ya Desemba 31 mwaka 2017 na januari 21 mwaka 2018.


NKURUNZIZA KUTAWALA CHAMA CHA CDD-FDD MILELE

Chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD mwishoni mwa juma kimemtangaza rais Pierre Nkurunziza kuwa kiongozi wa juu wa chama, hatua inayomfanya awe kiongozi wa maisha katika mkutano wa viongozi wa juu uliofanyika katika tarafa ya Buye anakotoka rais huyo.

Licha ya taarifa ya chama hicho iliyotolewa mwishoni mwa juma kutoeleza kwa kina kuhusu nafasi mpya waliyompa Nkurunziza, lakini ni wazi sasa kiongozi huyo anafanywa kuwa mtawala wa maisha, hatua inayozidisha sintofahamu zaidi kwenye siasa za nchi hiyo.


Haijafahamika ikiwa kutakuwa na marekebisho mengine ya katiba tofauti na yale yanayotarajiwa kupigiwa kura mwezi Mei mwaka huu ambapo ikiwa yataidhinishwa yatamruhusu kuwania urais kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 na kumfanya abaki madarakani hadi mwaka 2034.

Hata hivyo kumekuwa na mitazamo tofauti kuhusu hatuwa hiyo ambayo licha ya kuchukuliwa baadhi ya wafuasi wa chama wamenong'ona kuwa itakuwa ngumu kutekelezwa kwa hatuwa hiyo.

Chama hicho kimeahidi kutoa maelezo kuhusu cheo hicho na nini kitabadilika.

Evariste Ndayishimiye katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD amesema hakuna anaeweza kujifananisha na Pierre Nkurunziza katika chama hicho.

Wanasiasa wengi wa upinzani wamekosoa hatuwa hiyo ya chama tawala na kueleza kwamba kinataka kumfanya Nkurunziza kuwa kama Bokasa.

jeudi 1 mars 2018

WANAJESHI WAWILI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA NA MAHAKAMA YA GITEGA HUKO BURUNDI

Wanajeshi wawili wahukumiwa kifungo cha maisha jela, na kutakiwa kulipa faini ya franka za Burundi milioni 15 na miaka 20 ya kazi za umma kwa kosa la kumuuawa Evariste Ngenzi aliekuwa kiongozi wa chama tawala Mkoani Gitega.

Wanajeshi wawili na mwanamke mmoja anaedaiwa kuwa ndie aloiongoza mauaji hayo wamehukumiwa jana na mahakama kuu ya mjini Gitega.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya Usalama wahusika wa mauaji ni wanajeshi wawili na mwanamke mmoja.

Muathirika aliuawa katika mji wa Mutoyi, katika tarafa ya Bugendana mkoani Gitega Februari 26.




MKURUGENZI WA MASWASILIANO OFISI YA RAIS TRUMP HOP HICKS AJIUZULU

Mkurugenzi wa mawasiliano ofisi ya rais wa Marekani Donald Trump Hope Hicks ajiuzulu na kuwa mtu wa tano kujiuzulu katika uadhifa huo kwa kipndi cha mwaka mmoja.

Hope Hicks alikuwa miongoni mwa watu waaminifu kwa rais Trump, ambapo amefanya naye kazi kwa kipindi kirefu kabla ya kuwa rais. Mwanadada huyo asieongea sana alisikilizwa hivi majuzi kuhusu mkasa wa Urusi kuingilia uchaguzi wa urais nchini Marekani.


Mpaka sasa haijulikani nini sababu za kujiuzulu kwa mwanadasa huyo kutoka Ikulu ya White House na ambaye anafikisha idadi ya watu 5 ambao wameshajiuzulu kwenye uadhifa huo kwa kipindi cha miezi 13

MBUNGE WA CGAMA CHA KANU NCHINI KENYA APENDEKEZA MABADILIKO YA MFUMO WA UTAWALA

Mbunge wa chama cha KANU nchini Kenya Kassait Kamket, amependekeza mswada bungeni unaolenga kubadilisha mfumo wa uongozi nchini humo kwa kuibadilisha Katiba.

Mswada huu iwapo utakubaliwa na wabunge, ina maana kuwa Katiba mpya ya Kenya iliyopatikana mwaka 2010, itafanyiwa mabadiliko makubwa.

Mbunge huyo anapendekeza kuundwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu atakayekuwa na madaraka makubwa lakini pia kuwepo kwa rais ambaye atakuwa ishara ya umoja wa kitaifa.

Iwapo marekebisho hayo yatafanyika, bunge la pamoja, lile la kitaifa na Senate litamchagua rais ambaye atakuwa na jukumu la kumteua Waziri Mkuu kutoka kwenye chama chenye wabunge wengi bungeni.

Waziri Mkuu atahudumu kwa muda wa miaka mitano kabla ya Uchaguzi mwingine kufanyika, huku rais ambaye ni lazima awe na zaidi ya miaka 50, akihudumu kwa muhula mmoja wa miaka saba.


MAELFU WAJITOKEZA KUAGA MUILI WA NYOTA WA FILAMU NCHINI INDIA SRIDEV KAPOOR

Maelfu ya mashabiki wamejitokeza huko Mumbai kwa ajili ya mazishi ya Sridevi Kapoor, muigizaji nyota wa filamu za Bollywood ambaye alipata ajali ya kuzama bafuni katika hoteli moja huko Dubai mwishoni mwa juma lililopita ambako alikuwa amekwenda kuhudhuria sherehe ya harusi ya mwipwa wake.

Makundi ya watu wamejitokeza jana Jumatano asubuhi ili kutoa kuheshimu zao za mwisho kwa muigizaji huyo nyota wa filamu mwenye umri wa miaka 54 kabla ya kufanyika kwa mazishi yake

Mwili wake uliwekwa kwenye kikapu cha kioo kilichofunikwa na bendera ya India wakati akipelekwa katika safari yake ya mwisho kwenda kwenye chumba cha kuchomwa moto huku mumewe Boney Kapoor akisimama karibu.

Siku ya Jumapili asubuhi, familia ya muigizaji huyo ilithibitisha kifo chake ambapo polisi nchini India ilizuia muili kwa ajili ya uchunguzi, na mwisho wa siku ikabainika kuwa aliza kwa ajali ndaniya bafu.

vendredi 23 février 2018

RAIS WA MAHAKAMA YA RUFAA MJINI GITEGA NCHINI BURUNDI NA JAJI WA MAHAKAMA HIYO WATIWA MBARONI

Thomas Ntimpirangeze
Thomas Ntimpirangeza, rais wa Mahakama ya rufaa mjini Gitega na Prime Habiyambere, jaji katika mahakama hiyo, wametiwa nguvuni hivi majuzi kufuatia waranti ya kukamatwa kwao kutoka kwa hakimu mkuu wa jamuhuri.


Wawili hao walikamatwa kwa nyakati tofauti, ambapo mmoja alikamatwa ofisini kwake huko Gitega, huku mwingine akikamatwa akiwa ziarani jijini Bujumbura. Wote wawili kwa sasa wamewekwa korokoroni katika jela kuu la Mpimba.


Taarifa za awali zilieleza kwamba wawili hao walikamatwa baada ya kumuacha huru mshukiwa wa wizi wa dheruji ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu, ambapo ilikuwa ni msaada kutoka Ikulu ya Rais.


Huku habari nyingine zikieleza kwamba rais Mahakama ya rufaa alikamatwa baada ya kurusha kwenye mitandasno ya kijamii kampeni ya kura ya hapana katika uchaguzi wa kura ya maoni ujao nchini Burundi.


Hata hivyo hakimu mkuu wa Jamuhuri Sylvestre Nyandwi anasema wawili hao wamekamatwa kwa makosa ya Rushwa huku akikanusha taarifa kwamba wawili gao wamekamatwa kutokana na kuendesha kampeni ya hapana.

HASIRA YATAWALA YATAWALA MJINI DAPCHI SIKU 4 BAADA YA KUTOKEWEKA KWA WASICHANA 111

Waziri wa habari nchini Nigeria Lai Mohamed
Siku nne baada ya kutokea kwa shambulio katika shule moja mjini Dapchi nchini Nigeria, kumekuwa na mkanganyiko mkubwa katika mji huo uliopo kaskazini mashariki mwa Nigeria ambako vikosi vya usalama vimekabiliana na wananchi wenye hasira ambao hadi sasa hawajuwi wapi walipo binti zao.

Polisi imethibitisha kuwa wasichana 111 wa shule la wasichana mjini Dapchi wametoweka tangu kutokea kwa shambulio la kundi la kijihadi la Boko Haram

hofu imeendelea kutanda katika eneo hilo ikihofiwa kutokea kwa Chibok mpya, jimbo lililopo jirani na mji wa Borno ambako kundi la Boko Haram liliwateka wasichana 276 April mwaka 2014, tukio lililolaaniwa ulimwengu mzima.

Ujumbe wa serikali ukiongozwa na waziri wa habari Lai Mohamed ulielekea katika eneo hilo na hivyo kuzua hasira miongoni mwa wananchi ambao wanasema hawajuwi nani wa kuwapa msaada.

Hivi majuzi watu wenye silaha walivamia mji huo na kusababisha mtafaruku mkubwa.

Waziri wa ulinzi nchini Nigeria Jenerali Mansour Dan Ali amesema wasichana wengi walikimbia kutokana na uoga na baadhi wameanza kurejea shuleni.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...